Hakuna kuwalipa hao,Chadema wakiwatetea mnajidai kuwapiga
Wekeni sera zinazohusu maisha ya kila mtu .
Nilikua vijiweni nikiwa upande wa Lisu kwenye uchaguzi ndani ya Chama .
Watanzania wengi wanamkubali Lisu . Hata mapolisi wengi wanaonekana walifurahishwa na ushindi wa Lisu kuongoza Chadema .
Kinachowakwaza wengi ni kauli za Lisu dhidi ya Magufuli . Hapo kwa kweli Wanapishana na Lisu . Wengi hasa ukanda wenye watu wengi kama wa Kanda ya Ziwa wanaamini kuwa Magufuli alikua mzalendo ukilinganisha na Samia, Kikwete , Mkapa na Mwiinyi .
Ni kweli Magufuli alikua na mapungufu yake lakini ameshakufa yuko huko anajibu mbele za Mwenyezi Mungu. Kwa nini tusimwachie Mungu ahukumu.
Kwa nini Lisu anaendelea kuiumiza familia yake ,ndugu zake na kabila lake ambalo wanaona walimpoteza Shujaa wao ?
Kuisambaratisha CCM na kuliwavutia wana usalama wengi hasa wenye Asili ya Kanda ya Ziwa ni ama kuachana na siasa za kumkashifuuw Magufuli au kuongelea mazuri yake . Lakini naona vizuri zaidi ni kukam kimya na kutangaza msamaha ili Mungu ajibu . Vinginevyo Kisu atapata ushindi Mdogo kama ule dhidi ya Mbowe .
Lisu anatakiwa arejee somo la kumsema sana Mbowe .
Ilijenga chuki na wengi wakapiga kura za huruma kwa Mbowe. Lakini angesimamia sera zake tu na kuepuka kumjadili Mbise bila shaka angepata kura nyingi sana na huenda mbowe angejitoa mapema kabisa .
Siasa ni sayansi inabidi usome saikolojia ya Wapiga kura.