MwanaPekee
JF-Expert Member
- Jul 18, 2014
- 382
- 386
Jana tarehe 12/11/2019 katika uzinduzi wa kitabu kilichoandikwa na Rais Mstaafu Benjamin W. Mkapa, Rais Magufuli alisema kati ya mambo ambayo atamkumbuka Mzee Mkapa ni lile alilokubali wazo lake la kuanziswa kwa Mfuko wa Barabara (Road Fund) licha ya sehemu kubwa ya Baraza la Mawaziri kukataa kwa madai kuwa hauna tija. Ikumbukwe kuwa kwa kipindi hicho TANROADS haikuwepo, na ilianzishwa baadaye, ili kuongeza ufanisi wa pendekezo hilo hilo la JPM ambapo sote ni mashahidi wa kazi kubwa inayofanywa na TANROADS. Leo kila Mtanzania anaufikia mkoa wake kwa Barabara ya Lami tofauti na ilivyokuwa miongo michache iliyopita.
Suala la kujiuliza hapa, kama Mawaziri wengi wa kipindi hicho hawakuona umuhimu wa pendekezo hilo, leo barabara zetu zingekuwaje? Pia ikumbukwe kuwa barabara nyingi sana, pamoja na madaraja vimejengwa katika kipindi ambacho JPM alikuwa Waziri wa Ujenzi, na ndicho kipindi ambacho juhudi zake za kuhakikisha kuwa mikoa mingi inaunganishwa kwa barabara ya lami zilipigwa vita na baadhi ya watendaji wa serikali kiasi cha kutaka kuondoa uhai wake.
Hili ni dalili tosha kuwa uzalendo wa JPM haujaanza leo, unathibitika katika kazi nyingi alizozifanya katika mazingira ya hatari kwa muda mrefu. Kupigwa kwake vita na mafisadi hakujaanza leo, kumeanza tangu akiwa Waziri. Hivyo yote yaliyotokea yamemkomaza na kumfanya awe ni mtu asiyeyumbishwa na wapinga maendeleo.
Tumuombee sana Rais wetu kipenzi, Our God-given President.