Askari Mstaafu: Sijalipwa stahiki zangu, Polisi wamenipa Siku 7 nikabidhi nyumba la sivyo vitu vyangu vitatolewa nje

Askari Mstaafu: Sijalipwa stahiki zangu, Polisi wamenipa Siku 7 nikabidhi nyumba la sivyo vitu vyangu vitatolewa nje

Tatizo ni kuwa Hakuna mwenye uhalali (moral authority) wa kufuatilia na kuadhibu wakosaji kwa sababu wakubwa wenyewe wanayo mamlaka isiyo halali, maana wapo hapo walipo kupitia wizi wa kura
Dah umenikumbusha mbali sana ulipolitaja hilo neno "Moral Authority" na ambalo lina mahusiano na hawa wenzake akina Moral Autonomy, Moral Dilemma, Moral Ethics, Morality, nk!! Hakika somo la Ethics ni tamu sana.
 
Mbona kuhusu mafao ya kustaafu hajasema.
Pesa za mafao kapeleka wapi?
Huyu dingi karogwa au kapigwa na laana maana ile kazi laana nje nje.
Miaka 5 aliyokaa bure kwenye hiyo barrack kama angekuwa anachajiwa kodi angetakiwa kulipwa zaidi ya million 15.
Kwahiyo wamelipana juu kwa juu ahame
 
Karma, inaonekana aliumiza mioyo ya watu wengi akiwa kazini, sasa anaumizwa yeye!
 
Halafu kastaafu na 56yrs, duh maisha haya. Amemaliza nguvu zake Huko, sasa hivi Hana hata kibanda cha kujihifadhi
Life hii usipojiongeza utatia huruma huko mbele na mtu wa kukupa msaada hayupo ukute katika life yake kasomesha watoto vizuri na kusaidia sana watu kila akipata mshahara hakuna kitu anachobaki nacho bora angekopa Bank akiwa kazini ajenge banda lolote na popote kuliko kulia kwa Wasaga sumu hakuna kitu watamsaidia zaidi ya kumtoa tu.
 
Hakuna kuwalipa hao,Chadema wakiwatetea mnajidai kuwapiga

Wekeni sera zinazohusu maisha ya kila mtu .
Nilikua vijiweni nikiwa upande wa Lisu kwenye uchaguzi ndani ya Chama .
Watanzania wengi wanamkubali Lisu . Hata mapolisi wengi wanaonekana walifurahishwa na ushindi wa Lisu kuongoza Chadema .

Kinachowakwaza wengi ni kauli za Lisu dhidi ya Magufuli . Hapo kwa kweli Wanapishana na Lisu . Wengi hasa ukanda wenye watu wengi kama wa Kanda ya Ziwa wanaamini kuwa Magufuli alikua mzalendo ukilinganisha na Samia, Kikwete , Mkapa na Mwiinyi .
Ni kweli Magufuli alikua na mapungufu yake lakini ameshakufa yuko huko anajibu mbele za Mwenyezi Mungu. Kwa nini tusimwachie Mungu ahukumu.
Kwa nini Lisu anaendelea kuiumiza familia yake ,ndugu zake na kabila lake ambalo wanaona walimpoteza Shujaa wao ?

Kuisambaratisha CCM na kuliwavutia wana usalama wengi hasa wenye Asili ya Kanda ya Ziwa ni ama kuachana na siasa za kumkashifuuw Magufuli au kuongelea mazuri yake . Lakini naona vizuri zaidi ni kukam kimya na kutangaza msamaha ili Mungu ajibu . Vinginevyo Kisu atapata ushindi Mdogo kama ule dhidi ya Mbowe .

Lisu anatakiwa arejee somo la kumsema sana Mbowe .
Ilijenga chuki na wengi wakapiga kura za huruma kwa Mbowe. Lakini angesimamia sera zake tu na kuepuka kumjadili Mbise bila shaka angepata kura nyingi sana na huenda mbowe angejitoa mapema kabisa .
Siasa ni sayansi inabidi usome saikolojia ya Wapiga kura.
 
Mkuu ukishaona umekulia na kupata kazi kwenye nchi kama hii acha kuitegemea serikali kwenye kila kitu vitu vingine ni vya kujiongeza yaani tangu 1983 hadi sasa umeshindwa hata kujenga vyumba viwili vya kupangisha alafu unabaki unaitegemea serikali hii yenye wapigaji ikupe mafao. Tuache kuitegemea serikali kwenye kila kitu.

Yeye amejenga Mwanza, sasa unataka abebe mizigo kichwani .
Yaani atumie zaidi ya mil mbili kubeba mizigo halafu aanze safari za kuja DSM kufuatilia haki zake.

Yuko sahihi kabisa .
Mifumo ya rushwa haijali haki za watu . Watu wamekula pesa zake wakijua wazi kuwa ataondoka tu kwa sababu kuna watu wa kutetea uovu wao.

Amewaumbua mafisafisadi .
Kila mwaka bajeti ya kulipa madeni inapitishwa na bunge halafu miaka karibu sita haijalipwa . Wetu wanalipa na kwa rushwa na kujuana halafu asidai haki yake ili aonekane amejenga . Wewe uliona wapi mchaga hajui namna ya kuanzisha biashara ? Yule anadai chake . Wewe una kabiashara kako utoe mil. Mbili za nauli wakati yupo nje ya system ya kupata maslahi ya bure bure . Wampe hela zake akaishia Mwanza waone kama ataenda kuishi kwenye nyumba ya mtu ya bure .
 
Mzee John Samwel Swai(61) mstaafu wa Jeshi la Polisi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumsaidia asiondolewe katika kambi anayoishi kwani bado hajalipwa fedha za mizigo pamoja na fedha za likizo ambazo anapaswa kulipwa.

.Mzee huyo alistaafu mwaka 2020 baada ya kutumikia jeshi la polisi kuanzia mwaka 1983 amedai kupewa barua na Mkuu wa Kambi za Polisi inayomtaka kuhama ndani ya siku saba kuanzia Februari 04 mpaka leo Februari 10 na endapo asipohama vitu vyake vitatolewa nje.

Kupitia barua aliyopewa tarehe nne mwezi huu imesema “Umeariwa kukabidhi nyumba tajwa hapo juu, kwani umeshastaafu kazi toka 2020.

Oc Barracks amekuamuru kukabidhi nyumba tajwa hapo juu kwa kuwa umestaafu kazi. Umepewa siku 07 kuanzia leo tarehe 04/02/2025 hadi 10/02/2025 uwe tayari umekabidhi nyumba hiyo, Kushindwa kutekeleza amri hii, vitu vyako vitatolewa nje, hivyo unaamriwa kuviondoa mwenyewe kabla ya kutolewa”

Mzee Swai amewaomba wasaidizi wa Rais ambao Jeshi la Polisi lipo chini yao akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kumsaidia wakati huo serikali ikiendelea kushuhulikia malipo yao.

Jambo TV imefanya jitihda za kumtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime kwa njia ya simu lakini jitihada hazikuzaa matunda.
asilipwe kabisa,maana huenda ni karma labda inamtafuna huyo mstaafu,
Samia ni msikivu najua kilio chake kitamfikoa
 
Na jamii yetu ndiyo inawataka na kuwasifia . Ndio maana kwa sasa jamii imeoza mpaka viongozi wa dini .
Ndio maana manabii wanauza mpaka udongo ili kupata pesa badae wasije wakatukanwa na kuitwa wajinga.
Kuna askofu mmoja wa KKKT alifanya ufisadi mkubwa ili ajilimbikizie mali akistaafu asije akatukanwa.
Aliachia kanisa deni kubwa sana kwa waumini
Sio wote kuna wanaocheza madili wana nyumba na viwanja vya kutosha madili machafu machafu
 
Mzee John Samwel Swai(61) mstaafu wa Jeshi la Polisi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumsaidia asiondolewe katika kambi anayoishi kwani bado hajalipwa fedha za mizigo pamoja na fedha za likizo ambazo anapaswa kulipwa.

.Mzee huyo alistaafu mwaka 2020 baada ya kutumikia jeshi la polisi kuanzia mwaka 1983 amedai kupewa barua na Mkuu wa Kambi za Polisi inayomtaka kuhama ndani ya siku saba kuanzia Februari 04 mpaka leo Februari 10 na endapo asipohama vitu vyake vitatolewa nje.

Kupitia barua aliyopewa tarehe nne mwezi huu imesema “Umeariwa kukabidhi nyumba tajwa hapo juu, kwani umeshastaafu kazi toka 2020.

Oc Barracks amekuamuru kukabidhi nyumba tajwa hapo juu kwa kuwa umestaafu kazi. Umepewa siku 07 kuanzia leo tarehe 04/02/2025 hadi 10/02/2025 uwe tayari umekabidhi nyumba hiyo, Kushindwa kutekeleza amri hii, vitu vyako vitatolewa nje, hivyo unaamriwa kuviondoa mwenyewe kabla ya kutolewa”

Mzee Swai amewaomba wasaidizi wa Rais ambao Jeshi la Polisi lipo chini yao akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kumsaidia wakati huo serikali ikiendelea kushuhulikia malipo yao.

Jambo TV imefanya jitihda za kumtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime kwa njia ya simu lakini jitihada hazikuzaa matunda.
Angekuwa mwanajeshi wa JWTZ kule MIRAMBO BARRACKS TABORA Wala hata asingefukuzwa maana kule nyumba zingine ni makazi ya popo yani zile kota tangu mwaka 2009 zilikuwa zimeanza kukosa wakaaji kabisa.
 
Mzee John Samwel Swai(61) mstaafu wa Jeshi la Polisi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumsaidia asiondolewe katika kambi anayoishi kwani bado hajalipwa fedha za mizigo pamoja na fedha za likizo ambazo anapaswa kulipwa.

Mzee huyo alistaafu mwaka 2020 baada ya kutumikia jeshi la polisi kuanzia mwaka 1983 amedai kupewa barua na Mkuu wa Kambi za Polisi inayomtaka kuhama ndani ya siku saba kuanzia Februari 04 mpaka leo Februari 10 na endapo asipohama vitu vyake vitatolewa nje.

Kupitia barua aliyopewa tarehe nne mwezi huu imesema “Umeariwa kukabidhi nyumba tajwa hapo juu, kwani umeshastaafu kazi toka 2020. Oc Barracks amekuamuru kukabidhi nyumba tajwa hapo juu kwa kuwa umestaafu kazi. Umepewa siku 07 kuanzia leo tarehe 04/02/2025 hadi 10/02/2025 uwe tayari umekabidhi nyumba hiyo, Kushindwa kutekeleza amri hii, vitu vyako vitatolewa nje, hivyo unaamriwa kuviondoa mwenyewe kabla ya kutolewa”

Mzee Swai amewaomba wasaidizi wa Rais ambao Jeshi la Polisi lipo chini yao akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kumsaidia wakati huo serikali ikiendelea kushuhulikia malipo yao.

Jambo TV imefanya jitihda za kumtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime kwa njia ya simu lakini jitihada hazikuzaa matunda.

Chanzo: Jambo TV
 
Sasa hapo Mzee asaidiwe kitu Gani yaani Toka 2020 almost miaka mi5 Bado unataka kuishi kambini? Au Sheria zao zinawaruhusu?
 
Back
Top Bottom