Sawa, Mkuu. lakini hakuna anayesema kuwa Mtumishi wa Mungu awe masikini. Tunachosema ni kuwa ni vizuri Mtumishi wa Mungu akawa na Kiasi, hata Mungu mwenyewe ameyasema haya. Kuwa na Kiasi.
Ni Mungu huyu huyu pia aliyesema kawagaie masikini vyote ulivyo navyo, kisha unifuate.
ni Mungu huyu huyu anayesema kuwa ni rahisi kwa Ngamia kupita katika tundu la Sindano kuliko tajiri kuingia Ufalme wa Mungu.
Ni Mungu huyu huyu alieyesema kuwa hamuwezi kutumikia Mabwana wawili. Mungu na Mali.
Ni Mungu huyu huyu ambaye Mwna wake wa Pekee alipokuwa anatafuta wanafunzi wa kumsaidia kueneza neno la Ufalme wa Mungu alichagua watu wa chini kabisa, Wavuvi, Seremala nk. Hakuchagua tajiri miongoni mwa wanafunzi wake. Kuna somo kubwa hapo ambalo Wahubiri wetu wa kileo hawalioni.
Hatusemi Watumisghi wa Mungu wasiwe na Uwezo la hasha. Tunachosisitiza ni kuwa na kiasi, neno ambalo hata Mungu mwenyewe ametuasa nalo.
kama jamii nzima inakubaliana kwamba gari la aina ya Hummer ni gari la kifahari, pamoja na mwenzetu kusema ni trekta la kazi, kwa nini mtumishi wetu wa Mungu asiamue kununua Landrover, Toyota Surf na kadhalika??
Anapanda Hummer la mamilioni anakwenda kuhubiri injili wapi, for Heaven's sake??
After all, si hata Mwana wa Mungu kuna mahali amesema kuwa mnapoenda kuhubiri neno lake msibebe zaidi ya nguo na makubazi mliyovaa bila shaka akiwa na maana ya kuwa na kiasi katika mahitaji yenu? haya ya kwenda kuhubiri na Hummer yameanzia wapi??
Nimalizie tu kwa kusema kuwa kama ni vifungu, basi kila mmoja anaweza kutafsiri kifungu cha Biblia kwa jinsi anavyokiona yeye na ndio maana traditional churches zetu zimekuwa zikiparaganyika na kuanzishwa makanisa binafsi chungu nzima ambayo watumishi wa Mungu wanaoyamiliki wanaweza hata kukusomea vifungu vinavyowaruhusu kuwa na Hummer!
Indeed, Come to think of it, wanaweza hata wakakutafutia neno wakakuambia lina maana ya kuwa na Hummer ilimradi tu wahalalishe wao kumiliki Hummer na kuwa matajiri wa mali. hamuwezi kutumikia Mungu na Mali! hayo ni maneno ya Yesu sio ya Kwangu!!!
...well argued! Should i say more?