Mihangwa asilomia 85 namuelewa hizo 65 umepunguza
WanaMajlis,
Inaelekea mmeupenda huu mjadala maana nilitoa wazo tuumalize lakini
michango imeendelea.
Tuifanye hii barza yetu pawe mahali pa kuelimishana.
Nataka nieleze kitu muhimu katika kitabu kuwa kitabu cha rejea kwa
maana wasomaji kukisoma kwa kupata uelewa zaidi wa somo.
Ili kitabu kiingie katika dunia ya rejea katika Library ya Congress na
katika maktaba nyingine duniani muhimu kabisa ni kuwa kitabu kiwe
kwenye lugha ya Kiingereza au lugha kuu nyingine za dunia kama
Kifaransa na Kiarabu.
Ukiwa na kitabu nje ya lugha ya Kiingereza na ukategemea kuwa hicho
kitabu kitasomwa na kuwa rejea, hili haliwezekani na kitabu kitabaki
katika shubaka popote pale kilipo.
Hii ni sawa na kufanya kazi ya bure.
Baba wa Taifa alipatapo kusema kuwa Kiingereza ni Kiswahili cha dunia.
Nikita Khrushchev aliandika kitabu, ''Khrushchev Remembers,'' (1971)
kitabu hiki kilikuwa katika lugha ya Kirusi lakini kilikuwa kitabu hasa
ambacho kilieleza mengi katika historia ya Urusi kabla na baada ya Vita
Kuu zote mbili za dunia.
Katika hali iliyokuwapo Urusi wakati wa Vita Baridi kitabu hiki hakikuweza
kuchapwa Urusi, ilibidi kitolewe nje kwa siri kubwa ili kipate kuchapwa.
Kitabu hiki kilitafsiriwa katika Kiingereza na kilikuwa, ''Best Seller,'' mwaka
wa 1971.
Laiti kitabu hiki kingebaki katika lugha yake ya Kirusi kingebaki ndani ya
shimo la kiza kikuu na hakuna yeyote angekijua na kwa hivyo kukisoma
kiasi hata hapo Library of Congress kingekuwa kinapigwa na vumbi.
Ninayo nakala ya kitabu hiki na kwa kukipenda nimekifanyia ''binding,''
maana nakala yangu ilikuwa ni ''paper back,'' hivyo jalada halikukawia
kuchanika.