The Lastdream
JF-Expert Member
- Jan 23, 2024
- 1,970
- 4,616
hahaha kwahyo madada poa si watu wanaouza mwili ila wanatoa huduma Mbona sasa wanatafsiri ni watu wanaouza miili? Na kama wanatoa huduma ya kingono ushahidi unao pia?😂😂Kiuhalisia akiuza mwili habaki na kitu,,,ishu ni kutoa huduma ya ngono
Wanadharirika huku na maswali huku aliyewatuma anazunguka na kiti ofisi... hana habari hata kama Maafisa utamu wanamdai B kadhaa.!!Shahidi huyo pia alitakiwa kueleza kama washtakiwa walikuwa wakiuza miili yao, wao walibaki na nini na wateja walioinunua wako wapi.
Alikuwa nuota mbili akaamua awe wakili kujitegemea alisomea sheria akaingia Geshini......alipojitambua ......mHivi Madereka alikuwa ni polisi?
#YNWA
🤣🤣🤣🤣daaah sasa mkuu wataionyesha vipi mahakama hiyo bidhaa?Na waionyeshe mahakama hiyo bidhaa waliyoinunua
yakule kivp mkuu?Mbona karibia wote majina yao niyakule upande wa pili..then sioni mchagga hapo.😂🙄
Uzururaji inaweza kuthibitishwa kisheria kwa jinsi waliyokamatwa? Mzururaji sifa zake ni zipi?mkuu wa wilaya alikurupuka maana hizo kesi mahakama wanazifunguaga za uzururaji , maana kusema wanauza miili kuthibitisha ni ngumu mno
adriz Mamlukii gammaparticles hahahaha mbavu zanguWashtakiwa katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mfawidhi Rachael Kasebele ni Mariam Yusufu Mkinde (25) mkazi wa Magomeni, Mwazani Nassoro (25) mkazi wa Kigogo, Mwanaidi Salum (25) mkazi wa Mabibo, Faudhia Hassan (35) mkazi wa Ubungo na Tatu Omary (40) mkazi wa Ubungo.
Kesi hii jamani!Shahidi wa pili katika kesi ya ukahaba inayowakabili washtakiwa watano katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine Drive, ameileza mahakama hiyo kuwa waliwakamata washtakiwa hao kwa tuhuma za ukahaba kutokana na viashiria vya aina ya mavazi waliyokuwa wameyavaa na muda na mahali walikokutwa na polisi.
Hata hivyo, shahidi huyo ambaye ni askari kutoka Kituo cha Polisi Mburahati, WP Konstebo wa Polisi (PC), Tunusuru Malungula, alijikuta katika wakati mgumu alipotakiwa kueleza maana ya umalaya au ukahaba kutokana na viashiria hivyo alivyovitaja.
Ilikuwa ni wakati wa maswali ya dodoso aliyoulizwa na mawakili wa utetezi katika kesi hiyo, Peter Madeleka, Jebra Kambole na Maria Mushi, leo Alhamisi Juni 27, 2024, mpaka akasema kuwa hajui maana ya ukahaba.
Pia, amesema hajui kama kuna sheria inayobainisha sifa za mavazi yanayoashiria ukahaba wala inayoweka muda ambao mtu akikutwa barabarani anakuwa anajihusisha na ukahaba.
Shahidi huyo pia alitakiwa kueleza kama washtakiwa walikuwa wakiuza miili yao, wao walibaki na nini na wateja walioinunua wako wapi.
Washtakiwa katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mfawidhi Rachael Kasebele ni Mariam Yusufu Mkinde (25) mkazi wa Magomeni, Mwazani Nassoro (25) mkazi wa Kigogo, Mwanaidi Salum (25) mkazi wa Mabibo, Faudhia Hassan (35) mkazi wa Ubungo na Tatu Omary (40) mkazi wa Ubungo.
Katika kesi hiyo ya jinai namba 17277/2024, washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka moja la kufanya vitendo vya aibu mbele ya hadhara kwa ajili ya kufanya umalaya, kinyume na kifungu cha 176 (a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, marejeo ya mwaka 2022.
Mtoto mbichi sana huyo.Mishangazi nayo inauza utamu
Ni wavivu wa kujielimisha tu.Ila polisi huwa vilaza Sana.
NakaziaUjue kuthibitisha ukahaba ni ngumu sana yakija mambo ya sheria.
Kwa perepeche za mdomoni unaweza kuona ni rahisi tu. Ila kisheria kabisa kuthibitisha kwamba huyu anajiuza ni ngumu