Askari Tanapa auawa kwa kuchomwa mshale wenye sumu

Askari Tanapa auawa kwa kuchomwa mshale wenye sumu

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Afisa uhifadhi wa wanyamapori daraja la kwanza wa hifadhi ya Taifa ya Serengeri, Deus Mwakajegele ameuawa kwa kuchomwa mshale na watu wasiojulikana alipokuwa akitekeleza majukumu yake.

Tukio hilo limetokea jana Jumamosi Januari 21, 2023 katika eneo la Nyanungu wilayani Tarime baada ya kuchomwa mshale wenye sumu kichwani na kufariki katika hospitali ya Seliani Arusha alipopelekwa kwa ajili ya matibabu.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa wiki ya sheria mjini Musoma leo Jumapili Januari 22, 2023, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee amesema kuwa tukio hilo limetokea katika eneo lililokuwa na mgogoro ambao ulikuwa umetolewa maamuzi na vyombo vya dola.

"Nimesikitika sana yaani wananchi wamefikia hatua ya kumchoma askari mshale wenye sumu akiwa anatekeleza majukumu yake, hii ni mbaya sana" amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Pengine alikwenda kuingilai anaga za waharamia majangili za pembe za ndovu
 
Back
Top Bottom