Askofu anamiliki HAMMER ya 250million!

Status
Not open for further replies.
wajinga ndio waliwao......wanaojiita wachungaji wote wezi na matapeli tu.
Tatizo la wengi wasiojuwa jinsi ya kumiliki mema ni KUJAA WIVU MWINGI usiokuwa na faida kwao, hujui huyu mtu aliumia kiwango gani mpaka kuja kumiliki Hammer mnachojuwa ni kubwabwaja bila mipaka, kuwa nalo yeye inakupunguzia nini wewe au unagain nini, nini hasa kikufanye mpaka umchunguze mtumishi wa watu, mimi sio pastor na sio muumini wa hapo,lakini naamini pastor wa kweli ana haki ya kumiliki zaidi ya hapo. anatakiwa na ndege yake pia.
 
Hallo, nashukuru kwa maswali yako. God counts both quality and quantity, however, you are no body to know what is or what is not quantity or quality, kwasababu kwa upeo wako, naona hauelewi kitu kabisa, na sitahangaika kupoteza muda kukuelewesha, ukitaka okoka ukamwulize mchungaji wako.

Pili, ni vigumu sana wewe mwanadamu ambaye ni sisimizi mbele za Mungu, kuamua ni nini sahihi na nini si sahini, kwasababu mawazo ya mwanadamu ni mafupi kama pimbi. USICHANGANYE KAELIMU KAKO kuchanganua nini kitu cha Mungu kizuri au si kizuri kwa upeo wako, utapoteza muda bure, ndo maana mnakaa kuanza kujadili watumishi wa Mungu mkifikiri labda watumishi wa Mungu nisawa na watumishi wa selikali au NGO. Kunambia nisihukumu nisije nikahukumiwa, naona hauelewi maana ya sentensi hiyo biblically, hivyo, nakushauri ufike pale UBUNGO KANISA LA UFUFUO NA UZIMA, Utasaidiwa mambo mengi. Ila nakushauri, usije kuwa na juju au hirizi kiunoni humu, ukifika pale Kuna nguvu ya Mungu, utalipuka. kwa heri.
 

Kazi ipo...sasa God counts both quality and quantity, however, you are no body to know what is or what is not quantity or quality, ulijuaje haya kama mwanadamu hapaswi kujua...hayo mengine.....
 
Hamtuambii ni nani anayemiliki hiyo Hammer ila mmetoa orodha ya watumishi wa MUNGU semeni ni nani kati yao?? au wote wanamiliki magari ya aina ya Hammers???? Vinginevyo ninyi ni wazushi
 

Wanaosali pale ninawafahamu, hawana matusi na maneno machafu kama uliyonayo wewe! mwanadamu mbele za Mungu si sisimizi wala pimbi-mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu na si pimbi, isome upya Biblia. Angalikuwa hivyo Yesu asingemfia msalabani. mwanadamu yeyote anathamani sana mbele za Mungu kiasi Mungu anajua hata idadi ya nywele kichwani mwake. Hukunielewa, umejawa na hulka tu ya kumpenda mchungaji wako, jambo ambalo ni jema sana lakini halikupi spiritual immunity ya kuropoka hovyo. Swali langu la pili lilikuwa la msingi sana kwa wewe kudigest kutokana na comment zako

lakini nakupa ushauri wa bure angalia ulimi na kauli zako ili ziendane na kile unachoproclaim - WOKOVU.

Kauli zako si za aliyeokoka, ni kama za hamas anapomtukana mwisraeli -vinginevyo usijiite Mwana wa Mungu.

Soma ulichoandika na jiangalie upya.
Roho Mtakatifu akusaidie
 

anepingana na mungu akuna tofauti na kahaba so mungu akashugulike na yoyote anaepingana na maandiko ya bwana
 
Anayemiliki hammer yule mchungaji wa kanisa la ubungo maji(kanisa la misukule)
 
Kuna mchungaji mmoja ana kanisa lake Mbagala, halafu huwa anakuja kunywa bia Brake Point Kijitonyama ili waumini wake wasimuone! Amkeni jamani, don't be brainwashed. Muwe mnatumia na akili zetu vizuri wakati mwingine, msipelekwe pelekwe tu!
 
Kuna mchungaji mmoja ana kanisa lake Mbagala, halafu huwa anakuja kunywa bia Brake Point Kijitonyama ili waumini wake wasimuone! Amkeni jamani, don't be brainwashed. Muwe mnatumia na akili zetu vizuri wakati mwingine, msipelekwe pelekwe tu!

kanisa gani? halina jina? hatuhitaji jina lake, taja kanisa tu
 
Yaani ulaji fitana ni kila sehemu hivyo hakuna cha ajabu maana hawa viongozi wetu wa dini ndio wanafanya mambo ya ajabu kama haya
 
Ninyi mnaofuata hizi dini hebu nisaidieni. Sijaelewa ni kwa nini Mungu aumbe kila kitu including binadamu, halafu amtake binadamu atoe sadaka. Binadamu ana nini cha kumpa Mungu ilhali vyote including binadamu mwenyewe ni mali ya Mungu?

Watu mnadai 'fungu la kumi' ni mali ya Mungu, inakuwaje Mungu ashindwe kujitengea mwenyewe fungu hilo la vitu alivyoumba mwenyewe, hadi asubiri utashi wa binadamu (kiumbe chake) wa kumgawia? Contradiction nyingine ni kuwa hata huo utashi ni Mungu ameumba, ni yeye mwenyewe amefanya binadamu mmoja awe tofauti na mwingine, mmoja akubali kutoa hilo fungu na mwingine akatae. Hivi ni kweli kuwa ni Mungu anayehitaji hii michango? Labda si huyu tunayesikia kuwa ndiye aliyeumba kila kitu!

Na kama hizo pesa za sadaka anapewa Mungu, mbona tunaona zikitumika kununua magari kama haya yanayojadiliwa hapa, na watumiaji wake ni binadamu? Au hii ni lugha ya picha tu, kuwa hao wajanja-wajanja (wanaojiita maaskofu, wachungaji, manabii nk) ndio mungu mwenyewe?
 

Nimeipenda arguement yako. Niongeze tu kidogo. Labda imefika wakati kwa wabantu kurudi kwenye taratibu zao za kumuomba Mungu kupitia Milima na Mibuyu yao. Maana hata Hizi dini tulizoletewa zinatuambia kuwa huwezi kwenda kwa Mungu bila kupitia kwa mtu fulani na kadhalika.
Wazee wetu walipokuwa wakitoa kafara kwenye Mbuyu ama Mlima hawakuwa hawakuwa na maana kuwa wanauabudu ule mlima bali walikuwa wanajua kuwa alikuwepo mkubwa zaidi aliyeuweka hivyo walikuwa wanamsujudia kupitia huo Mlima/Mbuyu.
Naamini hata sasa ndivyo dini tulizoletewa zinavyofanya.
na sasa zinatuingia kwenye contradictions.
waitwao watumishi wa Mungu sasa ndio wanaoongoza kwa kudilute vifungu vya Maandiko matakatifu ili kuhalalisha uozo wao.
Ndio hao sasa wanataka kutuaminisha kuwa ni sawa Mtumishi wa Mungu kuwa na Gari la bei mbaya lakini wakati huo huo awe mstari wa mbele kuikemea serikali kuwa inawaacha mafisadi...
Ndio hao hao sasa wanataka kuhalalisha kuwa mtumishi wa Mungu ana haki ya kuwa Gay na kuwaongoza waumini wengine kwenye sala!!#@#*&^%$#@!!!😡
Kwa hakika wakati mwingine najikuta nikilazimika kumu-admire Mzee wetu mheshimiwa sana Kingunge N.M! At least hakufuata mkumbo wa sisi wengine wa kupapatikia hizi dini za kuja na mambo yake yanaenda vyema tu!!!
 
1. Mimi huwa si mtu ninayejadili sana mambo ya dini maana dini haina faida kwa maisha ya mwanadamu. Ila kwa msaada tu nilikuwa nasali kwenye moja ya dini hizi mbili mnazozizungumzia hapa za kale sana na si za kisasa kwa mujibu wa maelezo yenu.

2. Niliondoka kwa sababu muda wa kukaa huko ulitimia na ilikuwa lazima niondoke. Sasa suala la kuwa kuna Mungu au hakuna mimi sijui lakini nilipokea wito mpya baada ya miaka kama 5 hivi tangu niokoke, na niliondoka. Si unakumbuka Mungu alivyosema na Ibrahim kwamba ondoka kwa watu wako na jamaa zako nitakuonyesha mahali pa kwenda? sasa niko njiani naelekea huko Kanaani mpya. Suala la kukaa pale sio valid tena.

3. Kuna watu waliookoka wanaomtumikia Mungu kwenye kanisa nililotoka lakini kila mtu ameitwa kivyake hivyo siwezi kuwasemea. Ninavyojua wao pia wako pale kwa mpango wa Mungu na akiwataka waondoke wataondoka tu.

4.Swali hili nimelijibu kwenye jibu namba mbili. Ni kwamba nimeitwa sijui kwa sababu pale pakoje Mungu mwenyewe anajua. Ninachojua ukimuamini Yesu utaokoka mahali popote ulipo. Hata kwenye baa na kwenye madisko watu ukutana na Mungu na kuokoka. Kila mtu ameitwa kivyake. Alivyoitwa Petro si sawa alivyoitwa Barnaba wala alivyoitwa yule mtu wa kushi kule jangwani na wala sivyo alivyoitwa Sauli (Paulo). Na wewe unaweza kuitwa kivyako vyako sintaona ajabu. Fungua moyo wako mpe Yesu maisha yako uokoke.

5.Kwa wale ambao wana miaka kumi hawajaumwa nawashauri wampe Mungu utukufu maana yeye ni mwema sana uwapa mvua na mavuno wabaya na wema kwa makusudi kabisa, kama vile anavyowaponya wagonjwa na kuwaweka huru kutoka kwenye vifungo hivyo kwa makusudi kabisa........
 
Kumbe unajua values za wokovu sio?
Nakupa shauri Okoka basi!
 
Kumbe unajua values za wokovu sio?
Nakupa shauri Okoka basi!
 


Hapa ndipo waswahili huwa mnaniachaga hoi. Sasa, nyie mnadhani askofu ndiyo hataki kuishi maisha ya juu kama walivyo wengine?!
Ni madhehebu machache tu duniani, likiwamo Katoliki ambao wanawataka wachungaji/pastors wao waishi maisha ya kawaida. Na hii ni amri ya kanisa, siyo ya biblia, yaani hakuna sehemu ilipoandikwa kuwa askofu au mchungaji aishi maisha ya taabu huku waumini wao wakitanua!.
Waache watanue bila kujali source ya pesa zao, ili mradi waumini wao wamekubali kutoa mchango yao kuwawezesha waishi hivyo. Afterall, wewe dhehebu si lako, unawashwa nini?
 
Soma biblia vizuri.inasema hivi itakuwa vigumu kwa matajiri kuona ufalme wa binguni kuliko maskini kupita kwenye tundu la sindano. yesu ilimwapia yule bwana aliyemuuliza kwamba afanye nini ili arithi ufalme wa binguni yesu kamwabia vyote gawia maskini.Swali kwako, je wachungaji nao si ni binadamu wanaopigania kuingia ufalme wa binguni?
 
Yohana 12:26
Anayetaka kunitumikia ni lazima anifuate, hivyo kwamba popote pale nilipo mimi ndipo na mtumishi wangu atakapokuwa. Mtu yeyote anayenitumikia Baba yangu atampa heshima.

Please note the bolded words yana maana sana.
Na hilo andiko ambalo una quote linazungumzia nyie hasa matajiri msiotaka kutoa sadaka ziliwe na hao makuhani. Nyie matajiri wa sasa msiotaka kutoa sadaka mko kwenye hatari ya kukosa huo ufalme.
 
17 Yesu alipoanza tena safari yake, mtu mmoja alimjia mbio, akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, "Mwalimu mwema, nifanyeje ili niupate uzima wa milele?"

18 Yesu akamjibu, "Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mungu peke yake.

19 Unazijua amri: `Usizini; Usiue; Usiibe; Usitoe ushahidi wa uongo; Usidanganye; Waheshimu baba na mama yako."`

20 Naye akamjibu, "Mwalimu, hayo yote nimeyazingatia tangu ujana wangu."

21 Yesu akamtazama, akampenda, akamwambia, "Umepungukiwa na kitu kimoja: nenda ukauze vitu ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate."
22 Aliposikia hayo, alisikitika, akaenda zake akiwa na huzuni, kwa maana alikuwa na mali nyingi.
23 Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, "Jinsi gani itakavyokuwa vigumu kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu!"

24 Wanafunzi walishangazwa na maneno yake. Yesu akawaambia tena, "Watoto wangu, ni vigumu sana kuingia katika Ufalme wa Mungu!

25 Ni rahisi zaidi ngamia kupenya katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu."
26 Wanafunzi wake wakashangaa sana wakaulizana, "Ni nani basi, atakayeweza kuokoka?"

27Yesu akawatazama, akawaambia, "Kwa binadamu haiwezekani, lakini kwa Mungu si hivyo, maana kwa Mungu mambo yote huwezekana."
28 Petro akamwambia, "Na sisi je? Tumeacha yote, tukakufuata!"
29 Yesu akasema, "Kweli nawaambieni, kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu, au dada, au mama, au baba, au watoto au mashamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya Habari Njema,
30 atapokea mara mia zaidi wakati huu wa sasa nyumba, ndugu, dada, mama, watoto na mashamba pamoja na mateso; na katika wakati ujao atapokea uzima wa milele.
31 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza."

Kwa faida yako na wengine wanaotumia andiko hilo nimekuwekea passage yote uisome vizuri upate kuelewa maana wengi hapa wanadandia maandiko bila kuyasoma na hii ni hatari hata kwao wenyewe. Biblia huwa haisomwi kwa kudandia wapinga Kristo wanavyosema; bali kama biblia yenyewe inavyosema.
Soma vizuri, elewa story ilianzia wapi na kwa nini Yesu alisema hivyo. Na hapo utagundua wala unavyojaribu kulitumia andiko hilo sivyo. Badala yake linaweza kuwa linazungumza na wewe kabisa! Kuwa muangalifu kaka/dada/baba/mama. usije ukatumiwa kama yule jamaa wa Luka 4:3-12 aliyejaribu kutumia maandiko isivyotakiwa dhidi ya Yesu mwenyewe.
 
Kazi ipo...sasa God counts both quality and quantity, however, you are no body to know what is or what is not quantity or quality, ulijuaje haya kama mwanadamu hapaswi kujua...hayo mengine.....

Yaani nimewaza the same thing kwa kweli, sijui amejuaje...
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…