MWANDENDEULE
JF-Expert Member
- May 24, 2015
- 4,099
- 7,466
Hayo malipo ya mabaya yote aliyofanya dhidi ya raia, akae kwa kutulia huku vitu vikitolewa nje kwa amri ya bosi wake wa zamani.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama hajalipwa hela yake ya mizigo anastahili kuhifadhiwa hadi hapo atakapolipwa.Dah!Kwa nini asishauriwe ahamie yeye na familia yake kwenye ofisi zinazotakiwa zimlipe anachodai?
Huyo mzee nayeye kazingua toka mwaka 1983 hadi 2020 hujaanzaisha hata vitega uchumi.
Mzee John Samwel Swai(61) mstaafu wa Jeshi la Polisi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumsaidia asiondolewe katika kambi anayoishi kwani bado hajalipwa fedha za mizigo pamoja na fedha za likizo ambazo anapaswa kulipwa.
.Mzee huyo alistaafu mwaka 2020 baada ya kutumikia jeshi la polisi kuanzia mwaka 1983 amedai kupewa barua na Mkuu wa Kambi za Polisi inayomtaka kuhama ndani ya siku saba kuanzia Februari 04 mpaka leo Februari 10 na endapo asipohama vitu vyake vitatolewa nje.
Kupitia barua aliyopewa tarehe nne mwezi huu imesema “Umeariwa kukabidhi nyumba tajwa hapo juu, kwani umeshastaafu kazi toka 2020.
Oc Barracks amekuamuru kukabidhi nyumba tajwa hapo juu kwa kuwa umestaafu kazi. Umepewa siku 07 kuanzia leo tarehe 04/02/2025 hadi 10/02/2025 uwe tayari umekabidhi nyumba hiyo, Kushindwa kutekeleza amri hii, vitu vyako vitatolewa nje, hivyo unaamriwa kuviondoa mwenyewe kabla ya kutolewa”
Mzee Swai amewaomba wasaidizi wa Rais ambao Jeshi la Polisi lipo chini yao akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kumsaidia wakati huo serikali ikiendelea kushuhulikia malipo yao.
Jambo TV imefanya jitihda za kumtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime kwa njia ya simu lakini jitihada hazikuzaa matunda.
Hayo malipo ya mabaya yote aliyofanya dhidi ya raia, akae kwa kutulia huku vitu vikitolewa nje kwa amri ya bosi wake wa zamani.
Sio wote labda Makada .Wengi wamestaafu na wapo kitaa.Na mwaka uhu walitakiwa kustaafu watu wengi wameongezewa muda mpaka mwakani
Mwaka uhuu hasa maafisa wakuu kuna baadhi watu wameongezewa mudaSio wote labda Makada .Wengi wamestaafu na wapo kitaa.
Mkuu ukishaona umekulia na kupata kazi kwenye nchi kama hii acha kuitegemea serikali kwenye kila kitu vitu vingine ni vya kujiongeza yaani tangu 1983 hadi sasa umeshindwa hata kujenga vyumba viwili vya kupangisha alafu unabaki unaitegemea serikali hii yenye wapigaji ikupe mafao. Tuache kuitegemea serikali kwenye kila kitu.Wakila Rushwa wakajenga kila mji watasema kuwa ni mali za laana .
Wale waadilifu wakidai haki zao mnawasema walikua wanakula Bata .
Kwa taarifa yako kula Bata hakizuii mtu kutajirika labda mfanya biashara wa halali lakini kwa mafanya kazi Bata ni Sehemu ya madili .
Mawaziri na marais wakiamua kulimbikiza mali kwa vizazi na vitukuu kwa sababu ya watanzania wasio na shukurani hatuwezi kuwalaumu .
Polisi wengi wanatoka familia maskini . Wategemezi ni wengi hawezi kujenga majumba mengi kwa sababu Nyumba standard sio chini ya mil.70 . Sasa ana madhara gani ambao utampa akiba ya kupata mil. 70 x 2 yaani mlo.140 wakati hata kuinua mgongo chake na kikokotoo hakifuki mili 25 . Yeye amesema amepanga Mwanza sasa huwezi kumlazimisha ajenge na Dar es salaam .
Kwa nini tusiwalaumu na kuwawajibisha wanaokalia haki zake huku wakigawa pikipiki na baiskeli za rushwa ya uchaguzi zaidi ya bil. 90. Pesa ambazo zingetosha kulipa madeni yote ya Polisi,wanajeshi na hata migambo ili wakiiba kura waibe . Unatoa rushwa mitaani kwa wapiga kura halafu bado unatumia polisi kuiba kura huo si ushetani kabisa . Kama unategemea kuiba kura pesa za rushwa peleka kwenye maendeleo kama alivyofanya Magufuli .
Mgosi, Nchi hii hakuna Watu wenye maisha magumu Sana kama Polisi (both economically na socially maybe na mentally)Policcm na wenyewe kumbe wanapitia mapito ya aina hii baada ya kustaafu! Pole nyingi kwao.
Halafu kastaafu na 56yrs, duh maisha haya. Amemaliza nguvu zake Huko, sasa hivi Hana hata kibanda cha kujihifadhiDaah Nchi zetu za Afrika tuna roho mbaya sana yaani mtu kafanya kazi miaka yote hiyo harafu stahiki zake apewi kwa wakati na nyumba anafukuzwa yaani hii inawafanya watu wengi wawe wala rushwa wakubwa...
TII AMRI BILA SHURUTI... ONDOKAMzee John Samwel Swai(61) mstaafu wa Jeshi la Polisi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumsaidia asiondolewe katika kambi anayoishi kwani bado hajalipwa fedha za mizigo pamoja na fedha za likizo ambazo anapaswa kulipwa.
.Mzee huyo alistaafu mwaka 2020 baada ya kutumikia jeshi la polisi kuanzia mwaka 1983 amedai kupewa barua na Mkuu wa Kambi za Polisi inayomtaka kuhama ndani ya siku saba kuanzia Februari 04 mpaka leo Februari 10 na endapo asipohama vitu vyake vitatolewa nje.
Kupitia barua aliyopewa tarehe nne mwezi huu imesema “Umeariwa kukabidhi nyumba tajwa hapo juu, kwani umeshastaafu kazi toka 2020.
Oc Barracks amekuamuru kukabidhi nyumba tajwa hapo juu kwa kuwa umestaafu kazi. Umepewa siku 07 kuanzia leo tarehe 04/02/2025 hadi 10/02/2025 uwe tayari umekabidhi nyumba hiyo, Kushindwa kutekeleza amri hii, vitu vyako vitatolewa nje, hivyo unaamriwa kuviondoa mwenyewe kabla ya kutolewa”
Mzee Swai amewaomba wasaidizi wa Rais ambao Jeshi la Polisi lipo chini yao akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kumsaidia wakati huo serikali ikiendelea kushuhulikia malipo yao.
Jambo TV imefanya jitihda za kumtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime kwa njia ya simu lakini jitihada hazikuzaa matunda.
Sio wote kuna wanaocheza madili wana nyumba na viwanja vya kutosha madili machafu machafuC Mon men, miaka 37 upo kazi ni, hujajenga hata kabanda! Huyu alikula bata tu,
Hapo ndipo anajiuliza kwanini hakuiba siku ile ilipotokea chance ya kuibaTII AMRI BILA SHURUTI... ONDOKA
Tatizo ni kuwa Hakuna mwenye uhalali (moral authority) wa kufuatilia na kuadhibu wakosaji kwa sababu wakubwa wenyewe wanayo mamlaka isiyo halali, maana wapo hapo walipo kupitia wizi wa kuraTuhuma za fedheha kama hizi zikifuatiliwa zinaweza kwenda na watu, sema nini, Serikali ya viongozi kula kwa urefu wa kamba zao, hakuna mtu atafanywa kitu.
Kula Rushwa kuna raha yake uzeeni,C Mon men, miaka 37 upo kazi ni, hujajenga hata kabanda! Huyu alikula bata tu,