Askari 7 wanaodaiwa kumuua Mfanyabiashara wa Madini kupandishwa Kizimbani Januari 11

Askari 7 wanaodaiwa kumuua Mfanyabiashara wa Madini kupandishwa Kizimbani Januari 11

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kesi ya mauaji inayowakabili maofisa saba wa polisi mkoani Mtwara imepangiwa tarehe nyingine ya kusikilizwa kutokana na upelelezi kutokamilika.

Watuhumiwa hao jana walifikishwa kwa mara nyingine mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara na kupangiwa kusikilizwa tena Januari 11, mwaka huu.

Walifikishwa mahakamani mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Mussa Esanju.

Mara ya kwanza maofisa hao walifikishwa mahakamani Januari 25, mwaka 2022 kwa tuhuma za kufanya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda, wilayani Nachingwea mkoani Lindi.

Kesi hiyo ni namba 01 ya Mauaji mwaka 2020/2022 iliyoendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Florence Mbamba.

Washitakiwa ni Mrakibu wa Polisi, Gilbert Kalanje ambaye ni Mkuu wa Upelelezi, Wilaya ya Mtwara; Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Charles Onyango ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara na Mrakibu wa Polisi Msaidizi, Nicholaus Kisinza ambaye ni Mkuu wa Kikosi cha Intelijensia ya Jinai Mkoa wa Mtwara.

Wengine ni Mkaguzi wa Polisi, John Msuya; Mganga Mkuu wa Zahanati ya Polisi mkoani Mtwara, Mkaguzi wa Polisi, Msaidizi Marco Mbuta; Mkaguzi wa Polisi, Shirazi Mkupa pamoja na Koplo Salimu Mbalu.

HABARI LEO
 
Kwani bado wanatumikia nafasi zao za kazi? Maana wote wamendikwa vyeo vyao kama bado wanavitumikia.

Hii ni kesi ya nyani kupelekwa kwa ngedere. Ni swala la wakati tu ushahidi 'utakosekana' wa wakuwatia hatiani na maisha yao kuendelea.
 
Hao wanakula mvua za kutosha na baadhi watanyongwa
 
Ajali kazini,Gilbert Kalanje ni Depo yangu,tukafanya kazi wote Oysterbay na kisha Kawe Polisi,akapanda Vyeo mpaka kuwa SP,sasa hivi amemaliza mwaka Mahabusu[emoji24][emoji24]ukisikia maisha ni kupanda na kushuka ndio huku sasa
Sawa Afande jitahidini muache kuonea raia malipo Ni hapa hapa, haijakupata ukiwa kazini itakupata ukishastaafu.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Vipi huwa maaskari waliohusika kwa mkasa huu, wa kijinga kabisa tena jeshi la polic lakulinda raia na mali zake, ikibainika ni kweli, walakini wanyogwe mpaka kufa, ili iwe, fundisho. Tungekuwa nchi nyingine , ingekuwa maandamano, na kuchoma moto vituo vya polic, hii ni aibu sana.
 
Hapo Itakuwa Kama Zombe Wa Mkambalani Morogoro
Yaani Hao Mafanikio Yao Yanatokana Na Kumwaga Damu Za Watu Wasio Na Hatia
 
Waliohusika, ktk tukio hili, walakini wanyogwe hadi kufa, haya ni majambazi wakubwa. kuishi kwao hawa, hatupati faida au hasara, je! kwanini isiwe hivyo?
 
Back
Top Bottom