Askari amshushisa dereva matusi na kipigo, Ni vipi tunaweza kujitetea na uonevu bila hofu ya kuuliwa, kubambikiwa kesi za madawa, ugaidi, n.k

Askari amshushisa dereva matusi na kipigo, Ni vipi tunaweza kujitetea na uonevu bila hofu ya kuuliwa, kubambikiwa kesi za madawa, ugaidi, n.k

Hivi wahuni wa daladala, ma madereva wa malori ukiwalegezea wataua watamaliza watu barabarani, mhuni anahitaji mtu wa ku deal naye kihuni ndio atasikia
 
Wanaumoja Hawa ndugu na ni rahisi hata kukuua kupoteza ushaidi, omba hekima siku ukikutana na kadhia kama hiyo
Tuombe Mungu anipe hekima kama unavyosema.
Nishawahi anzisha varangati kituo cha polisi kabisa. Kisa WP mmoja alitaka kujifanya mjuaji. Hekima za mkuu wa kituo ndio ziliamua ugomvi ule.
 
askari huwa hawapigani kushindwa hilo ondoa kichwani,yaani ni lazima upoteze pambano hata kama ni kesho jioni.

yaani utambe kwamba umekaza kituo kizima wameufyata.weeee

Mbona nilishamdunda mmoja hadi akaomba watu wamsaidie kunidondosha chini Ili anipige nikiwa chini!!!

Yule bwege nilimtandika fara yule!!!

Nilimpiga mkasi wa mkono wa kulia kwenye koromeo (upanga ulio katikati ya dole gumba na kidole cha kwanza baada dole gumba), hapo hapo nikaunga na lower side kick ya mguu wangu wa kushoto (natumia orthodox stance) ya kwenye kitovu. Nikasimama!!!!

Akaja na ngumi nika-dance left side nikai-divert ngumi yake kwa mkono wangu wa kushoto af nikaukunja mkono aliokuwa amerusha ngumi kuupeleka mgongoni mwake kwa mkono wangu huo huo wa kushoto, af mkono wangu wa kulia nikamchomekea kidole gumba mdomoni upande wa pili wa mwili wake (far side) kwenye uwazi uliopo Kati ya meno na ngozi ya taya , na mguu wangu wa kushoto nimeubana nyuma ya mguu wake mmoja Ili nimbane vizuri..NILIPIGA VICHWA VYA PUA YULE ASKARI ALIKUWA ANALIA KAMA NG'OMBE.
 
Back
Top Bottom