Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,265
- 17,120
''Nimepewa orodha ya watu wanaoiibia TRA na kule bandarini.......nawajua kwa amajina'' Jakaya Mrisho Kikwete , 2010
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haishangazi kwa kuwa aliyetekwa ni mtetezi wa rasilimali ya Taifa na angekuwa fisadi au mwezi wa rasilimali za Taifa ningeishangaa nchi yangu.
Tangia ilipotangazwa publicly kuwa wezi wa pesa za EPA wamepewa (sikumbuki muda gani) kurudisha pesa walizoiba nje ya mfumo wa sheria za nchi Watanzania wengi walipoteza imani na serikali. Na kilichofuatia hapo ni wakuu wengine kulielewa hilo na kwa mfano polisi kazi yao kubwa imekuwa kupambana na wananchi waliopoteza imani na serikali yao huku wakijua fika kuwa wanakiuka viapo vyao, kwa maana hiyo sio ajabu kila ukweli unaundiwa tume ili ufichike.Fidelis Butahe na Jannifer Summi | 11 September 2012
MMOJA wa askari wa bandari, Cornell Kufahaizuru aliyeshiriki operesheni ya kuzuia jaribio la wizi wa shaba na mafuta Bandari ya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, juzi ametekwa na watu wanaodaiwa ni wahusika wa jaribio hilo.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe zilieleza kuwa juhudi za kumtafuta zinafanywa na vyombo vya dola nchini.
Licha ya Dk Mwakyembe,chanzo kingine cha habari cha kuaminika kutoka Kitengo cha Ulinzi na Usalama katika bandari hiyo, kimethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Waziri Mwakyembe alisema Kufahaizuru alitoweka siku moja baada ya kupambana na katika zoezi la wizi huo, hajulikani alipo.
"Juhudi za kumtafuta huyo kijana na waliomteka zinaendelea, lakini mpaka sasa hajapatikana ingawa kuna taarifa zisizo rasmi zinazoeleza kuwa kuna maeneo huwa anaonekana," alisema Dk Mwakyembe na kuongeza:
"Uhalifu wa aina hii ni mpya kabisa, huu ni ukurasa mpya wa uhalifu nchini lazima tupambane nao, unaweza kuufananisha na zile filamu za nchini Nigeria."
Awali, askari mmoja katika kitengo cha ulinzi bandarini hapo kwa sharti la kutotajwa, alidaiKufahaizuru alitekwa na watu wasiojulikana juzi.
Nini kilifuata baada ya hapo??''Nimepewa orodha ya watu wanaoiibia TRA na kule bandarini.......nawajua kwa amajina'' Jakaya Mrisho Kikwete , 2010
Kwani matapeli wa shaba nchi hii hawajulikani. Serikali acheni kutu chezea wahusika mnawajua hata viongozi waandamizi wa jeshi la police dili hili wanalijua. Hata baadhi ya cooper sheet zilizoibiwa kipindi cha nyuma zinajulikana zilipo.
Mabwepande inanukia....
Nini kilifuata baada ya hapo??
kazimzumbwi hiyo mdau,huko KISARAWE
Zomba umesikia mambo ya serikali ya jk, wapi ile maneno serikali inamkono mrefu??, watu wamekwiba mabilioni ya epa, meremeta, kiwira, uswis, rada, kesi za utata kama za babu seya,zombe, mauaji ya polisi kwa raia wake nyamongo, singida, morogoro, arusha, iringa, mwanza nk....maisha duni kwa kila mtanzania, ukosefu wa mikopo vyuo vikuuu takribani graduates 500,000 (2010-2011) hawana ajira... Wizi wa rasilimali kila sehemu... Na watu hao bado wapo serikalini na wengine ni mawaziri.... Hizi ni salamu zangu kwako zomba na mnaoishabikia nyinyiemu
Mkuu alafu kuku wangu mwaka huu wametaga sana na mashamba yangu mazao yamekubali kuliko muda mrefu sana sijui na hii ni sababu ya JK ?Badala ya kusifia wizi umegunduliwa nyie mnapindisha maneno. Miaka iliyopita tulisikia watu wakilizwa shaba zao uliona mtu kushikwa? Funguka. Huo wizi mpaka Zambia wakasusa kupitisha shaba zao hapa hakuna aliyekamatwa, sasa tunaona Kikwete akiwashika, si hao tu, juzi juzi tuliona shaba imekamatwa Morogoro. Na bado mtazidi kumchukia kwa kufichuwa madudu yenu.