Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupitia mtandao wa Polisi Wanawake wametembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha kwa lengo la kujionea vivutio vinavyopatikana katika hifadhi hiyo ambayo inapatikana ndani ya mkoa wa Arusha sambamba na kuhamasisha watu kutembelea vivutio hivyo kuelekea siku ya Wanawake duniani.
Aidha Askari hao wamebainisha kuwa wameona fahari kutembelea hifadhi hiyo yenye vivutio mbalimbali ambapo wametoa wito kwa Watu wengine kuwa na utaratibu wa kwenda kutembelea vivutio vilivyopo hapa Nchini kwani pamoja na kuona uzuri uliopo lakini pia watajifunza mambo mengi.