Askari Polisi wa kituo cha Oysterbay mbaroni kwa ujambazi

fangfangjt

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2008
Posts
571
Reaction score
139
Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limewatia mbaroni majambazi tisa wa kutumia silaha akiwemo askari polisi wa kituo cha polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaamu Bw. Suleimani Kova amesema majambazi hao wamekamatwa katika operesheni maalum ya jeshi hilo ambapo pia walifanikiwa kukamata sare za jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) zinazoaminika kutumika katika uhalifu pamoja na silaha na risasi.

Aidha kamanda kova ameeleza kukamata magari yanayosadikika kutumika katika uhalifu tofauti pamoja na yenye namba za usajili T865CEH aina ya Carina, na T967 AUG carina.

CHANZO: ITV
 
Mbona mapolisiccm wengi ni majambazi. Huo ujambazi ni kama "part time job" kwao kwa ajili ya kujiongezea kipato...
 
Halafu ndio hawa wanaoaminiwa na Mh. Pinda na kuamliwa watupige raia huku hao hao wanatuibia mali zetu ambazo wamefundishwa wazilinde.
 
atakuwa na akili kama yule alipiga picha na lema kule arusha tukampiga mnvua za ukwel jela. ukiwa chadema na akili zako zinavia
 
Mbona mapolisiccm wengi ni majambazi. Huo ujambazi ni kama "part time job" kwao kwa ajili ya kujiongezea kipato...

Duh! ila ni kweli, wengi wa hawa polisi wetu wanafanya part time job Kama hizo; ujambazi, wizi, madawa ya kulevya, nyara za taifa, ufisadi, rushwa, hongo, kubambikiza kesi, etc
 
halafu ndio hawa wanaoaminiwa na mh. Pinda na kuamliwa watupige raia huku hao hao wanatuibia mali zetu ambazo wamefundishwa wazilinde.

yani mkubwa nakwambia huyu pinda hiyo kauli cjui alitoaga wapi na kwa jeuri gani.....!
 
Duuh kweli kikulacho ki-nguoni mwako!ipo siku hawa wanaopewaga escot yapolice kupeleka pesa bank watajutia nafsi zao!
 
atakuwa na akili kama yule alipiga picha na lema kule arusha tukampiga mnvua za ukwel jela. ukiwa chadema na akili zako zinavia

Jamani haya ndiyo matusi yanayokatazwa. Kwa nini mtu akili zake zivie akiwa CDM? Honestly this is not fair. Nadhani huyu ndiye akili zake zimevia, whatever that means.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mizengo akiulizwa atasema ''wapige tu, waibe tu, tumechoka, liwalo na liwe"
 
Kwa hiyo kama mambo yataendelea kuwa hivi itafika mahali mtu ukimwona polisi ukimbie kwani hutakuwa na uhakika kama siyo polisi jambazi.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limewatia mbaroni majambazi tisa wa kutumia silaha akiwemo askari polisi wa kituo cha polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaamu Bw. Suleimani Kova amesema majambazi hao wamekamatwa katika operesheni maalum ya jeshi hilo ambapo pia walifanikiwa kukamata sare za jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) zinazoaminika kutumika katika uhalifu pamoja na silaha na risasi.

Aidha kamanda kova ameeleza kukamata magari yanayosadikika kutumika katika uhalifu tofauti pamoja na yenye namba za usajili T865CEH aina ya Carina, na T967 AUG carina.

CHANZO: ITV

Hivi wale policcm waliokamatwa na gunia 2 za bangi kule Moshi na wale waliokamatwa na meno ya tembo ishu iliishia wapi maana na hii itapita kama upepo kama ile nyingine. Hii ndio Tz bwana. Chukua Chako Mapema!
 
Duh! ila ni kweli, wengi wa hawa polisi wetu wanafanya part time job Kama hizo; ujambazi, wizi, madawa ya kulevya, nyara za taifa, ufisadi, rushwa, hongo, kubambikiza kesi, etc
mbona manes ,TRA bandari husemi acheni kuponda kazi za watu mbona a kwenu haziongelewi
 
Back
Top Bottom