Askari wa usalama barabarani Mafinga ni kero

Askari wa usalama barabarani Mafinga ni kero

Franky

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2012
Posts
2,270
Reaction score
2,844
Wasalaam,

Siku mbili izi kuna video ya Waziri wa mambo ya ndani ya nchi akiongea na viongozi wa vyombo vya usalama imeonekana kwenye mitandao ya kijamii.

Waziri huyo alionekana akiwalalamikia sana traffic kwa kufanya kazi bila kuzingatia sheria, utu pia kufanya overcrowding barabarani, unakuta traffic kila baada ya km 0.5 wamepaki gari zao wanakomaa kweli kweli kubargain na madereva.

Waziri aliwakemea wazi wazi akiwaweka wazi je wanataka nayeye awe kiongozi wa matamko kama wengine na kuwaambia ebu watupumzishe wasafiri kipindi hiki tukielekea kwenye balot boxes lasivo wanataka wakose kura maana wasafiri na madereva wao ndo mtaji wao.

Sasa hawa traffic wa Mafinga, Iringa ni kwamba wamepangiwa wengi sana halmashauri hii? Wanajitoa ufahamu? Wana kiburi? Hawaheshimu chain of command? Au wana njaa sanaa? Jamani eeeh ebu tupumzisheni basi kidogo corona imekula ela zetu zote wakati tupo karantin na nyie mnataka kutusumbua.

Au waziri katuzuga kimtindo kama alivokuwa yule kibakuri mtangulizi wakeee?
 
Halafu ukute unaamua kwa shingo upande kupunguza usumbufu na hivyo kumtoa buku 2 ya kununulia brush, unakuta anakomaa uongeze kama vile mlisaidiana kutafuta! Ila hawa jamaa wanaoitwa Polisi, wanapenda rushwa aisee!

Wachache sana ni waungwana.
 
Jamaa hawa sijui wakoje asee, eti mbona kaela kadogo bumbavu we unako?
 
Inabidi unajiandaa na buku mbili mbili unaomba chenji petrol station wakati unajaza mafuta, buku 10 parefu kwa traffic mmoja wakikupiga tochi 10 unaacha laki.
 
Last week nimetoka mbeya nimepigwa tochi maporini kwa kuviziwa, nakuja kusimamishwa mbele kabisa..
Alaf nampa elf 5 anakataa shenz kabisa yule jamaa..
Si akakwapua elf 10 kwenye wallet nikabaki nacheka tu [emoji38]
Naomba yule mwenye tochi anayejifichaga mbuga za Wanyama Mikumi karibu na Doma ''ALIWE NA SIMBA''.

Amiina
 
Katika mara mbili za mwisho nilizosimamishwa zote ilikua uonevu mtupu
1)nikitokea jijini dar njiani kuitafuta mlandizi baada ya mstari kuniruhusu Mimi upande wangu ku overtake nikalipita semi lililokua na escort mbele na nyuma kumbe jamaa kajificha kuleeee mbele.. Akanisimamisha na akalazimisha kuniandikia hata baada ya kumuonyesha 5000/=Naona aliona ndogo. Roho iliniuma sana kuonewa!
2)Kibaigwa nashusha ile down kuelekea pale Centre kumbe sijui pale huwa pana zebra hapo mbele askari dogo fulani akanionyesha kuwa nimepita juu ya zebra kwa 61km/h hivyo natakiwa nilipie serikali 30.000/=nikamwambia dogo na corona yote hii? Nashukuru huyu alinijeruhi kidogo japo napo niliumia maana sasa tunashindwa kudrive kwa uhuru highway
 
Kuna Wale wadada wawili pale eneo la ranchi barabara ya Moro Dom ila wao hawana madhara wanaangalia madeni tu
Naomba yule mwenye tochi anayejifichaga mbuga za Wanyama Mikumi karibu na Doma ''ALIWE NA SIMBA''.

Amiina
 
hawa wa mafinga wamezidi kuna jamaa anaitwa beruto huyu hata kwenye baa kama hununui unategemea kugongea watu wanakuita kuwa jamaa amekuja kutuberuto ikiwa na maana kaja kugongea kupiga tochi
 
hawa wa mafinga wamezidi kuna jamaa anaitwa beruto huyu hata kwenye baa kama hununui unategemea kugongea watu wanakuita kuwa jamaa amekuja kutuberuto ikiwa na maana kaja kugongea kupiga tochi
Hahaha beruto ni noma
 
Watakosaje sasa afu traffic wote wana magari aisee ila Police wa kawaida hawana magari wengi wao.

Mkuu kama wana vitambi siku zao zinahesabika maana amri imeshamfikia mura!
 
hawa wa mafinga wamezidi kuna jamaa anaitwa beruto huyu hata kwenye baa kama hununui unategemea kugongea watu wanakuita kuwa jamaa amekuja kutuberuto ikiwa na maana kaja kugongea kupiga tochi
Beruto namfahamu huyoo
 
Back
Top Bottom