Nilikuwa nasafiri kwa gari binafsi kama dereva kutoka Chalinze kwenda Tanga,Nilipofika check point ya KABUKU nikazuiliwa na maaskari nikituhumiwa kulipita gari la mbele yangu(overtaking) sehemu isiyoruhusiwa kijiji cha nyuma kama km 45. Nikawauliza maaskari mbona hakuna askari aliyenisimamisha kwenye eneo la tukio na kunihoji juu ya hilo?wakaniambia walikuwepo na wameniona nikivunja hiyo sheria. Baada ya nusu saa ya mabishano makali wakaja maaskari wakiwa na civilian car na kudai wao ndio walioniona wakiwa ndani kwenye hiyo gari yao!nikaandikiwa notification nikalipa nakuendelea na safari yangu.
Swali langu linakuja,je nilitendewa haki kutuhumiwa na baadae kulipishwa faini na askari aliyekuwa amejificha ndani ya gari?sheria inasemaje hapo naomba ufafanuzi
Swali langu linakuja,je nilitendewa haki kutuhumiwa na baadae kulipishwa faini na askari aliyekuwa amejificha ndani ya gari?sheria inasemaje hapo naomba ufafanuzi