Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Tangu juzi Rais Zelensky amesikika akisema hali kwenye mji aliosema hautowaponyoka hata siku moja kuwa ni mbaya na inadorora kwa upande wao kila saa.
Pamoja na malalamiko hayo lakini alikuwa akiwasifu sana askari wake kwa ushujaa wao kuendelea kushikilia sehemu walipo.
Leo inaonekana hali imezidi kuwa mbaya kwani askari wenyewe wamesema mambo yalivyo huko ni kama Jehanamu.
Vikosi vya Wagner wamepeleka mstari wa mbele askari wao wenye mafunzo ya hali ya juu ambao wanaharibu kila walichonacho kinachoweza kuwasaidia kupigana.
Dalili zinaonesha muda wowote kuanzia sasa watatangaza kuuwacha mji huo mikononi mwa Urusi kama walivyofanya kwa Soledar na kwengineko.
Mjio utakaofuata katika mpangilio wa Urusi huenda itakuwa ni Kharkiv.