Asking Aloud: Rais Samia anajua Katiba yetu ni batilifu, na Sheria mpya ya uchaguzi aliyosaini ni sheria batili kinyume cha katiba?

Mayala

nakukumbusha tu,TANZANIA ni kisiwa katika suala la sheria au katibakwanza kabisa ukiongelea sura ya mwanzo ya katiba kuhusu kuitambua serikali ya muungano hilo jambo ni batili sababu kinachoungana kinakuwa na mkataba,mkataba sharti uwe na ukomo.

ukizungumzia uhuru wa kupiga na kupigiwa kura ni batili,tTanzania haina private candidate.

Majukumu na haki ya za rais ni over power,Rais amegewa ardhi ya TANZANIA anweza kumuhamisha yeyote.

sheria zina contradictions kibao.
 
Yawezekana ikawa kweli au si kweli.
Kwa mfano ni kweli...
1."Nini kifanyike,lakini pia akikubali kubadilisha tusogeze uchaguzi Mkuu mbele ili mchakato wake ufanyiwe review na wadau?
2."Kwanini wasomi na wadau wamemchomekea Mh.Rais contents kinyume na Katiba,ajenda yao ni nini hasa"?
 
Kongole mwana "Yohana Mtembezi" mwenzangu kwa kuwa mpingaji namba moja wa JF wa uvunjifu wa katiba unaofanywa na walioapa kuilinda katiba hiyo.
Mungu akubariki sana ndugu.

Kule bungeni hatuna wabunge kama mazuzu,mule tuna mazuzu na matutusa.

Bunge ndio linalopaswa kuisimamia serikali,lakini cha kustaajabisha bunge hilo ndilo linalala kitanda kimoja na serikali.

Kule juu sitaki kupeleka lawama maana sote tunajua jinsi palivyo, ni "hakuchi kunakucha".

Nakupongeza sana kwa kuwa mpingaji mkubwa wa uvunjifu wa katiba, lakini kama mwanasheria,tena msomi na mwenye uelewa mpana, tunatokaje hapa tulipofika!!??

Endelea kupumzika kwa amani na mahala pema Mch. Christopher Mtikila.

Tuwe na Imani na viongozi wetu wa siasa na viongozi wa dini.
Watu wanapaniki sana kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu.
 
Kwamba katiba batili sio kwa Rais hadi Mama naye?
Sasa nani atawajibika?
Ni kweli katiba yetu ni batili kwasababu imenajisiwa na kuchomekewa ubatili. Walionajisi na waliochomeka ubatili huo, hawaijui katiba, wala hawajui walichofanya ni ubatili!, ila Mahakama Kuu ya Tanzania iliishautangaza ubatili huo na kuubatilisha.

Serikali ikapinga kwa kukata rufaa, Mahakama ya Rufani ikakiri ni ubatili uliofanywa na mhimili wa Bunge, hivyo ukarudishwa Bunge ndio liuondoe ubatili huo!, mpaka leo, Bunge halijauondoa, linaendelea kutunga sheria batili!.

Mama alipoingia, aliukuta huu ubatili, na awamu yake wanauendeleza!.

The only person wa kuwajibika ni mtu mmoja tuu, mwenye katiba.
P
 
Alipomteua Doto kuwa Naibu PM kinyume na katiba tulisema nyie wasaka fursa mkaona sisi tunaona wivu, hakuna mvunja katiba mkuu kama huyu maza hata yeye amewahi kuidharau katiba na kusema kijitabu mkashangalia.
Presidential appointment powers zinamruhusu Rais wa JMT to create any positions, hivyo yeye sii wa kwanza, alianza Rais Mwinyi alipomteua Lyatonga Mrema.
Ubatili wa Katiba ninauzungumza hapa ni uvunjifu wa Katiba kwa kutunga sheria batili inayokwenda kinyume na katiba, baada ya Mahakama kuutamka huo ni ubatili, Serikali Yetu ikauchukua ubatili huo na kuuchomekea kiubatili ndani ya katiba yetu ili kuuhalalisha!.
Serikali na Bunge, zinajifanya mbuni kujificha kichwa ndani ya mchanga na kujijua hazionekani!.
Ninachofanya hapa ni kumfungua tuu macho Mama kuwa tuna katiba batili na Serikali yake inaendelea kutunga sheria batili na kumpelekea yeye kuzisaini zianze kutumika!.

Kwa vile wasaidizi wake sheria hawamwelezi ukweli, acha tujitolee kuwasaidia kumweleza, ili tuachana na ubatili huu!.
P
 
Tanzania nchi yenye mbumbumbu wengi kiasi tunashindwa na sisimizi wadogo wanaoendesha maisha yao kwa kufuata katiba yao ya kutogombania mzoga na kuwa na haki sawa kwa wote.
Usiwatukane Watanzania mbumbumbu kwasababu kuielewa katiba kunahitaji a specialised knowledge, ambayp ni wachache wanajaaliwa kuwa nayo, ndio maana hao waserikali wanatunga miswada batili!, Bunge linatunga sheria batili, na Rais anasaini sheria batili kuanza kutumika!, huku wote wakijua na sheria halali, kwa kutoijua tuu katiba!.

Mimi nimejitolea kusaidia uelimishaji umma kuhusu, katiba, sheria na haki.
P
 
"kuielewa katiba kunahitaji a specialised knowledge"! Hatujawa mbumbumbu kiasi hicho, msitake kutupeleka chuo kikuu kusomea katiba kwa miaka mitano! Kwenye katiba kuna vipengele vingi sana, mimi sihitaji kuvijua vyote kwa wakati mmoja, ninachohitaji ni kuvijua vinavyohusu maisha yangu ya kila siku, japo nyie mnatudanganya kuwa katiba haituletei ugali mezani mkidhani sijui haki yangu ya mazao ninayolima.
Leo ndiyo nimejua kuwa mbumbumbu ni tusi kwa wanaccm! Kama ungeniita bungeni nikajieleze kuhusu kusema watanzania wengi ni mbumbumbu ningekushangaa kwani sijasema watanzania wote; hata hivyo ni njia nzuri ya kumnyamazisha mtu.
Na unatamani uwe Lakha!
 
Alipomteua Doto kuwa Naibu PM kinyume na katiba tulisema nyie wasaka fursa mkaona sisi tunaona wivu, hakuna mvunja katiba mkuu kama huyu maza hata yeye amewahi kuidharau katiba na kusema kijitabu mkashangalia.
Rais ana mamlaka ya kikatiba kuunda na kuondoa cheo katika serikali, kwa hiyo hapo hakumteua Naibu PM kinyume na katiba, aliunda cheo cha Naibu PM.
 
Rais ana mamlaka ya kikatiba kuunda na kuondoa cheo katika serikali, kwa hiyo hapo hakumteua Naibu PM kinyume na katiba, aliunda cheo cha Naibu PM.
Cheo cha Rais, Makamo, PM, Mawaziri na Wakuu wa Mikoa vimetajwa kwenye katiba, nionyeshe cheo cha Naibu PM kimetajwa kwenye ibara ipi? Kwamba Waziri Mkuu aliyepo ameshindwa kazi mpaka awe na Naibu? Mrema alivyoomba maslahi ya Naibu PM aliambiwa hicho cheo hakipo kikatiba na Ndugai au ulikuwa bado mchanga?
 
Wapi kwenye katiba imetajwa? Rais, Makamu, PM, Mawaziri na wakuu wa Mikoa wametajwa kwenye katiba, tuonyeshe Naibu PM ametajwa wapi? Kateua Jaji Mkuu amembaye kikatiba anatakiwa kuwa amestaafu kavunja katiba, kimsingi hakuna mvunja katiba kama huyu maza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…