Asking Aloud: Rais Samia anajua Katiba yetu ni batilifu, na Sheria mpya ya uchaguzi aliyosaini ni sheria batili kinyume cha katiba?

Mayala

nakukumbusha tu,TANZANIA ni kisiwa katika suala la sheria au katibakwanza kabisa ukiongelea sura ya mwanzo ya katiba kuhusu kuitambua serikali ya muungano hilo jambo ni batili sababu kinachoungana kinakuwa na mkataba,mkataba sharti uwe na ukomo.

ukizungumzia uhuru wa kupiga na kupigiwa kura ni batili,tTanzania haina private candidate.

Majukumu na haki ya za rais ni over power,Rais amegewa ardhi ya TANZANIA anweza kumuhamisha yeyote.

sheria zina contradictions kibao.
 
Yawezekana ikawa kweli au si kweli.
Kwa mfano ni kweli...
1."Nini kifanyike,lakini pia akikubali kubadilisha tusogeze uchaguzi Mkuu mbele ili mchakato wake ufanyiwe review na wadau?
2."Kwanini wasomi na wadau wamemchomekea Mh.Rais contents kinyume na Katiba,ajenda yao ni nini hasa"?
 
Wanabodi
Kama kawa, kila nipatapo fursa, huja na makala elimishi za kwa maslahi ya taifa, ambazo huwa na maswali, hoja, majibu utaweka mwenyewe, swali la leo ni Asking Aloud: "Jee Rais Samia anajua kuwa Katiba yetu ina ubatili fulani, uliochomekewa kiubatili hivyo kuifanya Tanzania kuwa na katiba Batili?. Je anajua kuwa hii sheria mpya ya uchaguzi aliyosaini hapa juzi kati ni sheria batili inayokwenda kinyume cha Katiba ya JMT ya Mwaka 1977?. Jee anajua ubatili huu unadhulmu haki ya Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa?. Jee anajua kila dhulma ya haki, huwa ina consequences?.

Kwanza naomba mnisamehe kwa kuandika mabandiko marefu, sometimes nakuwa too emotional, hivyo nondo zina tiririka tuu na ku flows.

Hili shurti la wanasiasa kudhaminiwa na chama cha siasa, ili kugombea uongozi ni shurti batili liko kinyume na katiba ya JMT ya mwaka 1977, na limechomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu.

Kufuatia ubatili huu, unamaanisha katiba yetu ina ubatili, na sheria mpya ya uchaguzi ni sheria batili, Serikali imetunga muswada batili, Bunge letu likatunga Sheria Batili, na Rais akaisaini hiyo Sheria batili kuanza kutumika.

Swali ni Je Rais Rais Samia, anajua kuwa hii sheria mpya ya uchaguzi aliyoisaini juzi juzi, kwa jicho la kisheria ni sheria batili?.

Japo Rais wa Tanzania, ana kinga ya kikatiba ya kutokushitakiwa kwa makosa yoyote atakayotenda akiwa madarakani katika utekelezaji wa majukumu yake ya urais, ila ibara ya 56A imesema specific kuwa kinga hiyo ya rais kutokushitakiwa, inahusu makosa mengine yote, ila haihusu Rais anapovunja katiba ya JMT, anashitakiwa kwa mujibu wa ibara ya 56A.

The only excuse ya rais kusaini sheria batili kuanza kutumika, ni kwa vile Rais wetu sio mwanasheria, hivyo hategemewi kuujua ubatili wa Katiba, ila kwa vile anawasaidizi wake sheria, wakiongozwa na Waziri wa sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hawa ni manguli wa sheria, wabobezi na wabobevu ambao wanaujua kabisa ubatili wa sheria hiyo, na ubatili wa Katiba, lakini hawajamweleza Rais Samia kuhusu ubatili huu kwa excuse kuwa ubatili huu umefanywa na awamu zilizotangulia, Rais Samia kaingia kaukuta, hivyo wakamtungia tuu sheria batili kwasababu sheria ikiyokuwepo nayo ni batili lakini ilikuwa inatumika!.

Kuna kanuni ya the doctrine of separation of powers between mihimili inayokwenda na kitu kinachoitwa checks and balance inayoitaka kila mhimili kuwa kiranja wa mhimili mwenzake usikiuke mamlaka yake wala usikiuke katiba.

Ibara ya 64 (5) ya Katiba imetamka wazi kuwa katiba ndio sheria mama, sheria nyingine yoyote itakayo kinzana na katiba, sheria hiyo itakuwa ni batili. Ijue Katiba kwa Jicho la Mtunga Katiba: Mtunga Katiba alimaanisha nini aliposema "Katiba ni Sheria Mama"? Ni kweli Katiba ni Sheria Mama? sheria batili sio Mahakama, ni katiba yenyewe, jukumu la Mahakama ni kuithibisha tuu huo ubatili na kutangaza kuwa ni batili, tangu siku Mahakama Kuu ya Tanzania ilipouthitisha ubatili huu na kuutangaza, kuanzia hapo ubatili huo unakuwa umeisha batilishika there and then!.

Licha ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuutangaza ubatili huu na kuubatilisha, lakini Serikali ya awamu ya Sita, bado imetunga muswada wa sheria wenye ubatili ule ule, na Bunge letu, likaupokea muswada huo batili na kuutungia sheria kitutusa, hali iliyowafanya wabunge wetu makini kugeuka kama mazuzu vile, checks and balance inatoka wapi?!.

Bunge letu chini mwalimu wangu, mwanasheria mbobezi na mbobevu, Dr. Tulia Akson, alipaswa kulitumia Bunge to i check Serikali kuwa haiwezi kututungia muswada batili, na Bunge lina mamlaka ya kuuondoa ubatili huo na kutunga sheria safi isiyo na ubatili, lakini Bunge letu, likatunga Sheria Batili kitutusa na kumpelekea Rais Samia kuisaini!.

Kwavile Rais Samia anawaamini sana wasaidizi wake, wamemtungia muswada batili na Bunge likitunga Sheria batili, Rais Samia yeye amesaini with very clear conscious kuwa anasaini sheria halali bila wasaidizi wake kumweleza kuwa sheria hiyo ni batili, hivyo kwenye hili la ubatili wa sheria mpya ya uchaguzi, Rais Samia hana kosa kabisa, wenye makosa ni Serikali kutunga muswada batili na Bunge kutunga sheria batili!.
-https://www.jamiiforums.com/threads/tuombe-mwaka-2024-uwe-ni-mwaka-wa-mageuzi-ya-kweli-ya-kidemokrasia-ya-kweli-tanzania-tume-huru-uchaguzi-huru-na-wa-haki-happy-new-year.2172208/
- Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?

Hili la huu ubatili, nimelipigia sana kelele kwenye all fronts,
live, social media na mainstream media. nimepandisha threads zaidi ya 50 !

Je inawezekana ni Anasikia kabisa kilio hiki, ila Wahafidhina wa Chama Chake Ndio Hawataki,

Sikuishia kuandika tuu, pia nimezungumza mara 3 kwenye mikutano

Swali la kujiuliza ni baada ya kelele zote hizi kuhusu ubatili wa Katiba yetu na ubatili wa sheria zetu, jee Rais Samia amezisikia?.

Naona maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa sheria batili yanaendelea, na mwakani tunakwenda kwenye uchaguzi mkuu na katiba batili na sheria batili!.

Kwa vile Mungu ni haki, no one knows for sure kwanini yule aliitwa na kuondoshwa mapema, usikute na hii dhulma ya haki za Watanzania, zimechangia, naendelea kusisitiza Mama yetu, if there is anything she can do to help out Watanzania kurejeshewa haki zao, Please do, utabarikiwa, tutabarikiwa na Tanzania itabarikiwa!.

Naamini kabisa kuna siku iso jina, kilio hiki cha haki kitasikika!.

Conclusion.
Namalizia kwa swali la msingi la bandiko hili. Jee Rais Samia anajua kuwa Katiba yetu ina ubatili fulani, uliochomekewa kiubatili hivyo kuifanya Tanzania kuwa na katiba Batili?. Je anajua kuwa hii sheria mpya ya uchaguzi aliyosaini hapa juzi kati ni sheria batili inayokwenda kinyume cha Katiba ya JMT ya Mwaka 1977?. Jee anajua ubatili huu unadhulmu haki ya Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa?. Jee anajua kila dhulma ya haki, huwa ina consequences?.
Jee Rais Samia Afanye Nini?.

Mungu Mbariki Rais Samia, jicho ona lake liione hii dhulma kubwa ya haki ya Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa airejeshe.

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Kongole mwana "Yohana Mtembezi" mwenzangu kwa kuwa mpingaji namba moja wa JF wa uvunjifu wa katiba unaofanywa na walioapa kuilinda katiba hiyo.
Mungu akubariki sana ndugu.

Kule bungeni hatuna wabunge kama mazuzu,mule tuna mazuzu na matutusa.

Bunge ndio linalopaswa kuisimamia serikali,lakini cha kustaajabisha bunge hilo ndilo linalala kitanda kimoja na serikali.

Kule juu sitaki kupeleka lawama maana sote tunajua jinsi palivyo, ni "hakuchi kunakucha".

Nakupongeza sana kwa kuwa mpingaji mkubwa wa uvunjifu wa katiba, lakini kama mwanasheria,tena msomi na mwenye uelewa mpana, tunatokaje hapa tulipofika!!??

Endelea kupumzika kwa amani na mahala pema Mch. Christopher Mtikila.

Wanabodi
Kama kawa, kila nipatapo fursa, huja na makala elimishi za kwa maslahi ya taifa, ambazo huwa na maswali, hoja, majibu utaweka mwenyewe, swali la leo ni Asking Aloud: "Jee Rais Samia anajua kuwa Katiba yetu ina ubatili fulani, uliochomekewa kiubatili hivyo kuifanya Tanzania kuwa na katiba Batili?. Je anajua kuwa hii sheria mpya ya uchaguzi aliyosaini hapa juzi kati ni sheria batili inayokwenda kinyume cha Katiba ya JMT ya Mwaka 1977?. Jee anajua ubatili huu unadhulmu haki ya Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa?. Jee anajua kila dhulma ya haki, huwa ina consequences?.

Kwanza naomba mnisamehe kwa kuandika mabandiko marefu, sometimes nakuwa too emotional, hivyo nondo zina tiririka tuu na ku flows.

Hili shurti la wanasiasa kudhaminiwa na chama cha siasa, ili kugombea uongozi ni shurti batili liko kinyume na katiba ya JMT ya mwaka 1977, na limechomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu.

Kufuatia ubatili huu, unamaanisha katiba yetu ina ubatili, na sheria mpya ya uchaguzi ni sheria batili, Serikali imetunga muswada batili, Bunge letu likatunga Sheria Batili, na Rais akaisaini hiyo Sheria batili kuanza kutumika.

Swali ni Je Rais Rais Samia, anajua kuwa hii sheria mpya ya uchaguzi aliyoisaini juzi juzi, kwa jicho la kisheria ni sheria batili?.

Japo Rais wa Tanzania, ana kinga ya kikatiba ya kutokushitakiwa kwa makosa yoyote atakayotenda akiwa madarakani katika utekelezaji wa majukumu yake ya urais, ila ibara ya 56A imesema specific kuwa kinga hiyo ya rais kutokushitakiwa, inahusu makosa mengine yote, ila haihusu Rais anapovunja katiba ya JMT, anashitakiwa kwa mujibu wa ibara ya 56A.

The only excuse ya rais kusaini sheria batili kuanza kutumika, ni kwa vile Rais wetu sio mwanasheria, hivyo hategemewi kuujua ubatili wa Katiba, ila kwa vile anawasaidizi wake sheria, wakiongozwa na Waziri wa sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hawa ni manguli wa sheria, wabobezi na wabobevu ambao wanaujua kabisa ubatili wa sheria hiyo, na ubatili wa Katiba, lakini hawajamweleza Rais Samia kuhusu ubatili huu kwa excuse kuwa ubatili huu umefanywa na awamu zilizotangulia, Rais Samia kaingia kaukuta, hivyo wakamtungia tuu sheria batili kwasababu sheria ikiyokuwepo nayo ni batili lakini ilikuwa inatumika!.

Kuna kanuni ya the doctrine of separation of powers between mihimili inayokwenda na kitu kinachoitwa checks and balance inayoitaka kila mhimili kuwa kiranja wa mhimili mwenzake usikiuke mamlaka yake wala usikiuke katiba.

Ibara ya 64 (5) ya Katiba imetamka wazi kuwa katiba ndio sheria mama, sheria nyingine yoyote itakayo kinzana na katiba, sheria hiyo itakuwa ni batili. Ijue Katiba kwa Jicho la Mtunga Katiba: Mtunga Katiba alimaanisha nini aliposema "Katiba ni Sheria Mama"? Ni kweli Katiba ni Sheria Mama? sheria batili sio Mahakama, ni katiba yenyewe, jukumu la Mahakama ni kuithibisha tuu huo ubatili na kutangaza kuwa ni batili, tangu siku Mahakama Kuu ya Tanzania ilipouthitisha ubatili huu na kuutangaza, kuanzia hapo ubatili huo unakuwa umeisha batilishika there and then!.

Licha ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuutangaza ubatili huu na kuubatilisha, lakini Serikali ya awamu ya Sita, bado imetunga muswada wa sheria wenye ubatili ule ule, na Bunge letu, likaupokea muswada huo batili na kuutungia sheria kitutusa, hali iliyowafanya wabunge wetu makini kugeuka kama mazuzu vile, checks and balance inatoka wapi?!.

Bunge letu chini mwalimu wangu, mwanasheria mbobezi na mbobevu, Dr. Tulia Akson, alipaswa kulitumia Bunge to i check Serikali kuwa haiwezi kututungia muswada batili, na Bunge lina mamlaka ya kuuondoa ubatili huo na kutunga sheria safi isiyo na ubatili, lakini Bunge letu, likatunga Sheria Batili kitutusa na kumpelekea Rais Samia kuisaini!.

Kwavile Rais Samia anawaamini sana wasaidizi wake, wamemtungia muswada batili na Bunge likitunga Sheria batili, Rais Samia yeye amesaini with very clear conscious kuwa anasaini sheria halali bila wasaidizi wake kumweleza kuwa sheria hiyo ni batili, hivyo kwenye hili la ubatili wa sheria mpya ya uchaguzi, Rais Samia hana kosa kabisa, wenye makosa ni Serikali kutunga muswada batili na Bunge kutunga sheria batili!.
-https://www.jamiiforums.com/threads/tuombe-mwaka-2024-uwe-ni-mwaka-wa-mageuzi-ya-kweli-ya-kidemokrasia-ya-kweli-tanzania-tume-huru-uchaguzi-huru-na-wa-haki-happy-new-year.2172208/
- Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?

Hili la huu ubatili, nimelipigia sana kelele kwenye all fronts,
live, social media na mainstream media. nimepandisha threads zaidi ya 50 !

Je inawezekana ni Anasikia kabisa kilio hiki, ila Wahafidhina wa Chama Chake Ndio Hawataki,

Sikuishia kuandika tuu, pia nimezungumza mara 3 kwenye mikutano

Swali la kujiuliza ni baada ya kelele zote hizi kuhusu ubatili wa Katiba yetu na ubatili wa sheria zetu, jee Rais Samia amezisikia?.

Naona maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa sheria batili yanaendelea, na mwakani tunakwenda kwenye uchaguzi mkuu na katiba batili na sheria batili!.

Kwa vile Mungu ni haki, no one knows for sure kwanini yule aliitwa na kuondoshwa mapema, usikute na hii dhulma ya haki za Watanzania, zimechangia, naendelea kusisitiza Mama yetu, if there is anything she can do to help out Watanzania kurejeshewa haki zao, Please do, utabarikiwa, tutabarikiwa na Tanzania itabarikiwa!.

Naamini kabisa kuna siku iso jina, kilio hiki cha haki kitasikika!.

Conclusion.
Namalizia kwa swali la msingi la bandiko hili. Jee Rais Samia anajua kuwa Katiba yetu ina ubatili fulani, uliochomekewa kiubatili hivyo kuifanya Tanzania kuwa na katiba Batili?. Je anajua kuwa hii sheria mpya ya uchaguzi aliyosaini hapa juzi kati ni sheria batili inayokwenda kinyume cha Katiba ya JMT ya Mwaka 1977?. Jee anajua ubatili huu unadhulmu haki ya Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa?. Jee anajua kila dhulma ya haki, huwa ina consequences?.
Jee Rais Samia Afanye Nini?.

Mungu Mbariki Rais Samia, jicho ona lake liione hii dhulma kubwa ya haki ya Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa airejeshe.

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
 
Tuwe na Imani na viongozi wetu wa siasa na viongozi wa dini.
Watu wanapaniki sana kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu.
 
Kwamba katiba batili sio kwa Rais hadi Mama naye?
Sasa nani atawajibika?
Ni kweli katiba yetu ni batili kwasababu imenajisiwa na kuchomekewa ubatili. Walionajisi na waliochomeka ubatili huo, hawaijui katiba, wala hawajui walichofanya ni ubatili!, ila Mahakama Kuu ya Tanzania iliishautangaza ubatili huo na kuubatilisha.

Serikali ikapinga kwa kukata rufaa, Mahakama ya Rufani ikakiri ni ubatili uliofanywa na mhimili wa Bunge, hivyo ukarudishwa Bunge ndio liuondoe ubatili huo!, mpaka leo, Bunge halijauondoa, linaendelea kutunga sheria batili!.

Mama alipoingia, aliukuta huu ubatili, na awamu yake wanauendeleza!.

The only person wa kuwajibika ni mtu mmoja tuu, mwenye katiba.
P
 
Alipomteua Doto kuwa Naibu PM kinyume na katiba tulisema nyie wasaka fursa mkaona sisi tunaona wivu, hakuna mvunja katiba mkuu kama huyu maza hata yeye amewahi kuidharau katiba na kusema kijitabu mkashangalia.
Presidential appointment powers zinamruhusu Rais wa JMT to create any positions, hivyo yeye sii wa kwanza, alianza Rais Mwinyi alipomteua Lyatonga Mrema.
Ubatili wa Katiba ninauzungumza hapa ni uvunjifu wa Katiba kwa kutunga sheria batili inayokwenda kinyume na katiba, baada ya Mahakama kuutamka huo ni ubatili, Serikali Yetu ikauchukua ubatili huo na kuuchomekea kiubatili ndani ya katiba yetu ili kuuhalalisha!.
Serikali na Bunge, zinajifanya mbuni kujificha kichwa ndani ya mchanga na kujijua hazionekani!.
Ninachofanya hapa ni kumfungua tuu macho Mama kuwa tuna katiba batili na Serikali yake inaendelea kutunga sheria batili na kumpelekea yeye kuzisaini zianze kutumika!.

Kwa vile wasaidizi wake sheria hawamwelezi ukweli, acha tujitolee kuwasaidia kumweleza, ili tuachana na ubatili huu!.
P
 
Tanzania nchi yenye mbumbumbu wengi kiasi tunashindwa na sisimizi wadogo wanaoendesha maisha yao kwa kufuata katiba yao ya kutogombania mzoga na kuwa na haki sawa kwa wote.
Usiwatukane Watanzania mbumbumbu kwasababu kuielewa katiba kunahitaji a specialised knowledge, ambayp ni wachache wanajaaliwa kuwa nayo, ndio maana hao waserikali wanatunga miswada batili!, Bunge linatunga sheria batili, na Rais anasaini sheria batili kuanza kutumika!, huku wote wakijua na sheria halali, kwa kutoijua tuu katiba!.

Mimi nimejitolea kusaidia uelimishaji umma kuhusu, katiba, sheria na haki.
P
 
Usiwatukane Watanzania mbumbumbu kwasababu kuielewa katiba kunahitaji a specialised knowledge, ambayp ni hub wachache wanajaaliwa kuwa nayo, ndio maana hao waserikali wanatunga miswada batili!, Bunge linatunga sheria batili, na Rais anasaini sheria batili kuanza kutumika!, huku wote wakijua na sheria halali, kwa kutoijua tuu katiba!.

Mimi nimejitolea kusaidia uelimishaji umma kuhusu, katiba, sheria na haki.
P

"kuielewa katiba kunahitaji a specialised knowledge"! Hatujawa mbumbumbu kiasi hicho, msitake kutupeleka chuo kikuu kusomea katiba kwa miaka mitano! Kwenye katiba kuna vipengele vingi sana, mimi sihitaji kuvijua vyote kwa wakati mmoja, ninachohitaji ni kuvijua vinavyohusu maisha yangu ya kila siku, japo nyie mnatudanganya kuwa katiba haituletei ugali mezani mkidhani sijui haki yangu ya mazao ninayolima.
Leo ndiyo nimejua kuwa mbumbumbu ni tusi kwa wanaccm! Kama ungeniita bungeni nikajieleze kuhusu kusema watanzania wengi ni mbumbumbu ningekushangaa kwani sijasema watanzania wote; hata hivyo ni njia nzuri ya kumnyamazisha mtu.
Na unatamani uwe Lakha!
 
3CB9F249-E459-4A85-911B-7C4C93F8F1D6.jpeg

Hii katuni ya Masoud ilinichukua muda sana kuielewa..
 
Alipomteua Doto kuwa Naibu PM kinyume na katiba tulisema nyie wasaka fursa mkaona sisi tunaona wivu, hakuna mvunja katiba mkuu kama huyu maza hata yeye amewahi kuidharau katiba na kusema kijitabu mkashangalia.
Rais ana mamlaka ya kikatiba kuunda na kuondoa cheo katika serikali, kwa hiyo hapo hakumteua Naibu PM kinyume na katiba, aliunda cheo cha Naibu PM.
 
Cheo cha Rais, Makamo, PM, Mawaziri na Wakuu wa Mikoa vimetajwa kwenye katiba, nionyeshe cheo cha Naibu PM kimetajwa kwenye ibara ipi? Kwamba Waziri Mkuu aliyepo ameshindwa kazi mpaka awe na Naibu? Mrema alivyoomba maslahi ya Naibu PM aliambiwa hicho cheo hakipo kikatiba na Ndugai au ulikuwa bado mchanga?
 
Presidential appointment powers zinamruhusu Rais wa JMT to create any positions, hivyo yeye sii wa kwanza, alianza Rais Mwinyi alipomteua Lyatonga Mrema.
Ubatili wa Katiba ninauzungumza hapa ni uvunjifu wa Katiba kwa kutunga sheria batili inayokwenda kinyume na katiba, baada ya Mahakama kuutamka huo ni ubatili, Serikali Yetu ikauchukua ubatili huo na kuuchomekea kiubatili ndani ya katiba yetu ili kuuhalalisha!.
Serikali na Bunge, zinajifanya mbuni kujificha kichwa ndani ya mchanga na kujijua hazionekani!.
Ninachofanya hapa ni kumfungua tuu macho Mama kuwa tuna katiba batili na Serikali yake inaendelea kutunga sheria batili na kumpelekea yeye kuzisaini zianze kutumika!.

Kwa vile wasaidizi wake sheria hawamwelezi ukweli, acha tujitolee kuwasaidia kumweleza, ili tuachana na ubatili huu!.
P
Wapi kwenye katiba imetajwa? Rais, Makamu, PM, Mawaziri na wakuu wa Mikoa wametajwa kwenye katiba, tuonyeshe Naibu PM ametajwa wapi? Kateua Jaji Mkuu amembaye kikatiba anatakiwa kuwa amestaafu kavunja katiba, kimsingi hakuna mvunja katiba kama huyu maza
 
Back
Top Bottom