Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Heshima sana wanajamvi,
Uwanja wa ndege wa kimataifa (KIA) Kilimajaro International Airport ni lango la utalii Tanzania.Uwanja huu umekuwa ukipokea wageni wengi wanaokuja kutalii katika Hifadhi zetu zilizojaliwa kila aina ya vivutio.
Bahati mbaya yupo askari mmoja kijana Mwanaume anayevalia kiraia amekuwa kero na msumbufu wa kutosha.Askari huyu anavizia wasafiri wanapoingia uwanja lango la mwanzo kabisa ukipita unamkuta anakusubiri tayari kuanza kukusumbua.
Kwanza atakuuliza una kiasi gani cha dollar kama hajaridhika na majibu yako atakuingiza katika chumba na kuanza kukupekua pekua utafikiri labda umebeba unga.
Wasafiri tunajua sheria kama umechukua kiasi zaidi ya USD 10,000 utatakiwa declare TRA,shida unaulizwa mara tu unapokaguliwa na mashine mwanzoni.Utaratibu unatakiwa kuulizwa unapokwenda departure lounge au unapokuwa umeshapita immigration.
Tunaomba mamlaka husika kubadili utaratibu huu mbovu ambao unatoa mwanya wa rushwa na kuifanya safari nzima kujaa karaha.
Mkuu wa Polisi KIA ni vyema ukambadili askari huyu anayelalamikiwa na wasafari wengi kuchelewa kumwondoa kutaendelea kulipaka tope jeshi la Polisi kwasababu ya askari mmoja ambaye hatosheki na mshahara wake.
Kwa ufuatiliaji wa karibu tembelea ofisi za ATCL,Ethiopia Airline na mawakala wa mashirika mbali mbali ya ndege kote huko Askari wenu ni habari kubwa na mbaya.
Ngongo safarini Johannesburg.