Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Kama kawa, kila nipatapo fursa, huja na makala elimishi za kwa maslahi ya taifa, ambazo huwa na maswali, hoja, majibu utaweka mwenyewe, swali la leo ni kujiuliza kwa sauti, asking aloud: "Je Rais Samia anajua kuwa Katiba yetu ina ubatili fulani, uliochomekewa kiubatili hivyo kuifanya Tanzania kuwa na katiba Batilifu?. Je anajua kuwa hii sheria mpya ya uchaguzi aliyosaini hapa juzi kati ni sheria batili inayokwenda kinyume cha Katiba ya JMT ya Mwaka 1977?. Je, anajua ubatili huu unadhulumu haki ya Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa?. Je anajua kila dhulma ya haki, huwa ina consequences?
Kwanza naomba mnisamehe kwa kuandika mabandiko marefu, sometimes nakuwa too emotional, hivyo nondo zina tiririka tuu na ku flows.
Hili shurti la wanasiasa kudhaminiwa na chama cha siasa, ili kugombea uongozi ni shurti batili liko kinyume na katiba ya JMT ya mwaka 1977, na limechomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu. Shurti la Mgombea Kudhaminiwa na Chama cha Siasa ni Shurti Batili, Lililochomekewa Kiubatili Ndani ya Katiba Yetu. Kwanini Tunalikumbatia?
Mahakama Kuu iliishalifutaSerikali, Bunge, Ziheshimu Mahakama! Kwanini Serikali na Bunge Hazijatekeleza Hukumu ya Mahakama kuhusu Ubatili wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi?
Kufuatia ubatili huu, unamaanisha katiba yetu ni katiba batilifu, ina ubatili, na sheria mpya ya uchaguzi ni sheria batili!. Serikali yetu tukufu imetunga muswada wenye kipengele batili, Bunge letu likatunga Sheria batili, na Rais akaisaini hiyo sheria batili kuanza kutumika bila yeye Rais kujua kuwa amesainishwa sheria batili!.
Swali ni Je Rais Rais Samia, anajua kuwa hii sheria mpya ya uchaguzi aliyoisaini juzi juzi, kwa jicho la kisheria ni sheria batili?
Japo Rais wa Tanzania, ana kinga ya kikatiba ya kutokushitakiwa kwa makosa yoyote atakayotenda akiwa madarakani katika utekelezaji wa majukumu yake ya urais, ila ibara ya 56A imesema specific kuwa kinga hiyo ya rais kutokushitakiwa, inahusu makosa mengine yote, ila haihusu Rais anapovunja katiba ya JMT, anashitakiwa kwa mujibu wa ibara ya 56A.
The only excuse ya rais kusaini sheria batili kuanza kutumika, ni kwa vile Rais wetu sio mwanasheria, hivyo hategemewi kuujua ubatili wa Katiba, ila kwa vile anawasaidizi wake sheria, wakiongozwa na Waziri wa sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hawa ni manguli wa sheria, wabobezi na wabobevu ambao wanaujua kabisa ubatili wa sheria hiyo, na ubatili wa Katiba, lakini hawajamweleza Rais Samia kuhusu ubatili huu kwa excuse kuwa ubatili huu umefanywa na awamu zilizotangulia, Rais Samia kaingia kaukuta, hivyo wakamtungia tuu sheria batili kwasababu sheria ikiyokuwepo nayo ni batili lakini ilikuwa inatumika!
Kuna kanuni ya the doctrine of separation of powers between mihimili inayokwenda na kitu kinachoitwa checks and balance inayoitaka kila mhimili kuwa kiranja wa mhimili mwenzake usikiuke mamlaka yake wala usikiuke katiba.
Ibara ya 64 (5) ya Katiba imetamka wazi kuwa katiba ndio sheria mama, sheria nyingine yoyote itakayo kinzana na katiba, sheria hiyo itakuwa ni batili. Ijue Katiba kwa Jicho la Mtunga Katiba: Mtunga Katiba alimaanisha nini aliposema "Katiba ni Sheria Mama"? Ni kweli Katiba ni Sheria Mama? sheria batili sio Mahakama, ni katiba yenyewe, jukumu la Mahakama ni kuithibisha tuu huo ubatili na kutangaza kuwa ni batili, tangu siku Mahakama Kuu ya Tanzania ilipouthitisha ubatili huu na kuutangaza, kuanzia hapo ubatili huo unakuwa umeisha batilishika there and then!
Licha ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuutangaza ubatili huu na kuubatilisha, lakini Serikali ya awamu ya Sita, bado imetunga muswada wa sheria wenye ubatili ule ule, na Bunge letu, likaupokea muswada huo batili na kuutungia sheria kitutusa, hali iliyowafanya wabunge wetu makini kugeuka kama mazuzu vile, checks and balance inatoka wapi?
Bunge letu chini mwalimu wangu, mwanasheria mbobezi na mbobevu, Dr. Tulia Akson, alipaswa kulitumia Bunge to i check Serikali kuwa haiwezi kututungia muswada batili, na Bunge lina mamlaka ya kuuondoa ubatili huo na kutunga sheria safi isiyo na ubatili, lakini Bunge letu, likatunga Sheria Batili kitutusa na kumpelekea Rais Samia kuisaini!. Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?
Kwavile Rais Samia anawaamini sana wasaidizi wake, wamemtungia muswada batili na Bunge likitunga Sheria batili, Rais Samia yeye amesaini with very clear conscious kuwa anasaini sheria halali bila wasaidizi wake kumweleza kuwa sheria hiyo ni batili, hivyo kwenye hili la ubatili wa sheria mpya ya uchaguzi, Rais Samia hana kosa kabisa, wenye makosa ni Serikali kutunga muswada batili na Bunge kutunga sheria batili!.
- Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?
Hili la huu ubatili, nimelipigia sana kelele kwenye all fronts,
live, social media na mainstream media. nimepandisha threads zaidi ya 50 !
Je inawezekana ni Anasikia kabisa kilio hiki, ila Wahafidhina wa Chama Chake Ndio Hawataki, Katiba ni Sheria Mama. Sheria Yoyote Kinyume na Katiba ni Batili. Wanasheria Wetu, Waliwezaje Kufanya Madudu Haya Kuchomeka Batili Ndani ya Katiba?
Swali la kujiuliza ni baada ya kelele zote hizi kuhusu ubatili wa Katiba yetu na ubatili wa sheria zetu, jee Rais Samia amezisikia?.
Naona maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa sheria batili yanaendelea, na mwakani tunakwenda kwenye uchaguzi mkuu na katiba batili na sheria batili!.
Kwa vile Mungu ni haki, no one knows for sure kwanini yule aliitwa na kuondoshwa mapema, usikute na hii dhulma ya haki za Watanzania, zimechangia, naendelea kusisitiza Mama yetu, if there is anything she can do to help out Watanzania kurejeshewa haki zao, Please do, utabarikiwa, tutabarikiwa na Tanzania itabarikiwa!.
Naamini kabisa kuna siku iso jina, kilio hiki cha haki kitasikika!.
Conclusion.
Namalizia kwa swali la msingi la bandiko hili. Jee Rais Samia anajua kuwa Katiba yetu ina ubatili fulani, uliochomekewa kiubatili hivyo kuifanya Tanzania kuwa na katiba Batili?. Je anajua kuwa hii sheria mpya ya uchaguzi aliyosaini hapa juzi kati ni sheria batili inayokwenda kinyume cha Katiba ya JMT ya Mwaka 1977?. Jee anajua ubatili huu unadhulmu haki ya Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa?. Jee anajua kila dhulma ya haki, huwa ina consequences?.
Jee Rais Samia Afanye Nini?.
Mungu Mbariki Rais Samia, jicho ona lake liione hii dhulma kubwa ya haki ya Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa airejeshe.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali

- Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi. Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!
- Ombi kwa Rais Samia: Sheria Mpya ya Uchaguzi Bado ina Ubatili. Haki ya Kuchagua na Kuchaguliwa imeporwa! Irejeshwe kwa Mujibu wa Katiba!
- Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.
- Je, wajua Muswada Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2023 ni batili? Ni mvinyo wa zamani, kwenye chupa mpya? Why ubatili huu?
- Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa?
- Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa! Sheria ya Uchaguzi ni kosa. Kwanini tunarudia kosa? Haki si hisani, ni stahiki. Bunge tutendeeni haki!
- Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?
Hili la huu ubatili, nimelipigia sana kelele kwenye all fronts,
live, social media na mainstream media. nimepandisha threads zaidi ya 50 !
Je inawezekana ni Anasikia kabisa kilio hiki, ila Wahafidhina wa Chama Chake Ndio Hawataki, Katiba ni Sheria Mama. Sheria Yoyote Kinyume na Katiba ni Batili. Wanasheria Wetu, Waliwezaje Kufanya Madudu Haya Kuchomeka Batili Ndani ya Katiba?
- Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
- Shurti la Mgombea Kudhaminiwa na Chama cha Siasa ni Shurti Batili, Lililochomekewa Kiubatili Ndani ya Katiba Yetu. Kwanini Tunalikumbatia?
- Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
- Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?
- Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi. Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!
- Haki, Haki, Haki! Serikali, Bunge na Mahakama hazina uwezo wala mamlaka ya kupora haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Je, jicho ona litaliona hili?
- Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?