Pre GE2025 Asiyekubalika kwao anawezaje kushawishi Wananchi Wamchague Samia?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
View attachment 2860069

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kasimu Majaliwa ametangaza hadharani huko kwao Ruangwa kwamba kwenye Jimbo hilo Rais Samia atashinda Uchaguzi kwa 100% , hapa anazungumzia uchaguzi wa 2025 , hata hivyo hakuna kikao chochote ambacho ccm ilikaa kuteua Mgombea Urais wala hakuna mahali popote ambapo Tume ya Uchaguzi imetangaza kupitisha majina ya Wagombea Urais .

Bali kinachofahamika ni kwamba Kasimu Majaliwa hakubaliki kwao na wala hana ushawishi wowote wa kuwezesha Samia kuchaguliwa kwa asilimia hizo na Wana Ruangwa.

Labda kwa Wasahaulifu na kwa wageni wa jf ni kwamba , Kwenye ulioitwa uchaguzi mkuu wa 2020 , Kasimu Majaliwa ni miongoni mwa Wabunge wa ccm waliopita bila kupingwa , baada ya kugundua kwamba hakubaliki kwao aliamua kuhujumu kila mgombea kutoka vyama vingine , wengine waliporwa fomu huku wengine wakiokotwa kwenye mapori ya Mkuranga Mkoa wa Pwani wakiwa na majeraha makubwa , Hivi mtu ambaye hawezi kuwa mbunge bila Wagombea wengine kutekwa anawezaje kushawishi wananchi wamchague Samia , Kwanini anamdanganya Rais , Amelenga jambo gani ?
Hongera Erythrocyte kwa ushindi wa Uchawa Bora 2023 humu JF!
 
Muwe watu timamu basi kwani ushindi huletwa na ushawishi??
 
Chawa anawezaje kumpa za uso Waziri Mkuu ?
Usingekuwa chawa usingeandika eti Mh. Majaliwa hakubariki wakati Chadema na vyama vyote vya upinzani viliogopa kupambana nae. Poa huwezi kukubali kuwa Mh. Mbowe (anayekubalika sana kwao! Ahahahahaha!!) alishindwa VIBAYA SANA na Kijana mdogo Mwl. Saasisha Mafuwe! Ahahahahaha! Kwa chawa HAWEZI kukubali! Ahahahahaha!!!
 
Jomba unafuatilia mambo ya CCM kuliko ya saccoss yenu ya CHADEMA... vipi mchango wa kusaidia HANANG mmefikisha Tsh ngapi?
 
Usingekuwa chawa usingeandika eti Mh. Majaliwa hakubariki wakati Chadema na vyama vyote vya upinzani viliogopa kupambana nae. Poa huwezi kukubali kuwa Mh. Mbowe (anayekubalika sana kwao! Ahahahahaha!!) alishindwa VIBAYA SANA na Kijana mdogo Mwl. Saasisha Mafuwe! Ahahahahaha! Kwa chawa HAWEZI kukubali! Ahahahahaha!!!
JF kuna haja sana ya kuangalia afya ya akili kwa wanaojiunga humu .
 
Walioanza kampeni mapema watakatwa bila kujali nafasi zao za awali.

Tusilaumiane.
 
View attachment 2860069

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kasimu Majaliwa ametangaza hadharani huko kwao Ruangwa kwamba kwenye Jimbo hilo Rais Samia atashinda Uchaguzi kwa 100% , hapa anazungumzia uchaguzi wa 2025 , hata hivyo hakuna kikao chochote ambacho ccm ilikaa kuteua Mgombea Urais wala hakuna mahali popote ambapo Tume ya Uchaguzi imetangaza kupitisha majina ya Wagombea Urais .

Bali kinachofahamika ni kwamba Kasimu Majaliwa hakubaliki kwao na wala hana ushawishi wowote wa kuwezesha Samia kuchaguliwa kwa asilimia hizo na Wana Ruangwa.

Labda kwa Wasahaulifu na kwa wageni wa jf ni kwamba , Kwenye ulioitwa uchaguzi mkuu wa 2020 , Kasimu Majaliwa ni miongoni mwa Wabunge wa ccm waliopita bila kupingwa , baada ya kugundua kwamba hakubaliki kwao aliamua kuhujumu kila mgombea kutoka vyama vingine , wengine waliporwa fomu huku wengine wakiokotwa kwenye mapori ya Mkuranga Mkoa wa Pwani wakiwa na majeraha makubwa , Hivi mtu ambaye hawezi kuwa mbunge bila Wagombea wengine kutekwa anawezaje kushawishi wananchi wamchague Samia , Kwanini anamdanganya Rais , Amelenga jambo gani ?

Kama Waziri mkuu ni chawa , nani atapona?
 
Back
Top Bottom