African businesses
Member
- Feb 13, 2024
- 80
- 204
Habari zenu waungwana, binafsi leo nimeumia sana baada ya kugundua licha ya kuspend miaka mingi kuitafuta elimu kwenye hizi shule zetu za serikali, leo ndio nimegundua kumbe Mimi sikwenda shule bali niliudhuria kwenye hivi vituo vya kukuzia watoto vinavyomilikiwa na serikali
Kwa ufupi ni kwamba serikali haimiliki shule bali serikali inamiliki vituo ambavyo watoto wanapelekwa kukua ili badae waje kua tatizo kwenye jamii yetu.
Nadhani kila mtu anajua jinsi gani shule inavyotakiwa kuwa yahani shule ni muunganiko wa vitu viwili mazingira yaliyo bora kwa ajili ya kujifunza na content inayomjenga na kumuanda mwanafunzi kukabiliana na changamoto atazokutana nazo katika maisha.
Sasa kama hivi vituo vinavyomilikiwa na serikali tukiviita ni shule basi wote tutakua hatujui mahana ya shule, kwani hivi vituo vinavyomilikiwa na serikali vinakosa sifa zote za kuitwa shule.
Kwa kumalizia labda tu niseme serikali haijawai kumiliki shule bali inamiliki vituo vya kukuzia watoto ili badae waje kua wanajeshi polisi wasiojua wajibu wao, panya road, wadada wanaojiuza, wafanyabiashara wadogowadogo ambao wamejazana mabarabarani, wezi vibaka majambazi, wachungaji na mashee uchwara na sasa hivi kuna machawa.
Kama ulisoma shule zinazomilikiwa na serikali au zile za tasisi binafsi zinazofanana na shule za serikali na unajidai ulienda shule jaribu kufikiria upya.