Asilimia 61 ya Pombe zinazonywewa Tanzania ni haramu

Asilimia 61 ya Pombe zinazonywewa Tanzania ni haramu

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Biashara haramu ya pombe ina athari nyingi na za kina, ikiathiri uchumi wa Tanzania, uwekezaji, na pia kuhatarisha afya ya jamii kwa kiwango kikubwa.

Akifanya Mahojiano na Mwananchi, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Breweries Limited (TBL), Michelle Kilpin, alitoa tathmini yake kuhusu hali ya sasa ya pombe haramu nchini.

Alisema, “Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Euromonitor umebaini kuwa asilimia 61 ya pombe yote inayotumiwa Tanzania ni haramu.”

Aliongeza kuwa hali hii ina athari nyingi, ikiwemo upotevu wa mapato ya kodi unaofikia takriban shilingi trilioni 1 kila mwaka. Aidha, pombe haramu mara nyingi huwa na ubora duni na haina udhibiti, jambo linalosababisha hatari kubwa kwa afya ya umma na kuongeza mzigo katika mfumo wa huduma za afya.

Kwa upande wa sekta ya viwanda, alieleza kuwa hali hii inaleta ushindani usio wa haki, kwani wauzaji wa pombe haramu hukwepa kodi, hivyo kuwafanya wafanyabiashara wanaofuata sheria kushindwa kushindana ipasavyo huku wakijitahidi kutoa bidhaa salama na zenye ubora.

Wanywa pombe mnaitwa huku.

Shadeeya hapa wanywaji mnatuonea.😂😂😂😂

Kwanza Nimeshangaa kuona % ni kubwa sana.
kama ni kweli. Hapa uzembe ni wa TRA na wazalishaji wenyewe.

Sisi tunakunywa Pombe kwa kujua ziko kwa standards inayotakiwa na zimelipiwa Kodi na kufuata utaratibu uliowekwa na Serikali.
 
Pombe yeyote yenye alcohol ni hatari Kwa afya ya mtumiaji. Hilo ndilo lingefaa kusemwa na huyo mama na ingetakiwa hizo pombe za TBL ziwekewe onyo la tahadhari ya afya Kama sigara zinavyowekewa. Hayo maneno mengine ya kuzikandia pombe Nyingine haramu ni ujinga au upumbavu usio na msingi, sumu ni sumu tu hata ikiwa regulated.
 
Economic war
 
Pombe zote zimeandikwa.
Hairuhusiwi kuuzwa kwa mtu chini ya miaka 18. Na kunywa pombe kupita kiasi ni hatar kwa afya yako.

Hata wangeweka maneno ya Onyo makubwa kama Sigara. Bado watu wangetumia tu.

Focus iwe kwenye kuzipa standard sahihi Vileo vyote na kuondoa zile zenye hatarishi zaid.

Hizi zinazokwepa kodi mostly zitakuwa hazina kiwango kilichokubaliwa.
 
Shadeeya hapa wanywaji mnatuonea.😂😂😂😂
🤣🤣🤣
Kwanza Nimeshangaa kuona % ni kubwa sana.
kama ni kweli. Hapa uzembe ni wa TRA na wazalishaji wenyewe.
Ni kweli kabisa na TRA ana lawama zake hapa japo ndo mpunguze sa.😜 Teh
Sisi tunakunywa Pombe kwa kujua ziko kwa standards inayotakiwa na zimelipiwa Kodi na kufuata utaratibu uliowekwa na Serikali.
Hahahaaa. Poleni.

Sa best hapo sijui ndo mnafanyaje? Munaacha au mnafumba macho? 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom