Dah umenikumbusha mbali sana ulipolitaja hilo neno "Moral Authority" na ambalo lina mahusiano na hawa wenzake akina Moral Autonomy, Moral Dilemma, Moral Ethics, Morality, nk!! Hakika somo la Ethics ni tamu sana.Tatizo ni kuwa Hakuna mwenye uhalali (moral authority) wa kufuatilia na kuadhibu wakosaji kwa sababu wakubwa wenyewe wanayo mamlaka isiyo halali, maana wapo hapo walipo kupitia wizi wa kura
Life hii usipojiongeza utatia huruma huko mbele na mtu wa kukupa msaada hayupo ukute katika life yake kasomesha watoto vizuri na kusaidia sana watu kila akipata mshahara hakuna kitu anachobaki nacho bora angekopa Bank akiwa kazini ajenge banda lolote na popote kuliko kulia kwa Wasaga sumu hakuna kitu watamsaidia zaidi ya kumtoa tu.Halafu kastaafu na 56yrs, duh maisha haya. Amemaliza nguvu zake Huko, sasa hivi Hana hata kibanda cha kujihifadhi
Hakuna kuwalipa hao,Chadema wakiwatetea mnajidai kuwapiga
Mkuu ukishaona umekulia na kupata kazi kwenye nchi kama hii acha kuitegemea serikali kwenye kila kitu vitu vingine ni vya kujiongeza yaani tangu 1983 hadi sasa umeshindwa hata kujenga vyumba viwili vya kupangisha alafu unabaki unaitegemea serikali hii yenye wapigaji ikupe mafao. Tuache kuitegemea serikali kwenye kila kitu.
asilipwe kabisa,maana huenda ni karma labda inamtafuna huyo mstaafu,Mzee John Samwel Swai(61) mstaafu wa Jeshi la Polisi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumsaidia asiondolewe katika kambi anayoishi kwani bado hajalipwa fedha za mizigo pamoja na fedha za likizo ambazo anapaswa kulipwa.
.Mzee huyo alistaafu mwaka 2020 baada ya kutumikia jeshi la polisi kuanzia mwaka 1983 amedai kupewa barua na Mkuu wa Kambi za Polisi inayomtaka kuhama ndani ya siku saba kuanzia Februari 04 mpaka leo Februari 10 na endapo asipohama vitu vyake vitatolewa nje.
Kupitia barua aliyopewa tarehe nne mwezi huu imesema “Umeariwa kukabidhi nyumba tajwa hapo juu, kwani umeshastaafu kazi toka 2020.
Oc Barracks amekuamuru kukabidhi nyumba tajwa hapo juu kwa kuwa umestaafu kazi. Umepewa siku 07 kuanzia leo tarehe 04/02/2025 hadi 10/02/2025 uwe tayari umekabidhi nyumba hiyo, Kushindwa kutekeleza amri hii, vitu vyako vitatolewa nje, hivyo unaamriwa kuviondoa mwenyewe kabla ya kutolewa”
Mzee Swai amewaomba wasaidizi wa Rais ambao Jeshi la Polisi lipo chini yao akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kumsaidia wakati huo serikali ikiendelea kushuhulikia malipo yao.
Jambo TV imefanya jitihda za kumtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime kwa njia ya simu lakini jitihada hazikuzaa matunda.
why?asilipwe kabisa
Sio wote kuna wanaocheza madili wana nyumba na viwanja vya kutosha madili machafu machafu
Ili wapate laana hao wasiomlipawhy?
Angekuwa mwanajeshi wa JWTZ kule MIRAMBO BARRACKS TABORA Wala hata asingefukuzwa maana kule nyumba zingine ni makazi ya popo yani zile kota tangu mwaka 2009 zilikuwa zimeanza kukosa wakaaji kabisa.Mzee John Samwel Swai(61) mstaafu wa Jeshi la Polisi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumsaidia asiondolewe katika kambi anayoishi kwani bado hajalipwa fedha za mizigo pamoja na fedha za likizo ambazo anapaswa kulipwa.
.Mzee huyo alistaafu mwaka 2020 baada ya kutumikia jeshi la polisi kuanzia mwaka 1983 amedai kupewa barua na Mkuu wa Kambi za Polisi inayomtaka kuhama ndani ya siku saba kuanzia Februari 04 mpaka leo Februari 10 na endapo asipohama vitu vyake vitatolewa nje.
Kupitia barua aliyopewa tarehe nne mwezi huu imesema “Umeariwa kukabidhi nyumba tajwa hapo juu, kwani umeshastaafu kazi toka 2020.
Oc Barracks amekuamuru kukabidhi nyumba tajwa hapo juu kwa kuwa umestaafu kazi. Umepewa siku 07 kuanzia leo tarehe 04/02/2025 hadi 10/02/2025 uwe tayari umekabidhi nyumba hiyo, Kushindwa kutekeleza amri hii, vitu vyako vitatolewa nje, hivyo unaamriwa kuviondoa mwenyewe kabla ya kutolewa”
Mzee Swai amewaomba wasaidizi wa Rais ambao Jeshi la Polisi lipo chini yao akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kumsaidia wakati huo serikali ikiendelea kushuhulikia malipo yao.
Jambo TV imefanya jitihda za kumtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime kwa njia ya simu lakini jitihada hazikuzaa matunda.
ndio wamsaidie hao wakubwaHao wadogo wadogo Huwa wanatumia tu kutekeleza amri za wakubwa zao