Askari aliyezuia wizi bandarini Dar atekwa

Askari aliyezuia wizi bandarini Dar atekwa

''Nimepewa orodha ya watu wanaoiibia TRA na kule bandarini.......nawajua kwa amajina'' Jakaya Mrisho Kikwete , 2010
 
Kwenye hili, intelijensia ya IGP Mwema haipo.
 
wamuwahi mabwepandeni na mwenye namba ya Juma Mgaza ampigie awahi kumuokota, na hivi Mwanahalisi limefungiwa, thijui!!!
 
Haishangazi kwa kuwa aliyetekwa ni mtetezi wa rasilimali ya Taifa na angekuwa fisadi au mwezi wa rasilimali za Taifa ningeishangaa nchi yangu.

mtu anakutumia sms kwa cm ambayo ni registerd in tz aafu unashindwa kumlocate? Mbona hosea alisema jana mtu atakayemtumia vitisho wana uwezo wa kulocate hata pc iliyotumika kuandika jf?
 
The following takes place between 7:00 pm and 8:00pm @ TPA,,,,,,,,,
 
Fidelis Butahe na Jannifer Summi | 11 September 2012

MMOJA wa askari wa bandari, Cornell Kufahaizuru aliyeshiriki operesheni ya kuzuia jaribio la wizi wa shaba na mafuta Bandari ya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, juzi ametekwa na watu wanaodaiwa ni wahusika wa jaribio hilo.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe zilieleza kuwa juhudi za kumtafuta zinafanywa na vyombo vya dola nchini.

Licha ya Dk Mwakyembe,chanzo kingine cha habari cha kuaminika kutoka Kitengo cha Ulinzi na Usalama katika bandari hiyo, kimethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Waziri Mwakyembe alisema Kufahaizuru alitoweka siku moja baada ya kupambana na katika zoezi la wizi huo, hajulikani alipo.

"Juhudi za kumtafuta huyo kijana na waliomteka zinaendelea, lakini mpaka sasa hajapatikana ingawa kuna taarifa zisizo rasmi zinazoeleza kuwa kuna maeneo huwa anaonekana," alisema Dk Mwakyembe na kuongeza:

"Uhalifu wa aina hii ni mpya kabisa, huu ni ukurasa mpya wa uhalifu nchini lazima tupambane nao, unaweza kuufananisha na zile filamu za nchini Nigeria."

Awali, askari mmoja katika kitengo cha ulinzi bandarini hapo kwa sharti la kutotajwa, alidaiKufahaizuru alitekwa na watu wasiojulikana juzi.
Tangia ilipotangazwa publicly kuwa wezi wa pesa za EPA wamepewa (sikumbuki muda gani) kurudisha pesa walizoiba nje ya mfumo wa sheria za nchi Watanzania wengi walipoteza imani na serikali. Na kilichofuatia hapo ni wakuu wengine kulielewa hilo na kwa mfano polisi kazi yao kubwa imekuwa kupambana na wananchi waliopoteza imani na serikali yao huku wakijua fika kuwa wanakiuka viapo vyao, kwa maana hiyo sio ajabu kila ukweli unaundiwa tume ili ufichike.
Mlolongo wa haya yote ni kuzaliwa kwa jeshi lenye malengo tofauti na lile la awali ambalo outwardly kazi yake ni kulinda raia lakini inwardly (ukweli) ni wachumia matumbo yao mpaka kufikia hatua ya kupanga utekaji na ujambazi mkubwa mkubwa juu ya wale wanaotetea haki.
Kama kweli askari anayetekeleza kiapo chake kwa kuzuia wizi anaweza kufanyiwa hivyo, unaweza kujaza ni jinsi gani na sisi wananchi tusio na nafasi yoyote tutatendewa vipi na POLISI hao!!??? ...Marehemu Mwangosi anaweza kutupa jibu labda

 
''...........tukiwafukuza mafisadi nchi itayumba................'' by mizengo pinda.
 
Hivi nchi hii ina laana gani? Kweli askari anaweza kutekwa na wahalifu then wanatoa masharti ya wezi wenzao kuachiwa hii kweli TZ!!!. Mwalimu JK alisema haiwezekani kiongozi awe mfanyabiashara watu tukaona hana maana sasa viongozi hawa wameamua si kuwa wafanyabiashara tu bali majambazi kabisa. Kova na ndugu zake wanawajua wezi wote wakubwa hapa nchini tatizo kwa kuwa wanagawana hizo mali wanaishia kukimbizana na wezi wa kuku tandale hao ndugu zao hawakamatwi, matokeo yake ndio haya
 
Kwani matapeli wa shaba nchi hii hawajulikani. Serikali acheni kutu chezea wahusika mnawajua hata viongozi waandamizi wa jeshi la police dili hili wanalijua. Hata baadhi ya cooper sheet zilizoibiwa kipindi cha nyuma zinajulikana zilipo.


Muzamir Katunzi
 
Mimi naamini hamna ujambazi wowote mkubwa unaofanyika hapa Tanzania bila kuhusisha Polisi.. I am telling you siku polisi wakiamua kusema no..ujambazi utaisha siku hiyi hiyo. Otherwise itakuwa ni movies tu zinazotofautiana na seasons na stellings.. Makamando wangine ni wasanii tu..huku wanakula cha juu!!!
 
Zomba umesikia mambo ya serikali ya jk, wapi ile maneno serikali inamkono mrefu??, watu wamekwiba mabilioni ya epa, meremeta, kiwira, uswis, rada, kesi za utata kama za babu seya,zombe, mauaji ya polisi kwa raia wake nyamongo, singida, morogoro, arusha, iringa, mwanza nk....maisha duni kwa kila mtanzania, ukosefu wa mikopo vyuo vikuuu takribani graduates 500,000 (2010-2011) hawana ajira... Wizi wa rasilimali kila sehemu... Na watu hao bado wapo serikalini na wengine ni mawaziri.... Hizi ni salamu zangu kwako zomba na mnaoishabikia nyinyiemu

Badala ya kusifia wizi umegunduliwa nyie mnapindisha maneno. Miaka iliyopita tulisikia watu wakilizwa shaba zao uliona mtu kushikwa? Funguka. Huo wizi mpaka Zambia wakasusa kupitisha shaba zao hapa hakuna aliyekamatwa, sasa tunaona Kikwete akiwashika, si hao tu, juzi juzi tuliona shaba imekamatwa Morogoro. Na bado mtazidi kumchukia kwa kufichuwa madudu yenu.
 
Hivi sifa kuu ya kumjua Mtanzania sehemu yoyote ukimwita MWIZI anaitika kwa tabasamu mzito, ukimwambia we mwizi wa kichaga njoo hapa, ataitika naam mzee, au we mwizi wa kipare mambo vipi, utasangaa, utawaona majizi kama M.S.O.F.E na M.A.S.S.A.W.E wanasifiwa sana majukwaani , hivi ni lazima sifa hizi ndio maendeleo ama vipi?
 
Badala ya kusifia wizi umegunduliwa nyie mnapindisha maneno. Miaka iliyopita tulisikia watu wakilizwa shaba zao uliona mtu kushikwa? Funguka. Huo wizi mpaka Zambia wakasusa kupitisha shaba zao hapa hakuna aliyekamatwa, sasa tunaona Kikwete akiwashika, si hao tu, juzi juzi tuliona shaba imekamatwa Morogoro. Na bado mtazidi kumchukia kwa kufichuwa madudu yenu.
Mkuu alafu kuku wangu mwaka huu wametaga sana na mashamba yangu mazao yamekubali kuliko muda mrefu sana sijui na hii ni sababu ya JK ?

Wabongo tuache kupeana credit na kuchukua credit na kujipongeza ambako hakuna maana.., JK ni kazi yake kuona nchi inakwenda sawa ila ni ukweli usiopingika kipindi hiki kutokana na udhaifu fulani mambo yamekuwa yakienda ndivyo sivyo.., na watendaji kazi wake wamekuwa wakifanya wanavyotaka (kwahio hapa kosa ni la either hawaogopi na wanafanya watakavyo au uchaguzi / uteuzi wake haufai)
 
Back
Top Bottom