Askari wa Uhifadhi TANAPA afariki kwa kugongwa na Nyati katika Hifadhi ya Taifa Mkomazi

Askari wa Uhifadhi TANAPA afariki kwa kugongwa na Nyati katika Hifadhi ya Taifa Mkomazi

 
Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), William Mwakilema amesema kifo cha Askari huyo wa Uhifadhi Daraja la Tatu, Samwel Edward Nassari kimetokea Agosti Mosi, 2023 eneo la Mbula katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi wakati akitekeleza majukumu yake ya ulinzi

Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi inapatikana katika mikoa ya Kilimanjaro na Tanga ndani ya Wilaya za Same na Lushoto, ilianzishwa kama Pori la Akiba lililomegwa kutoka katika Pori kubwa la Akiba la Ruvu kabla ya kubadilishwa kuwa Hifadhi ya Taifa, ina ukubwa wa Kilomita za Mraba 3,245


Hapo kwenye KUGONGWA na nyati ndiyo inaleta shida. R.I.P
 
Back
Top Bottom