Askari amuua askari mwenzie Mtwara

Askari amuua askari mwenzie Mtwara

Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Eliuterius Hyera, aliyekuwa Mkuu wa Kituo Kidogo cha Polisi Chiungutwa wilayani Masasi, amefariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa risasi na askari mwenzie.

Taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Nicodemus Katembo leo Februari 03, 2024, imeeleza kuwa askari hao walikuwa kwenye jukumu la ukamataji wa mtuhumiwa anayedaiwa kuvunja ofisi (Haikutajwa) na kuiba.

“Mtuhumiwa huyo alianza kukimbia ili asikamatwe ndipo Askari aliyekuwa na bastola alipofyatua risasi kwa lengo la kufanikisha ukamataji na ikapelekea kumjeruhi Mkaguzi huyo.

Juhudi za kuokoa maisha yake zilifanyika kwa kupelekwa Hospitali ya Ndanda ambapo alifariki dunia akiendelea na matibabu.” Imeeleza taarifa ya ACP Katembo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitalini hapo kwa uchunguzi zaidi, huku mtuhumiwa akiendelea kushikiliwa kwa hatua zaidi za kisheria.

Source - CloudsTv

Jamaa wanajua kulindana sana….kwa haya maelezo kesi imeisha hapo….ukisoma kwa umakini hii habari utajua kuna vitu vingi vimefichwa!
 
Mungu wetu halali, huyo mwizi anakila sababu ya kuishi kama police wengine.
 
Masai wa zanziber waajiriwe jeshini tu, watunyooshe
 
Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Eliuterius Hyera, aliyekuwa Mkuu wa Kituo Kidogo cha Polisi Chiungutwa wilayani Masasi, amefariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa risasi na askari mwenzie.

Taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Nicodemus Katembo leo Februari 03, 2024, imeeleza kuwa askari hao walikuwa kwenye jukumu la ukamataji wa mtuhumiwa anayedaiwa kuvunja ofisi (Haikutajwa) na kuiba.

“Mtuhumiwa huyo alianza kukimbia ili asikamatwe ndipo Askari aliyekuwa na bastola alipofyatua risasi kwa lengo la kufanikisha ukamataji na ikapelekea kumjeruhi Mkaguzi huyo.

Juhudi za kuokoa maisha yake zilifanyika kwa kupelekwa Hospitali ya Ndanda ambapo alifariki dunia akiendelea na matibabu.” Imeeleza taarifa ya ACP Katembo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitalini hapo kwa uchunguzi zaidi, huku mtuhumiwa akiendelea kushikiliwa kwa hatua zaidi za kisheria.

Source - CloudsTv
Wakubwa waache Kutembea na Wake za Askari wadogo tafadhali kwani wenye Wake hubeba Roho za Visasi ambavyo huvisindikiza katika Matukio yatakayowabeba kuwa ni Oparesheni tu za Kijeshi ambapo Mmoja akifa / akiuwawa hiyo itaitwa ni bahati mbaya.
 
Back
Top Bottom