Mimi juzi tu nimemkataza mpwa wangu kuja kukaa kwangu.
Ni hivi, huyu mpwa wangu nilimleta mjini, nikasimamia show akapata msingi wa kukaa mjini. Mimi baadae nikachomoka nimefikia ughaibuni ila mke wangu mmoja yupo mkoani. Sasa mpwa anataka kuhama Dar kurudi mkoani baada ya miaka kama 7 hivi toka nimuache Dar, anaomba nimpe hifadhi kwangu.
Yaani afikie kwa mke wangu anapojipanga, hii siyo mara ya kwanza yeye kujaribu kurudi mkoani, 2019 aliniomba hifadhi hivi hivi nikamruhusu, cha kushangaza alifika kwangu na watoto wawili, kwanza hakuniambia amepata mtoto wingine mdogo. Wa kwanza nilijua anaye ila pia hakuniambia anakuja naye kwangu.
Sasa baada ya muda akaamua kuondoka kurudi Dar, leo anaomba kurudi kwangu. Inamaana nitakuwa na wajibu wa kumlisha na watoto wake wawili, najua tu atakapofika tu wataanza mambo yao ya wanawake watagombana na mke wangu bure, mke wangu na mtoto wangu nawahudumia kwa bajeti nayoiweza mimi, nikimruhusu aje na watoto wake wawili ntakuwa na bajeti ya watu watano na karaha juu.
Nimeamua kuwa mbaya. Sitaki ujinga wa ndugu. Isitoshe nyumbani kwao siyo mbali na ninapoishi sema kwa kuwa amechezea maisha kama mwanamke anaona aibu kwenda kukaa nyumbani kwao.
Nimemuambia kwangu hakuna nafasi ajipange atafute namna ya kuanza maisha. Nimefanya hivyo kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima katika familia yangu na pia kumpa changamoto ajisimamie, siyo kila siku aje kuomba msaada atazoea.