Asilimia 90 ya ngano inatoka nje, kwahiyo tunakulaga chapati za Urusi, wananunua wanapaki wanatuuzia

Asilimia 90 ya ngano inatoka nje, kwahiyo tunakulaga chapati za Urusi, wananunua wanapaki wanatuuzia

Dunia imeingia kwenye janga la mafuta na ngano, lakini bado watu wanang'ang'ania kutoza kodi. Mfumko wa bei unazidi kuteketeza uchumi wa mtanzania lakini bado jitihada za kudhibiti hazijaonekana. Kuna haja kama taifa tuyaishi maono ya kijamaa. Tuanzishe mashamba ya umwagiliaji, tutumie vijana wasio na ajira kulima. Serikali isiingie sana kwenye ubepari,kwamba kila jambolifanywe na private sector. Ni bora tukafanye Mapinduzi ya kilimo na viwanda. Viwe chini ya usimamizi wa jeshi mpaka uchumi utakapo kaa sawa. Mvua hazinyeshi Nchi inaenda kuingia kwenye janga la njaa,je kama Nchi tunajipangaje. Hatua stahiki zinapaswa kuchukuliwa ili kuokoa Nchi na anguko la uchumi.
 
Najiuliza sana maswali yale mashamba ya KITULO na west kilimanjaro yalifia wapi mpaka kuagiza ngano Urusi?
Serikali yangu wakati mwingine mnatuchosha akili zetu wananchi
 
... hiyo ni ngao; imeripotiwa pia kwamba mahitaji ya mafuta ya kula kwa mwaka ni tani 700,000 ambapo uzalishaji wa ndani ni tani 30,000 wakati tani 670,000 zikiagizwa toka nje! Bado sukari kila mara ni uhaba! Aibu kwa CCM waliolifikisha taifa hapa! Wao muda wote wanawaza uchaguzi na wizi wa kura; mengine yote hadaa.
Si ukalime upunguze nakisi,unataka wakalime uvccm
 
Taifa la watu legelege wanaopenda mteremko kuanzia wanaume mpaka wanawake, kila utapeli ukizuka lazima waibiwe, kila kamari ikija maelfu wanaingia huko, kila umbeya ukizuka Taifa zima wanaujadili.......Leo chief unataka tuzalishe ngano? tuendelee kucheza baikoko tu na Singeli ndio fani yetu hiyo tukomae itatutoa..
Kila mtu anataka kukata mauno
Awe msanii

Ova
 
Enzi ya Mwalimu aliwaleta wazungu kutoka Canada wakatuanzishia mashamba ya NGANO kule Hanang tukawa tunajitosheleza kwa ngano na kupika mikate ya SIHA!!! Ilikuwaje mpaka yale mashamba ya BASUTO yakafa?
Inakuwaje nchi inapiga hatua kwenda mbele ,halafu anakuja mtawala mwingine nchi inarudi nyuma? Lazima kuna kitu tunafanya kama nchi ambacho hakiko sahihi; ni kitu gani hicho?
hayo mashamba ni mara wapewe wananchi hayana faida yamebaki sehem ya malisho ya mifugo
 
Nchi yetu ya kijamaa. Na sifa moja ya uchumi wa kijamaa ni upungufu wa bidhaa mbalimbali na uzalishaji mdogo.
 
Back
Top Bottom