Askari feki wakamatwa wakiwa na AK 47 bandia

Askari feki wakamatwa wakiwa na AK 47 bandia

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, limeendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda usalama wa raia na mali zao kwa kuimarisha doria, misako na operesheni mbalimbali za wahalifu pamoja na usalama barabarani, na kuendelea kushirikisha wananchi katika kubaini, kuzuia na kudhibiti uhalifu nchini.

Katika operesheni yake ya mwezi Agosti hadi Septemba 2026 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi limefanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 441 kwa tuhuma za makosa mbalimbali ya jinai ikiwa ni pamoja na watuhumiwa watatu kwa kujifanya watumishi wa Serikali katika vyombo vya Dola hukuwakiwa na sare zinazofanana na sare za Jeshi la Polisi Tanzania, silaha bandia pamoja na vitu vingine.

Soma Pia: Tabora: Watu 6 ikiwemo askari wauawa, silaha ya kivita AK-47 yachukuliwa

#HABARI- Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, limeendelea kutekeleza majukumu yake ya kulin.webp
#HABARI- Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, limeendelea kutekeleza majukumu yake ya kul...webp
 
Tukiachana na hao waliokutwa na sare,Je kukutwa na silaha bandia ndani ila hujatishia mtu ni kosa.

BTW:Inabidi kuwadindia watekaji kwa sasa mpaka uthibitishe silaha ni OG au toy!!😁
 
Back
Top Bottom