Asilimia kubwa ya Watanzania wanatumia nguvu za giza katika Biashara, Ajira na Harakati za Maisha Kiujumla

Asilimia kubwa ya Watanzania wanatumia nguvu za giza katika Biashara, Ajira na Harakati za Maisha Kiujumla

Uchawi ni imani potofu! Ukiuamini, umepotea. Mimi ninaingia mwaka wa tatu huu! Hakuna cha uchawi, wala nini! Halafu biashara imenyooka kama rula.

Kutokubweteka, nidhamu ya pesa pamoja na ulinzi wake madhubuti, nidhamu kwa wateja, ubunifu, kujiongeza, kukwepa kodi za kijinga za TRA, kununua bidhaa za magendo kwa bei ya chini na kwenda kuuza kwa bei ya sokoni, kutumia fursa mbalimbali, nk ndiyo uchawi wenyewe huo sasa!!!
Mkuu mwambie huyo mshirikina, na mtoa kafara!
 
We subiri tu shetani anakulia mingo pigo 1 tu chali
As i told you! Ukiwa na wazo zuri la biashara, una mtaji wa uhakika, ukaenda kuanzisha hiyo biashara katika eneo sahihi! Una soko la uhakika, una nidhamu kwa wateja wako, bei ya bidhaa zako ni rafiki kuliko washindani wako!

Aisew huo uchawi na chuma ulete sijui, utausikia tu kwa jirani. Binafsi biashara yangu nimemkabidhi Mwenyezi Mungu, badala ya hao waganga wenu wa kienyeji.
 
Kwenye siasa, uchawi 100%

Biashara uchawi upo kwa 75% waliobaki hawajielewi wamuamini Mungu au waingie kwa sangoma😂😂😅😅

Kwenye Ajira uchawi unatumika kupandisha vyeo, kulinda vyeo na kurudisha kazini wadau waliotimuliwa.

Mahakamani huko 90% na zaidi kuna mauza uza kibao ya ushirikina. na umeua wengi sana kwenye kesi kama za Mirathi

Kwenye mapenzi huko 90% ya kina mama wanatulisha vitu vizito sana ili tuwapende na kuwasikiliza..

90% ya kesi za mirathi humalizwa na ushirikina. Jikute wewe ndio unapinga wadau wasiuze mali utajikuta jalalani unaokota kopo

Narudi
Ndio unajua Leo? Tanzania ipo top 10 ya Nchi zinazoamini ushirikina Duniani.
 
As i told you! Ukiwa na wazo zuri la biashara, una mtaji wa uhakika, ukaenda kuanzisha hiyo biashara katika eneo sahihi! Una soko la uhakika, una nidhamu kwa wateja wako, bei ya bidhaa zako ni rafiki kuliko washindani wako!

Aisew huo uchawi na chuma ulete sijui, utausikia tu kwa jirani. Binafsi biashara yangu nimemkabidhi Mwenyezi Mungu, badala ya hao waganga wenu wa kienyeji.
Umemkabidhi Mungu ili nini wakati unafuata formula za biashara? Mungu aongeze nini? Kwanini hauwi neutral?
 
MBAYA ZAIDI UTAKUTA ANATUMIA NGUVU ZA KIZA,KWA SIRI,HUKU AKIWA NI MTU WA KANISA KWELI NA KUWAASA WENGINE WAACHANE NA NGUVU ZA GIZA TUMTEGEMEE YESU,IN FACT JEHANAM ITAJAA KWELIKWELI.
Nuru na Giza hazikai pamoja, ni vigumu kuwa kote kote.
 
Ila wana wa Ishmael kwa kupenda uganga hawajambo.
Mmoja juzi kaenda Tanga kuroga aliposikia kuwa boss hatamwongezea tena mkataba baada ya kuisha alionao
😂😂😂😂Kuroga Tanga ni kama bima ya afya
 
Uchawi ni imani potofu! Ukiuamini, umepotea. Mimi ninaingia mwaka wa tatu huu! Hakuna cha uchawi, wala nini! Halafu biashara imenyooka kama rula.

Kutokubweteka, nidhamu ya pesa pamoja na ulinzi wake madhubuti, nidhamu kwa wateja, ubunifu, kujiongeza, kukwepa kodi za kijinga za TRA, kununua bidhaa za magendo kwa bei ya chini na kwenda kuuza kwa bei ya sokoni, kutumia fursa mbalimbali, nk ndiyo uchawi wenyewe huo sasa!!!
Waulize wachina bulldozer ilipotea huko Handeni, we piga kelele huku mitandaoni ila wabwanga huko Lushoto pia ni wachawi sana
 
Ukizaliwa Tanzania tayari una vinasaba vya uchawi kabisa haina haha ya kupiga kelele pale Kariakoo wafanyabiashara wakubwa 100% ni wanga na hawana furaha, mtu anashinda pale mpaka saa 6 ndo anarudi kwake usiku na 11 alfajiri yuko pale.
 
Inawezekana kuna ukweli mkuu, maana nchi za kiafrika haziendelei ni pamoja na kuendekeza mambo ya kishirikina, uchawi, ulozi na matakataka mengine kwenye kila nyanja.......wakati mzungu anarusha satellite angani, wataalamu wetu wa asili wanashindana kurusha nyungo usiku....
 
Wakati wa kudai Uhuru viongozi walikuwa wanaenda kuloga Bagamoyo ili mkoloni awape uhuru, hii tabia iko kwenye damu ya watz wengi.
 
Wakati wa kudai Uhuru viongozi walikuwa wanaenda kuloga bagamoyo ili mkoloni awape uhuru,hii tabia iko kwenye damu ya watz wengi
Walifanya na matambiko, tunaweza tukawa tunaumiza vichwa kutaka kujua kwa nini bongolala haiendelei pamoja na kuwa na rasilimali lukuki, kumbe ilishafungwa kwenye maagano ya kimizimu na kiganga, namuomba Mungu aingilie kati aisee....
 
Uchawi ni imani potofu! Ukiuamini, umepotea. Mimi ninaingia mwaka wa tatu huu! Hakuna cha uchawi, wala nini! Halafu biashara imenyooka kama rula.

Kutokubweteka, nidhamu ya pesa pamoja na ulinzi wake madhubuti, nidhamu kwa wateja, ubunifu, kujiongeza, kukwepa kodi za kijinga za TRA, kununua bidhaa za magendo kwa bei ya chini na kwenda kuuza kwa bei ya sokoni, kutumia fursa mbalimbali, nk ndiyo uchawi wenyewe huo sasa!!!

Imenyooka kama rula,noted [emoji3]
 
Back
Top Bottom