Askari Polisi 6, Maafisa wa TFS wawili na Walinzi Binafsi 11 watuhumiwa kujeruhi Bodaboda na kusababisha vifo vyao

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia na kuwahoji kwa kina askari wa Kampuni ya ulinzi PASCO LTD 11, Maafisa wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) wawili na askari Polisi 6.

Kushikiliwa kwa watu hao kunatokana na tuhuma za kujeruhiwa kwa watu wawili ambao baadae walipoteza maisha na suala hili uchunguzi wake tayari unaendelea kufanyika.

Tarehe 28 Agosti, 2023 Majira ya saa 8 (nane) usiku eneo la Kiluvya Ubungo, maafisa kutoka katika taasisi hizo wanadai wakati wa utekelezaji wa majukumu yao, lilitokea kundi la watu wanaokadiriwa kuwa 30 wakiwa na pikipiki zilizokuwa zimebeba magunia ya mkaa ambayo ni mazao ya misitu na walipofika eneo la ukaguzi na kuamriwa wasimame, walikaidi na kuanza kufanya fujo kubwa kwa kuwarushia mawe Maofisa wa maliasili na wenzao wakishinikiza pikipiki zilizo kuwa na mkaa kinyume na sheria ziachiwe.

Mafisa wa timu hiyo waliokuwa na silaha walianza kufyatua risasi kwa lengo la kuwatawanya na kujilinda. Hata hivyo ilibainika watu wawili walijeruhiwa katika purukushani hizo na walipoteza maisha baada ya kufikishwa Hospitali ya Mloganzila.

Katika tukio hilo Pikipiki 16 ambazo zilitelekezwa na watu hao na magunia ya mkaa vilipelekwa Mpingo House.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum linachunguza mazingira yote ya tukio hili kwa kushirikiana na mamlaka zingine za kisheria na halitasita kuwezesha kuchukuliwa kwa hatua zingine za kisheria kulingana na sheria za Nchi.

Watu waliokuwa kwenye kazi hiyo wako chini ya ulinzi na silaha zao zimepelekwa kwenye mamlaka za kiuchunguzi za silaha/bunduki Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Mloganzila kwa uchunguzi.
 
haya masuala yahusuyo maliasili inabidi yapatiwe ufumbuzi wa kudumu, vinginevyo tutaendelea kupoteza nguvu kazi kama taifa.
 
Hii ni kazi ya lawama kabisa mlinzi hana Amani mda wowote kinanuka kweli kaligraph majonzi
 
Yahitajika nguvu kubwa sana kulinda miti.

Mkaa uzuiwe kwa nguvu zote

Kuni zizuiwe kwa nguvu zote
 
Kwa hiyo waliamriwa wasimame wakakaidi,wakaanza kufanya fujo

Hiyo inaweza ikawachomoa

Ova
 
Askari wa Kampuni ya ulinzi 11, Maafisa wa Wakala wa Huduma za Misitu(TFS) wawili na Askari Polisi 6.
 
duuh! hii ni hatari..sassa walivyowapa hizo silaha walitaka wazitumie kuchana nywele
 
Hatimaye walipakodi wanauawa kwa silaha zilizonunuliwa kuwalinda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…