Askari Mstaafu: Sijalipwa stahiki zangu, Polisi wamenipa Siku 7 nikabidhi nyumba la sivyo vitu vyangu vitatolewa nje

Dah!Kwa nini asishauriwe ahamie yeye na familia yake kwenye ofisi zinazotakiwa zimlipe anachodai?
Kama hajalipwa hela yake ya mizigo anastahili kuhifadhiwa hadi hapo atakapolipwa.

Cha kujiuliza, mwaka wa 6 huu, hela ya mizigo ilipelekwa kumlipa nani kwa miaka yote na bajeti yake ipo?

Officer in Command(Oc) wa hiyo kambi kafanya makusudi kumfukuza ili kuuangalia mnyororo wa uwajibikaji.

Hizo fedha zitakuwa zililiwa na kiongozi au bwana fedha alizipiga.

Tuhuma za fedheha kama hizi zikifuatiliwa zinaweza kwenda na watu, sema nini, Serikali ya viongozi kula kwa urefu wa kamba zao, hakuna mtu atafanywa kitu.

Natumaini taarifa hii itapush mambo yake kushuhulikiwa haraka.
 
Huyo mzee nayeye kazingua toka mwaka 1983 hadi 2020 hujaanzaisha hata vitega uchumi.

Wakila Rushwa wakajenga kila mji watasema kuwa ni mali za laana .
Wale waadilifu wakidai haki zao mnawasema walikua wanakula Bata .
Kwa taarifa yako kula Bata hakizuii mtu kutajirika labda mfanya biashara wa halali lakini kwa mafanya kazi Bata ni Sehemu ya madili .

Mawaziri na marais wakiamua kulimbikiza mali kwa vizazi na vitukuu kwa sababu ya watanzania wasio na shukurani hatuwezi kuwalaumu .

Polisi wengi wanatoka familia maskini . Wategemezi ni wengi hawezi kujenga majumba mengi kwa sababu Nyumba standard sio chini ya mil.70 . Sasa ana madhara gani ambao utampa akiba ya kupata mil. 70 x 2 yaani mlo.140 wakati hata kuinua mgongo chake na kikokotoo hakifuki mili 25 . Yeye amesema amepanga Mwanza sasa huwezi kumlazimisha ajenge na Dar es salaam .

Kwa nini tusiwalaumu na kuwawajibisha wanaokalia haki zake huku wakigawa pikipiki na baiskeli za rushwa ya uchaguzi zaidi ya bil. 90. Pesa ambazo zingetosha kulipa madeni yote ya Polisi,wanajeshi na hata migambo ili wakiiba kura waibe . Unatoa rushwa mitaani kwa wapiga kura halafu bado unatumia polisi kuiba kura huo si ushetani kabisa . Kama unategemea kuiba kura pesa za rushwa peleka kwenye maendeleo kama alivyofanya Magufuli .
 
Na mwaka uhu walitakiwa kustaafu watu wengi wameongezewa muda mpaka mwakani
 
Mzee John Samwel Swai(61) mstaafu wa Jeshi la Polisi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumsaidia asiondolewe katika kambi anayoishi kwani bado hajalipwa fedha za mizigo pamoja na fedha za likizo ambazo anapaswa kulipwa.

.Mzee huyo alistaafu mwaka 2020 baada ya kutumikia jeshi la polisi kuanzia mwaka 1983 amedai kupewa barua na Mkuu wa Kambi za Polisi inayomtaka kuhama ndani ya siku saba kuanzia Februari 04 mpaka leo Februari 10 na endapo asipohama vitu vyake vitatolewa nje.

Kupitia barua aliyopewa tarehe nne mwezi huu imesema “Umeariwa kukabidhi nyumba tajwa hapo juu, kwani umeshastaafu kazi toka 2020.

Oc Barracks amekuamuru kukabidhi nyumba tajwa hapo juu kwa kuwa umestaafu kazi. Umepewa siku 07 kuanzia leo tarehe 04/02/2025 hadi 10/02/2025 uwe tayari umekabidhi nyumba hiyo, Kushindwa kutekeleza amri hii, vitu vyako vitatolewa nje, hivyo unaamriwa kuviondoa mwenyewe kabla ya kutolewa”

Mzee Swai amewaomba wasaidizi wa Rais ambao Jeshi la Polisi lipo chini yao akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kumsaidia wakati huo serikali ikiendelea kushuhulikia malipo yao.

Jambo TV imefanya jitihda za kumtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime kwa njia ya simu lakini jitihada hazikuzaa matunda.

Kwa kuwa Jeshi la Polisi pamoja na Mapolisi wenyewe huwa hawawatendei Haki raia wa kawaida, sioni tatizo hata kidogo kwa huyo Askari Polisi mstaafu kufanyiwa dhuluma juu ya stahiki zake.
Muosha huoshwa!
Hakuna kitu kibaya hapo.

Good for the Jews is good for the gunners, and bad for the Jews is bad for the gunners!
 
Hayo malipo ya mabaya yote aliyofanya dhidi ya raia, akae kwa kutulia huku vitu vikitolewa nje kwa amri ya bosi wake wa zamani.

Wanaofanya mabaya wanaogelea kwenye magunia ya pesa mkuu.

Walimteka mtu wanaanza na akaunti yake kwanza .
Huyo mpaka akajitokeza hadharani badi ujue alikua mwadilifu sana .
Kazi za umma au biashara mtu mwadilifu anapata changamoto kubwa sana kufikia maisha bora . Zaidi anakua na amani tu moyoni lakini sio mali .

Tusiwadanganye watu kuwa wale wasio na mali ni watu wala rushwa au wanaonyima wetu haki zao.
Hivi kwa mfano Daktari alihudumia watu kwa haki bila rushwa na yule anayeweka mbele pesa ni yupi jioni anapata pesa ya kuweka gari mafuta kwa urahisi ? Yupi mshahara wake utakaa bila kutumika.

Tunatakiwa tuwatie moyo labda pawe na ushahidi usio na shaka kuwa alikua ni mtu wa kudhulumu wetu. Lakini hapo ameshutumiwa na serikali ambayo tunaipa kodi kwa ajili ya watumishi wake wachache kulinganisha na wingi wa watu mil.65 .
 
Wakila Rushwa wakajenga kila mji watasema kuwa ni mali za laana .
Wale waadilifu wakidai haki zao mnawasema walikua wanakula Bata .
Kwa taarifa yako kula Bata hakizuii mtu kutajirika labda mfanya biashara wa halali lakini kwa mafanya kazi Bata ni Sehemu ya madili .

Mawaziri na marais wakiamua kulimbikiza mali kwa vizazi na vitukuu kwa sababu ya watanzania wasio na shukurani hatuwezi kuwalaumu .

Polisi wengi wanatoka familia maskini . Wategemezi ni wengi hawezi kujenga majumba mengi kwa sababu Nyumba standard sio chini ya mil.70 . Sasa ana madhara gani ambao utampa akiba ya kupata mil. 70 x 2 yaani mlo.140 wakati hata kuinua mgongo chake na kikokotoo hakifuki mili 25 . Yeye amesema amepanga Mwanza sasa huwezi kumlazimisha ajenge na Dar es salaam .

Kwa nini tusiwalaumu na kuwawajibisha wanaokalia haki zake huku wakigawa pikipiki na baiskeli za rushwa ya uchaguzi zaidi ya bil. 90. Pesa ambazo zingetosha kulipa madeni yote ya Polisi,wanajeshi na hata migambo ili wakiiba kura waibe . Unatoa rushwa mitaani kwa wapiga kura halafu bado unatumia polisi kuiba kura huo si ushetani kabisa . Kama unategemea kuiba kura pesa za rushwa peleka kwenye maendeleo kama alivyofanya Magufuli .
Mkuu ukishaona umekulia na kupata kazi kwenye nchi kama hii acha kuitegemea serikali kwenye kila kitu vitu vingine ni vya kujiongeza yaani tangu 1983 hadi sasa umeshindwa hata kujenga vyumba viwili vya kupangisha alafu unabaki unaitegemea serikali hii yenye wapigaji ikupe mafao. Tuache kuitegemea serikali kwenye kila kitu.
 
Policcm na wenyewe kumbe wanapitia mapito ya aina hii baada ya kustaafu! Pole nyingi kwao.
Mgosi, Nchi hii hakuna Watu wenye maisha magumu Sana kama Polisi (both economically na socially maybe na mentally)
1. Economically: Wana kipato kidogo Sana chenye makato yasiyoeleweka na 75% ya Polisi ni vibarua Sio waajiriwa
2. Socially: wanaongoza kugongewa wake zao na Watoto wao, Yaani unakuta familia imekaa mgogoro
3: mentally: ndio kama huyu Mzee Swai

Ila sasa ukiwaona huku nje wanavyojifaragua na kujiona wa maana. Kumbe maisha yao yote wanatumika Tu na CCM
20241127_144855.jpg
 
Daah Nchi zetu za Afrika tuna roho mbaya sana yaani mtu kafanya kazi miaka yote hiyo harafu stahiki zake apewi kwa wakati na nyumba anafukuzwa yaani hii inawafanya watu wengi wawe wala rushwa wakubwa...
Halafu kastaafu na 56yrs, duh maisha haya. Amemaliza nguvu zake Huko, sasa hivi Hana hata kibanda cha kujihifadhi
 
Mzee John Samwel Swai(61) mstaafu wa Jeshi la Polisi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumsaidia asiondolewe katika kambi anayoishi kwani bado hajalipwa fedha za mizigo pamoja na fedha za likizo ambazo anapaswa kulipwa.

.Mzee huyo alistaafu mwaka 2020 baada ya kutumikia jeshi la polisi kuanzia mwaka 1983 amedai kupewa barua na Mkuu wa Kambi za Polisi inayomtaka kuhama ndani ya siku saba kuanzia Februari 04 mpaka leo Februari 10 na endapo asipohama vitu vyake vitatolewa nje.

Kupitia barua aliyopewa tarehe nne mwezi huu imesema “Umeariwa kukabidhi nyumba tajwa hapo juu, kwani umeshastaafu kazi toka 2020.

Oc Barracks amekuamuru kukabidhi nyumba tajwa hapo juu kwa kuwa umestaafu kazi. Umepewa siku 07 kuanzia leo tarehe 04/02/2025 hadi 10/02/2025 uwe tayari umekabidhi nyumba hiyo, Kushindwa kutekeleza amri hii, vitu vyako vitatolewa nje, hivyo unaamriwa kuviondoa mwenyewe kabla ya kutolewa”

Mzee Swai amewaomba wasaidizi wa Rais ambao Jeshi la Polisi lipo chini yao akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kumsaidia wakati huo serikali ikiendelea kushuhulikia malipo yao.

Jambo TV imefanya jitihda za kumtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime kwa njia ya simu lakini jitihada hazikuzaa matunda.
TII AMRI BILA SHURUTI... ONDOKA
 
Tuhuma za fedheha kama hizi zikifuatiliwa zinaweza kwenda na watu, sema nini, Serikali ya viongozi kula kwa urefu wa kamba zao, hakuna mtu atafanywa kitu.
Tatizo ni kuwa Hakuna mwenye uhalali (moral authority) wa kufuatilia na kuadhibu wakosaji kwa sababu wakubwa wenyewe wanayo mamlaka isiyo halali, maana wapo hapo walipo kupitia wizi wa kura
 
Back
Top Bottom