Askari Shahidi ashindwa kueleza maana ya Kahaba na Malaya katika Kesi ya Wanawake waliokamatwa Riverside wakidaiwa kujiuza

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Shahidi wa pili katika kesi ya ukahaba inayowakabili washtakiwa watano katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine Drive, ameileza mahakama hiyo kuwa waliwakamata washtakiwa hao kwa tuhuma za ukahaba kutokana na viashiria vya aina ya mavazi waliyokuwa wameyavaa na muda na mahali walikokutwa na polisi.

Hata hivyo, shahidi huyo ambaye ni askari kutoka Kituo cha Polisi Mburahati, WP Konstebo wa Polisi (PC), Tunusuru Malungula, alijikuta katika wakati mgumu alipotakiwa kueleza maana ya umalaya au ukahaba kutokana na viashiria hivyo alivyovitaja.

Ilikuwa ni wakati wa maswali ya dodoso aliyoulizwa na mawakili wa utetezi katika kesi hiyo, Peter Madeleka, Jebra Kambole na Maria Mushi, leo Alhamisi Juni 27, 2024, mpaka akasema kuwa hajui maana ya ukahaba.

Pia, amesema hajui kama kuna sheria inayobainisha sifa za mavazi yanayoashiria ukahaba wala inayoweka muda ambao mtu akikutwa barabarani anakuwa anajihusisha na ukahaba.

Shahidi huyo pia alitakiwa kueleza kama washtakiwa walikuwa wakiuza miili yao, wao walibaki na nini na wateja walioinunua wako wapi.

Washtakiwa katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mfawidhi Rachael Kasebele ni Mariam Yusufu Mkinde (25) mkazi wa Magomeni, Mwazani Nassoro (25) mkazi wa Kigogo, Mwanaidi Salum (25) mkazi wa Mabibo, Faudhia Hassan (35) mkazi wa Ubungo na Tatu Omary (40) mkazi wa Ubungo.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 17277/2024, washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka moja la kufanya vitendo vya aibu mbele ya hadhara kwa ajili ya kufanya umalaya, kinyume na kifungu cha 176 (a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, marejeo ya mwaka 2022.
 
Hahahaha Daah mkuu hivi hamuwezi kutuwekea kama kipindi kile cha mboye watu walikuwa wanafinywa maswali mpaka mikojo.
 
Swali fikirishi kama walikuwa wanauza mwili wamebaki na nini na walionunua wameondoka na nini hahaha 🤣
 
Hahaha wanunuzi wako wapi 😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom