Askari Polisi wa Dar aliyetajwa na Rais Samia arejeshwe ili kudhibiti ujambazi ni nani?

Askari Polisi wa Dar aliyetajwa na Rais Samia arejeshwe ili kudhibiti ujambazi ni nani?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Wote tumesikia kutoka kwa Mh Rais alipokuwa anaongea na Wanaoitwa Wazee wa Dar es Salaam kuhusu kuongezeka kwa matukio ya ujambazi Jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake (maana Jiji ni Ilala tu) ambapo Mh Rais amemuagiza IGP kulishughulikia jambo hilo na kulikomesha haraka huku akiagiza yule askari aliyehamishwa ambaye ni mahiri kwenye kukomesha majambazi arejeshwe .

Ni askari yupi huyo aliyehamishwa na sasa anatakiwa kurejeshwa ili kudhibiti ujambazi? Ni nani alimhamisha na kwa sababu zipi?
 
Rais anataka kusema dawa ya ujambazi Dsm anayo huyo askari mmoja pekee? kwani yeye mafunzo yake aliyapatia wapi tofauti na hawa wengine?

Awe makini na hizi kauli zake, zitashusha ari ya kazi kwa hawa askari waliopo, vyema serikali yake itoe msaada unaohitajika mengine amuachie IGP ayamalize.
 
Rais anataka kusema dawa ya ujambazi Dsm anayo huyo askari mmoja pekee? kwani yeye mafunzo yake aliyapatia wapi tofauti na hawa wengine?

Awe makini na hizi kauli zake, zitashusha ari ya kazi kwa hawa waliopo, vyema serikali yake itoe msaada unaohitajika mengine amuachie IGP ayamalize.
Mmebakia kukosoa tu wasukuma. Mbona kauli za dikteta magufuli mlikuwa hamzikosoi,,mlikuwa mnajifanya"ooh, watu wamemnukuu vibaya Rais"**
 
Mambosasa ajiandae kwenda Lindi kisha Muroto a.k.a Mr. Misifa aje Dar.
FB_IMG_16113870153977100.jpg
 
Nchi inaelekea halijojo tangu jpm aondoke kila kitu kinakufa ,huyu anategemeq mtu mmoja akomeshe ujambawazi kwa eneo lenye watu zaid ya million 6
Mnajitahidi sana kumkwamisha Mama SSH na chokochoko zenu lakini hamtoweza kamwe.Mmebaki tu kulaumu hata pasipo na sababu.Tulieni dawa iwaingie..mwendazake ameshalala milele.
 
Back
Top Bottom