Askari wa Suma JKT asiyejielewa!

Askari wa Suma JKT asiyejielewa!

Mivyumba

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2017
Posts
275
Reaction score
533
Jana kwenye mida ya Saa 21:30 hivi Usiku, nilikuwa Kituo cha Feri Ndani ya Daladala za Machinga Complex tukiwa na abiria wengine, tukisubiri gari lijae tuondoke.

Gari lilivyojaa, dereva alianza kuondoa gari Taratibu kuingia barabarani! Mara ghafla,akapanda huyu ASKARI wa SUMA JKT akiwa na pingu mikononi but alikuwa amevaa nguo za Kiraia, akaenda akamshika Dereva amtoe kwenye usukani amfunge pingu huku gari ikiwa barabarani!

Watu wakawa wamesimama wengine wanashuka,na wengine wanamzuia yule ASKARI! Akatokea baba Mmoja akamzuia yule ASKARI, then akamuomba Kitambulisho chake na baadae akaamuru gari liende polisi.

Kwa kufupisha Stori, ni kwamba tulifanikiwa kufika polisi na Taratibu zikaendelea then tukaondoka na wakaahidi kumlaza selo huyo ASKARI mwenzio,but ilionekana wanavunga tu sijui kumuogopa/ Lah.

NATAMANI KUJUA,je kuna Sheria zinazowakinga hawa SUMA JKT kufanya vile?

Je, hakuna Miongozo ya kikazi inayomuelekeza Utaratibu na namna ya kumkamata mshitakiwa??
Swali la Mwisho, kwani Majukumu ya Polisi na SUMA yanaingiliana hadi kuagizwa Yeye kumkamata mtuhumiwa?
 
Jana kwenye mida ya Saa 21:30 hivi Usiku,nilikuwa Kituo cha Feri Ndani ya Daladala za Machinga Complex tukiwa na abiria wengine,tukisubiri gari lijae tuondoke.
Gari lilivyojaa,dereva alianza kuondoa gari Taratibu kuingia barabarani! Mara ghafla,akapanda huyu ASKARI wa SUMA JKT akiwa na pingu mikononi but alikuwa amevaa nguo za Kiraia,akaenda akamshika Dereva amtoe kwenye usukani amfunge pingu huku gari ikiwa barabarani!!!
Watu wakawa wamesimama wengine wanashuka,na wengine wanamzuia yule ASKARI ! Akatokea baba Mmoja akamzuia yule ASKARI,then akamuomba Kitambulisho chake na baadae akaamuru gari liende polisi.
Kwa kufupisha Stori ,ni kwamba tulifanikiwa kufika polisi na Taratibu zikaendelea then tukaondoka na wakaahidi kumlaza selo huyo ASKARI mwenzio,but ilionekana wanavunga tu sijui kumuogopa/ Lah.

NATAMANI KUJUA,je kuna Sheria zinazowakinga hawa SUMA JKT kufanya vile??!
Je, hakuna Miongozo ya kikazi inayomuelekeza Utaratibu na namna ya kumkamata mshitakiwa??
Swali la Mwisho, kwani Majukumu ya Polisi na SUMA yanaingiliana hadi kuagizwa Yeye kumkamata mtuhumiwa???
Mwananchi yoyote au askari jeshi lolote anaruhusiwa kumkatama muharifu na kumpeleka polisi na jukumu la kudhibiti uharifu siyo jukumu la vyombo vya ulinzi pekee!! Ila ni jukumu la kila Mwananchi.
 
Mwananchi yoyote au askari jeshi lolote anaruhusiwa kumkatama muharifu na kumpeleka polisi na jukumu la kudhibiti uharifu siyo jukumu la vyombo vya ulinzi pekee!! Ila ni jukumu la kila Mwananchi.
Ndio Utaratibu ulivyo? Kumshusha akiwa anaendesha gari si ndio???
 
Nakupa jibu fupi. Hao traffic wame ondolewa barabarani sasa hii njia wameibuni wenyewe. Huyo Suma JKT ni chawa wa traffic hawawezi mlaza jela mfanyakazi wao.
 
Unanijua mimi nani? Enzi za dictor Magu hazikuwapo

Kwa sasa enzi za demokrasia zimerudi kwa nguvu.
 
Kuna theory na practically em njoo nikamate nipeleke polisi ..
 
Hakuna watu qanafiki Kama Sisi watanzania,uliwezaje kumuona kama anemuondoa dereva kwenye usukani wakati hujui Kwa nini alimkamata dereva
?
 
Unanijua mimi nani? Enzi za dictor Magu hazikuwapo

Kwa sasa enzi za demokrasia zimerudi kwa nguvu.
Kwanini zisirudi? Kwani Kuna ubaya Gani? Watu lazima wa jivunie elimu, mamlaka na pesa zao. Great Achievements must be openly revieled towards people to see so that there's bold self confidence to endure threat and self defense.

RRONDO
 
Mnawalea hao wajinga sana, siku kenge inaitwa sijui suma JKT au askari yeyote akinizingua nitamng'ata sikio niondoke nalo.

[emoji38][emoji38][emoji38]punguza hasira mkuu
 
Mkuu poleni kwa mkasa huo na hii ni matokeo ya kuishi in a shithole country, tunahitaji katiba mpya, ni police pekee ndio watakua na uwezo to arrest, sio fujo zinazofanyika wakati huu,citizens arrest ni kumzuia suspect ,taarifu police ili wake wafanye arrest, majeshi mengine yote hayataruhusiwa to arrest, immigrations ni kitengo cha law enforcement ndio watakua na uwezo wa to arrest suspected illegal immigrants.
 
Sheria zinazowapa NGUVU .CPA S.14 NA 16
Screenshot_20220807-075024.jpg
Screenshot_20220807-075009.jpg
 
Back
Top Bottom