"Askari" aonekana akimwekea Davis Mosha kitu mfukoni

Kweli kaweka kitu na nafikiri jaamaa aliye juu kaona mchezo huo
!
!
Ndio.... Kamwekea Kitu Mfukoni.
Angalia vzr ni kweli huyo jamaa katoa kitu mfukoni mwake akamuwekea Davis kisha akamsukuma.
Hizo mbinu walisoma zamani kabla ya tekinolojia na wao wanaendelea kuzitumia ka kukariri bila kujua teknolojia inawaumbua, kwa mwendo huo kamwe hatutafika maana ni full mawazo mgando
ingawa wanasema heshimu uwezo wa mtu wa kufikiri ila mida fulani lazima kuhoji uwezo wa watanzania, kwa nini hutumia hisia kufanya hitimisho?
 
Nimeangalia kwa makini clip ya askari waliojifanya kuwa wa IMMIGRATION waliokwenda kwa Davis Mosha,Mmoja wa hao "maaskari" aliyevaa shati la kijivu alimsogelea kwa kumvizia Davis Mosha wakati wakibishana na hao "askari feki" akamuwekea kitu mfukoni halafu akamsukuma. Tumesikia kuwa Davis Mosha alipelekwa polisi.....Ninahisi kuwa aidha walimtilia bangi au Dawa za kulevya au simu waliyosema aliwanyang'anya wao. Aliyevaa shati la kijivu anafanana na yule aliyemtolea Nape Nnauye bastola mwaka jana.
Inasikitisha kuona nchi yetu inaharibiwa na hao askari wa Makonda. Huo ni mfano mwingine wa aina ya uvamizi unaofanywa na askari wa Makonda, ukianzia Clouds TV, Utekaji wa Roma Mkatoliki na uvamizi kwenye kituo cha mafuta cha Peter Zakaria huko mkoani Mara. Aina hiyo ya uvamizi na utekaji unafanana kwa namna moja au nyingine hivyo inaonekana mpangaji wa hayo maovu inawezekana akawa mtu mmoja ambaye si mwenye akili kabisa, Tumefikia pabaya kwa mambo yanayotokea nchini mwetu imekuwa kama Uganda wakati wa Idi Amin na Malyamungu walivyokuwa wakitumia vikosi vya State Bureau kuteka na kuua (au kupoteza watu....Kama anavyosema Jerry Muro) Hiyo link hapo chini utaona video yote. Kama utaclick na itashindwa kufanya kazi copy

Hawa ni kama wale walioenda kwa Zakaria!hivi kwa nini kazi za polisi zimeingiliwa????halafu hilo jeshi halipo kikatiba
 
Sawa Mosha ana ubabe wa kipumbavu na kwanini azuie Maafisa Uhamiaji kufanya kazi zao, lakini je mna maoni gani na mashaka ya mleta mada kwamba huyo jamaa kaweka kitu mfukoni mwa Mosha?

Ukiangalia, unaona wazi jinsi huyo askari anavyoingiza mkono mfukoni mwake kisha anaenda kumbana Mosha upande wa kushoto!!
Yaani na wewe unathubutu kabisa kusema UNAONA WAZI. kazi kweli kweli.
 
Kupitia huyu tunapata picha kwamba wapo watanzania wengi wanateseka kwa kesi za kubambikiwa kama hizi. Ikigundulika ukweli kwenye hili, itakua vyema mahakama ikachukua hatua kali dhidi ya hao maafisa na mkuu wao wa operation ili iwe fundisho.
Kwani hapo Mosha kabambikiziwa kesi gani?
 
Ila wabongo sie kwa kutunga lol unkiangalia vizuri jamaa aliweka alitoa mkono mgukoni lengo ni kutaka kumshika mtuhumiwa hata alipogeuka utaona shati yake imekunjana na mkanda wa suruali kuweni makini na hisia zenu
Nami km nimeona hivyo ,dizaini alitaka kumpiga Tanganyika jeki ,akawahiwa
 
Kwani hapo Mosha kabambikiziwa kesi gani?
Endelea kufatilia hiyo kesi utasikia kunakitu alikamatwa nacho. Binafsi siumii kwan nmesikia ndiye mfadhiri wa hao watesi so kama wamegeukana ni jambo la kheri. Inawezekana ndivo Mungu ameamua watesi waanze kupukutika namna hiyo!
 
Ukiangalia kwa makini huyo mwenye shati la kijivu ametoa kitu mfukoni kwake akamsogelea Davis Mosha (Akajiweka upande kwa upande au kwa kiingereza "side by side" Kwa mkono wa kulia ambao aliufunga/aliukunja alipoutoa mfukoni mwake akaingiza kwenye mfuko wa suruali wa kushoto wa suruali wa Davis Mosha wakati huo akitumia mkono wa kushoto kumsukuma Mosha. Ukiangalia kwa makini mkono wa kulia wa huyo "askari"baada ya kuuingiza mfukoni kwa Davis Mosha akautoa ukiwa hauna kitu (Tofauti na mwanzo) halafu akatumia mikono yake miwili kumsukuma Mosha. Angalia kwa makini alichokuwa akifanya...kuwa "Detail oriented" Suruali kubana siyo tatizo kwa sababu si lazima alichowekewa siyo lazima kiwe kikubwa pia kumbuka hiyo suruali Davis Mosha anatumia hiyo mifuko ya suruali aidha kuwekea walet au inatosha pia kuweka mikono yake, hivyo suruali kubana siyo tija. Hapo yeyote mwenye macho na akili timamu anaona kilichotokea. Hapo ni simply kubambikiza....Hiyo system ya kubambikiza siyo ngeni hapa Tanzania hao polisi uchwara na polisi wa kawaida ni kitu wanachofanya siku zote. LINI HUU UONEVU UTAKWISHA?
Nadhani ni hisia zako tu. Mifuko imebana namna hiyo siyo rahisi. Tajiri yako kachemsha. mwambie hii awamu siyo ya Kiwete ambayo mwenye fedha ndiye ''aliyejua'' sheria!
 
Msingi wa hoja hii umeuelewa lakini mkuu?
Umeeleweka sana. Labda wewe ndiyo hujaelewa. Kwa hiyo hao maofisa walijua kabisa kuwa Mosha angefanya vurugu na wakati wa vurugu watakuwa na chance ya kumwekea kitu mfukoni?
 
Hoja sio kama alifanikiwa kuweka au hapana bali hoja ni dhamira ya huyo jamaa!! Hoja yako ni sahihi, kutokana na suruali ya Mosha kubana, inawezekana zoezi lilishindikana lakini je, si inaonesha alikuwa na hiyo nia?
Swali: Hao maofisa kabla ya kwenda walijua kabisa kuwa ni lazima Mosha atafanya vurugu, na kuwasukuma sukuma hivyo watapata muda wa kumwekea kitu mfukoni wakati wa vurugu?
 
Nimeangalia kwa makini clip ya askari waliojifanya kuwa wa IMMIGRATION waliokwenda kwa Davis Mosha,Mmoja wa hao "maaskari" aliyevaa shati la kijivu alimsogelea kwa kumvizia Davis Mosha wakati wakibishana na hao "askari feki" akamuwekea kitu mfukoni halafu akamsukuma. Tumesikia kuwa Davis Mosha alipelekwa polisi.....Ninahisi kuwa aidha walimtilia bangi au Dawa za kulevya au simu waliyosema aliwanyang'anya wao. Aliyevaa shati la kijivu anafanana na yule aliyemtolea Nape Nnauye bastola mwaka jana.
Inasikitisha kuona nchi yetu inaharibiwa na hao askari wa Makonda. Huo ni mfano mwingine wa aina ya uvamizi unaofanywa na askari wa Makonda, ukianzia Clouds TV, Utekaji wa Roma Mkatoliki na uvamizi kwenye kituo cha mafuta cha Peter Zakaria huko mkoani Mara. Aina hiyo ya uvamizi na utekaji unafanana kwa namna moja au nyingine hivyo inaonekana mpangaji wa hayo maovu inawezekana akawa mtu mmoja ambaye si mwenye akili kabisa, Tumefikia pabaya kwa mambo yanayotokea nchini mwetu imekuwa kama Uganda wakati wa Idi Amin na Malyamungu walivyokuwa wakitumia vikosi vya State Bureau kuteka na kuua (au kupoteza watu....Kama anavyosema Jerry Muro) Hiyo link hapo chini utaona video yote. Kama utaclick na itashindwa kufanya kazi copy

Huyu askali ni mpuuzi kweli kweli, yaani katoa kitu kabisa na kumuwekea Davis. Nadhani tusihusishe na Makonda au serikali, hilo ni suala la maadili ya mtu binafsi. Nadhani dunia nzima imeona jinsi askali wetu wasivyokuwa na maadili
 
Back
Top Bottom