Kuna wengi wana uliza kama mimi nasali makanisa hayo, ndiyo, mimi ni prominent religious person wa karibu sana na watu hao wote. Nina uhakika huyo ana makanisa Japan, Korea na China. I mean the one mwenye kanisa la UFUFUO NA UZIMA pale ubungo, na gari ile alipewa zawadi na makanisa ya japan. mimi nasali hapo. njoo pale hata leo, utakuta kuna wajapani wamejaa pale, wengine wamekuja kujifunza uchungaji from him, wengi wanaishi hapa.
Kwa mchungaji mwingine, hasa mwenye hammer nyeupe sijui, naye si tatizo pamoja na kwamba sisali huko, ila ni wenzangu katika Bwana. Hii ni kitu cha kawaida.
Angalia wahubiri kama kina Bonke, Beny Hinn etc, hawa wanamiliki ndege, ma vitu vya thamani, vingine wamepewa tu na washirika wao watumie, na huwezi kuwalazimisha waviuze, wewe unayetaka waviuze ni wivu tu kwa vitu ambavyo haujachangia. kwa kifupi kwetu sisi walokole, tunaamini kuwa, UKIMPOKEA mtumishi wa Mungu kwa kumbariki na kitu chochote, unampokea Mungu, "imeandikwa, atakayempokea yeye niliyemtuma, anipokea mimi, na awayeyote atakaye mpa mtumishi wangu nga kikombe cha maji, atapata thawabu, pia, ampokeaye nabii, atapata thawabu ya nabii". HIVYO, ukimchangia mtumishi wa Mungu kwa chochote, iwe pesa, gari, ndege, nyumba etc lazima utapata thawabu kwa Mungu. HII NI IMANI YETU, hatuhitaji wewe uturidhie kama ni vyema au si vyema, and DON'T EVER QUESTION vile tunavyofanya kwa watumishi wetu, na hatutaki muwajadili watumishi wetu, kwasababu ni sisi tunaowahudumia.
Pia, tangu agano la kale, Mungu aliwaamuri wana wa Israel wawape Walawi fungu la kumbi la kila watakachopata. KWANINI?, Kwasababu walawi hawakupata urithi wa ardhi kule Israel kati ya yale makabila kumi na mawili. Na fungu hili la Kumi, Mungu alisema litakuwa ndio urithi wao walawi AMBAO NI UKOO WA KIKUHANI/KICHUNGAJI.
Hivyo, Wachungaji wa kilokole ni Walawi wetu, kila tunachopata tunatakiwa kutoa fungu la kumi, na linaenda moja kwa moja kwenye account zao. THE BIGGER THE NUMBER OF MEMBERS YOU HAVE, THE BIGGER THE TITHE(TEN PERCENT) WILL BE. Hivyo, kama mchungaji ni mzembe ana wanashirika wachache, atapata fungu chache ambalo hata nunua hata baiskeli, labda tu abarikiwe kwa namna nyingine na washirika. Angalia, Kakobe, Gwajima, Gamanywa, Lwakatale, Efatha, kuna watu zaidi ya elfu ishirini wengine. KUNA NAMNA YA KU APPROPRIATE PESA ZA KANISA, KWA KUFUATA BIBLIA, NA WACHUNGAJI HAO WOTE HAWAJAKOSEA KITU.
KUSEMA KUWA WAUZE ILI PESA WASAIDIE WATU, HUO NI MTAZAMO WAKO. Mungu ndiye anajua namna anavyowasaidia hao unaowaonea huruma. KIKUBWA HAPA NI WIVU TU KWASABABU MNAONA MUNGU AMEWABARIKI. Fumbeni midomo yenu kwa Jina la Yesu, na nawahakikishia, mtavuna mnachopanda kwenye mioyo ya watu hapa, ukimgusa mtu wa Mungu, umemgusa Mungu, ukimdhihaki mtu wa Mungu, umemdhihaki Mungu mwenyewe, ukimshambulia pia unamshambulia Mungu, NA WASHINDANAO NA BWANA WATAPONDWA KABISA, JIANDAENI KUPONDWA KABISA. ASANTE.