Asilimia mia moja tunapita, ila kuna sharti dogo sana

Bora lile neno angetamka kwa mkewe ila sio mbele ya hadhara, ametutia nuksi.
 
Mashabiki wa taifa stars hamnazo. Kuna timu pale ya kwenda round ya pili? Kocha kasema pale kuna majina tuu hakuna wachezaji.
Sasa yeye mwenyewe anachagua wachezaji ligi daraja la saba huko ulaya unaacha watu wanaocheza champions league africa
 
HAMUWEZI PITA MIMI NIMEKAA HAPA. MPIRA SIYO UHAMASISHAJI.
 
Mimi bado nabaki optimistic kwamba tutavuka hatua hii.

iko hivi mashindano yana timu 24.
Katika hatua hii zinachujwa timu 8 tu.
Timu 16 zitabaki kwa hatua inayofuata..

Kwa msingi huu, hata watakaoshika nafasi ya tatu kwny group level (watakuwa 6) wa4 kati ya 6 watafuzu straight kupitia dirisha la best loser.

Hivyo stars wetu hata wakishinda mechi moja tu watafuzu kama ilivyokuwa kwa Malawi afcon iliyopita.

Tujiepusheni na malawama ya kifala
 
Timu lako la Kifala ....

Huwezi epuka lawama.
 
Tunahitaji kocha wazalendo yaani watanzania,ikiwezekana Serikali igharamie kusomesha makocha 100 kwa mwaka mmoja ulaya,kipaumbele kocha awe mtu aliyewahi kucheza mpira ...tutapiga hatua kuliko hawa makocha wa kigeni.Tujifunze kwa waliofanikiwa wengi walitumia kocha wazalendo
 
Rome was not built in a day. Kwa nini tusianze kuwaandaa vijana. Naona walioitwa wanaleta matumaini.

Samatta, Msuva, Manula , Tshabalala ni mzigo tu. Waacheni wastaafu.
 

Tungekuwa tunacheza kama Msumbiji ningekubali, ila kwa mpira wa Jana hamna kitu. Tena kwa Zambia na DRC tutapigwa nyingi, maana morrocco alituchukulia poa Jana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…