Askari waonywa kutotumia lugha za kifedhuli, waambiwa rushwa ni chanzo cha ajali

Askari waonywa kutotumia lugha za kifedhuli, waambiwa rushwa ni chanzo cha ajali

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Kamishna wa Polisi Zanzibar, CP Awadhi Juma Haji ametoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi kufanya oparesheni za kukamata madereva wote ambao wataendesha abiria bila kuvaa kofia ngumu katika pikipiki, kuendesha kwa mwendo kasi, kuendesha gari bila leseni na makosa ya kuegesha magari hovyo.

Amesisitiza kuwa ametoa maelekezo ya askari kutoa huduma bora kwa wananchi wanapokuwa barabarani.

“Hata kama ni dereva amefanya makosa lazima ashughulikiwe kwa lugha nzuri, zisitumike lugha mbaya za kifedhuli.

“Jambo lingine ni suala la rushwa, uwepo wa rushwa wakati mwingine ni chanzo cha kuchochea ajali, tumekemea, askari watimize wajibu wao wa kutojihusisha na vitendo hivyo,

“Askari wachukue hatua dhidi ya wale wanaowashawishi kutaka kuwapa rushwa, hatua kali sana zichukuliwe dhidi yao, Jeshi la Polisi hatuwezi kuvumilia wale wanaofanya makosa kisha wanakuwa chanzo cha ajali,” amesema CP Awadhi Juma Haji.


Source: Wasafi Digital
 
Back
Top Bottom