Askari wa Tanzania wanaoshiriki Mkutano Nchini Marekani wajengewa uwezo katika upigaji wa shabaha

Askari wa Tanzania wanaoshiriki Mkutano Nchini Marekani wajengewa uwezo katika upigaji wa shabaha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2024-09-05 at 05.57.04_372bf14b.jpg

WhatsApp Image 2024-09-05 at 05.57.08_76ca9dae.jpg

Katika kuhakikisha askari wa Kike wanakuwa imara na mahiri katika kila nyanja wanazohudum Suala la kujengewa umahiri katika ulengaji wa Shaba kwa askari hao likatolewa na wabobezi wa shabaha (Sniper) kutoka Jeshi la Polisi Nchini Marekani.

Miongoni mwa askari wa kike waliopata mafunzo ya ukupigaji shabaha nchini humo ni Koplo wa Jeshi la Polisi Kutoka Nchini Tanzania CPL Salome Masanyiwa ambaye amepata fursa hiyo amebainisha kuwa mafunzo hayo yamemjenga na kumuongezea umahiri katika upigaji wa shabaha tofauti na kipindi cha Nyuma.
WhatsApp Image 2024-09-05 at 05.57.09_a3aa9bd2.jpg

WhatsApp Image 2024-09-05 at 05.57.07_953c02b4.jpg
Aidha CPL Salome amesisitiza kuwa mafunzo hayo yamemuongezea utaalam katika matumizi ya silaha na ulengaji wa shabaha huku akiweka wazi kuwa anakwenda kupeleka ujuzi huo alioupata kwa askari wengine kutoka nchini Tanzania ambao hawakupata fursa ya mafunzo hayo.
 
Ila wazungu tech wako juu sana
Sisi huku kulenga lazima uende porini
Afande kanyoa kihuni na bado kulenga shida anaendekeza usela kuaibisha taifa
Huyo FBI yuko very strong lakini muonekano wa kike kabisa
 
Huyo afande wetu alipitia mafunzo pale moshi!? Kulenga shabaha alivukaje, au ndio nafasi za kupeana!?
Kwa jinsi alivyoshika bunduki anaonesha hata ile basic tuya kushika bunduki hana
 
Ila wazungu tech wako juu sana
Sisi huku kulenga lazima uende porini
Afande kanyoa kihuni na bado kulenga shida anaendekeza usela kuaibisha taifa
Huyo FBI yuko very strong lakini muonekano wa kike kabisa
Umesahau kunyoa denge la polisi!? 😛 😛
 
Kudadeki afande kapeleka vi kaunda suti Marekani wanavotunyanyasiaga navyo mtaani bongo
 
Sio afande hata kufagia uwani hawezi
Kweli afande au yupo ofisini tu
Kashindwa hata kufuatisha anavyofanya mwenzake?
 
Huyo aliyevaa koti jeusi walimuokota soko gani mbona ni kama muuza vitumbua hiyo silaha mara yake ya kwanza kushika?

Juzijuzi Waziri wa ulinzi hawezi tumia binoculars, miezi kadhaa nyuma askari jeshi ameshiriki ubakaji na kujirekodi, leo huyu anashika silaha kwa kukunja uso kama yuko msalani. Alivyoshika kama chupa ya sumu vile. Kwenye suala la ulinzi tuko weupe ni amani tu inatubeba
 
Katika kuhakikisha askari wa Kike wanakuwa imara na mahiri katika kila nyanja wanazohudum Suala la kujengewa umahiri katika ulengaji wa Shaba kwa askari hao likatolewa na wabobezi wa shabaha (Sniper) kutoka Jeshi la Polisi Nchini Marekani.

Miongoni mwa askari wa kike waliopata mafunzo ya ukupigaji shabaha nchini humo ni Koplo wa Jeshi la Polisi Kutoka Nchini Tanzania CPL Salome Masanyiwa ambaye amepata fursa hiyo amebainisha kuwa mafunzo hayo yamemjenga na kumuongezea umahiri katika upigaji wa shabaha tofauti na kipindi cha Nyuma.
Aidha CPL Salome amesisitiza kuwa mafunzo hayo yamemuongezea utaalam katika matumizi ya silaha na ulengaji wa shabaha huku akiweka wazi kuwa anakwenda kupeleka ujuzi huo alioupata kwa askari wengine kutoka nchini Tanzania ambao hawakupata fursa ya mafunzo hayo.
Mafunzo Kama haya ya kulenga shabaha nafikiri ingekuwa Bora zaidi kwa wa-Tanzania wangepelekwa Askari wa kutoka kwenye Majeshi mengine yaliyopo hapa Tanzania kama vile JWTZ/TPDF, lakini siyo kuwapeleka Askari kutoka katika Jeshi la Polisi kwa sababu matokeo au matunda ya Mafunzo hayo itakuwa ni kuwaongezea machungu ya misiba zaidi kwa Raia wema wasio na hatia ambao kwa miaka ya hivi karibuni wamekuwa wahanga wakubwa Sana wa kufanyiwa vitendo viovu vya kikatili kutoka kwa Askari Polisi. Mafunzo hayo badala ya kuja kuwa neema kwa Wananchi wa Tanzania matokeo yake yatakuwa ni mabaya zaidi kwani yanaweza yakaja kutumika vibaya katika kuvunja haki za msingi kabisa za binadamu ( Kama vile kuhujumu haki za kuishi) kwa Raia wema wasio na hatia, kwani uzoefu ni Mwalimu mzuri zaidi.
 
Back
Top Bottom