Askari Shahidi ashindwa kueleza maana ya Kahaba na Malaya katika Kesi ya Wanawake waliokamatwa Riverside wakidaiwa kujiuza

Askari Shahidi ashindwa kueleza maana ya Kahaba na Malaya katika Kesi ya Wanawake waliokamatwa Riverside wakidaiwa kujiuza

Washtakiwa katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mfawidhi Rachael Kasebele ni Mariam Yusufu Mkinde (25) mkazi wa Magomeni, Mwazani Nassoro (25) mkazi wa Kigogo, Mwanaidi Salum (25) mkazi wa Mabibo, Faudhia Hassan (35) mkazi wa Ubungo na Tatu Omary (40) mkazi wa Ubungo.
adriz Mamlukii gammaparticles hahahaha mbavu zangu
 
Shahidi wa pili katika kesi ya ukahaba inayowakabili washtakiwa watano katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine Drive, ameileza mahakama hiyo kuwa waliwakamata washtakiwa hao kwa tuhuma za ukahaba kutokana na viashiria vya aina ya mavazi waliyokuwa wameyavaa na muda na mahali walikokutwa na polisi.

Hata hivyo, shahidi huyo ambaye ni askari kutoka Kituo cha Polisi Mburahati, WP Konstebo wa Polisi (PC), Tunusuru Malungula, alijikuta katika wakati mgumu alipotakiwa kueleza maana ya umalaya au ukahaba kutokana na viashiria hivyo alivyovitaja.

Ilikuwa ni wakati wa maswali ya dodoso aliyoulizwa na mawakili wa utetezi katika kesi hiyo, Peter Madeleka, Jebra Kambole na Maria Mushi, leo Alhamisi Juni 27, 2024, mpaka akasema kuwa hajui maana ya ukahaba.

Pia, amesema hajui kama kuna sheria inayobainisha sifa za mavazi yanayoashiria ukahaba wala inayoweka muda ambao mtu akikutwa barabarani anakuwa anajihusisha na ukahaba.

Shahidi huyo pia alitakiwa kueleza kama washtakiwa walikuwa wakiuza miili yao, wao walibaki na nini na wateja walioinunua wako wapi.

Washtakiwa katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mfawidhi Rachael Kasebele ni Mariam Yusufu Mkinde (25) mkazi wa Magomeni, Mwazani Nassoro (25) mkazi wa Kigogo, Mwanaidi Salum (25) mkazi wa Mabibo, Faudhia Hassan (35) mkazi wa Ubungo na Tatu Omary (40) mkazi wa Ubungo.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 17277/2024, washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka moja la kufanya vitendo vya aibu mbele ya hadhara kwa ajili ya kufanya umalaya, kinyume na kifungu cha 176 (a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, marejeo ya mwaka 2022.
Kesi hii jamani!
 
Hapo bado hajaulizwa Hawa ndo uliwakamata hizo nguo ndo za kikahaba?
 

Attachments

  • Screenshot_2024-06-29-11-02-14-662_com.google.android.youtube.jpg
    Screenshot_2024-06-29-11-02-14-662_com.google.android.youtube.jpg
    625.3 KB · Views: 6
Ujue kuthibitisha ukahaba ni ngumu sana yakija mambo ya sheria.
Kwa perepeche za mdomoni unaweza kuona ni rahisi tu. Ila kisheria kabisa kuthibitisha kwamba huyu anajiuza ni ngumu
Nakazia
 
Hapo Wabongo wanafuraha mnoo, ila wakimamatwa mashoga na kuachiwa wanabwataaa, ko mnadhani sheria inachagua eeeh?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom