Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,904
- 1,064
Kiby, Hivi kumtetea askofu kuna kosa gani? maana si wote kwamba tutakuwa na mawazo yaliyo sawa. Najua leo kuna wengine wanaona iwe hivi na wengine tunaona tuwe hivi.Sitaki kujiingiza katika mtego wa mtu aliye amua kumtetea Askofu kuliko kuitetea kweli ya Yesu. Hata nikikupa ushahidi utaukubali?? Kuna jirani yangu mchaga wa rombo ameniomba nauli ya kuhudhuria massomo ya katikati ya wiki hapo ufufuo na nimemsaidia kama mara nne. Yeye anatokea magomeni kagera. Sasa wewe hukumu mwenyewe kuomba nauli kuhudhuria mafundisho ya bilionea wapi na wapi.
Namshangaa sana huyo anayekuomba nauli wewe kwenda kule kanisani maana maandiko yanatuzuia. Hata hivyo kuna kosa gani mtu kuomba msaada kwa jamii yake?
Leo hii wewe unatanua kwenye internet lakini kuna watu wanatamani hawawezi, sijui umewasaidia nini. Wengine wanatumia hata net za maofisini bure wakati kuna watu wanatamani hawawezi.
Jaribu kuelewa kuwa hapa duniani haitakuja kuwezekana watu wote tukawa sawa. Tunaishi mtaa mmoja na wote tunalipa same tax to the government lakini uwezo wetu na hata huduma kwetu huko huko mitaani inatofautiana. Hatuwezi kuwa sawa hata siku moja watu wote. Bado wahitaji wataendelea kuwapo na wenye uwezo wataendelea kuwepo. Na wote tunaishi mtaa mmoja huo huo.
Sijui kama umeelewa nini hasa point yangu.