Askari wa usalama barabarani fuatilieni usalama wa abiria Noah za Mbinga - Litembo?

Hakuna anayejali

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2023
Posts
418
Reaction score
526
Habari wanajukwaa.

Leo nilikuwa nasafiri nilipofika stend nimeikuta Noah inapakia abiria. Ajabu ticket ina maelezo ya gari nyingine, lakini yenyewe plate namba nyingine.

Tumetoka pale tupo 8 na ilipotoka stend ikapakia tena wawili kwenye buti, wengine wakasimama ndani na mwingine mbele kwa dereva manake mbele abiria wa3 nje na dereva, jumla ya abiria 15 na mizigo juu hadi roof inagonga. Nikawambia ni hatari kwa watu na mali yao.

Usalama barabarani fuatilieni hili gari isijaze kuliko uwezo Mbinga via Litembo. Askari msijali maokoto tu.

 
Noah boda bajajiji ni miladi ya polisi usalama barabarani pesa wanayo kusanya hawa jamaa niyingi kuliko inayo ingia serikalini
 
Shukrani sana kinga ni bora
 
Nunua coaster mpya wapelekee huenda ikasaidia kupunguza adha.
 
Ndugu yangu cha kushukuru mungu umefika salama basi.hayo mengine mungu anajua
 
Abiria 15 mbona wachache kwa Noah nenda Mahenge To Mwaya hadi 20 mnakaa kwa kupakatana.
Ndio usafir wa vijijini ulivyo.
Ikitokea imetokea hakuna waandishi wa habari huko
 
Nunua coaster mpya wapelekee huenda ikasaidia kupunguza adha.
Coaster utakesha na abiria upati kwani matajiri hawàoni Hilo labda uziblock Noah zote.
Sehem nyingi tu coaster zinachemka Noa chapu inajaa inaondoka
 
Umenikumbusha enzi ya defender 110 hatari sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…