Askofu anamiliki HAMMER ya 250million!

Askofu anamiliki HAMMER ya 250million!

Status
Not open for further replies.
Sawa, Mkuu. lakini hakuna anayesema kuwa Mtumishi wa Mungu awe masikini. Tunachosema ni kuwa ni vizuri Mtumishi wa Mungu akawa na Kiasi, hata Mungu mwenyewe ameyasema haya. Kuwa na Kiasi.

Ni Mungu huyu huyu pia aliyesema kawagaie masikini vyote ulivyo navyo, kisha unifuate.

ni Mungu huyu huyu anayesema kuwa ni rahisi kwa Ngamia kupita katika tundu la Sindano kuliko tajiri kuingia Ufalme wa Mungu.
Ni Mungu huyu huyu alieyesema kuwa hamuwezi kutumikia Mabwana wawili. Mungu na Mali.

Ni Mungu huyu huyu ambaye Mwna wake wa Pekee alipokuwa anatafuta wanafunzi wa kumsaidia kueneza neno la Ufalme wa Mungu alichagua watu wa chini kabisa, Wavuvi, Seremala nk. Hakuchagua tajiri miongoni mwa wanafunzi wake. Kuna somo kubwa hapo ambalo Wahubiri wetu wa kileo hawalioni.

Hatusemi Watumisghi wa Mungu wasiwe na Uwezo la hasha. Tunachosisitiza ni kuwa na kiasi, neno ambalo hata Mungu mwenyewe ametuasa nalo.

kama jamii nzima inakubaliana kwamba gari la aina ya Hummer ni gari la kifahari, pamoja na mwenzetu kusema ni trekta la kazi, kwa nini mtumishi wetu wa Mungu asiamue kununua Landrover, Toyota Surf na kadhalika??

Anapanda Hummer la mamilioni anakwenda kuhubiri injili wapi, for Heaven's sake??

After all, si hata Mwana wa Mungu kuna mahali amesema kuwa mnapoenda kuhubiri neno lake msibebe zaidi ya nguo na makubazi mliyovaa bila shaka akiwa na maana ya kuwa na kiasi katika mahitaji yenu? haya ya kwenda kuhubiri na Hummer yameanzia wapi??

Nimalizie tu kwa kusema kuwa kama ni vifungu, basi kila mmoja anaweza kutafsiri kifungu cha Biblia kwa jinsi anavyokiona yeye na ndio maana traditional churches zetu zimekuwa zikiparaganyika na kuanzishwa makanisa binafsi chungu nzima ambayo watumishi wa Mungu wanaoyamiliki wanaweza hata kukusomea vifungu vinavyowaruhusu kuwa na Hummer!

Indeed, Come to think of it, wanaweza hata wakakutafutia neno wakakuambia lina maana ya kuwa na Hummer ilimradi tu wahalalishe wao kumiliki Hummer na kuwa matajiri wa mali. hamuwezi kutumikia Mungu na Mali! hayo ni maneno ya Yesu sio ya Kwangu!!!

...well argued! Should i say more?
 
Siwezi ingia rohoni kwa mtumishi, na nimesema sishabikii ukwasi hata kidogo, ila kama amepewa na hakuwa na gari unataka nini? pengine anatafuta mnunuzi unajuaje? So wakati anasubiri ulitaka apande daladala atukanwe na konda kisha aje kuwahubiria watu amani. Kwa vile ni mtu wa nje huwezi elewa nini kinaendelea kuna kipindi mtumishi anafunga hata kuongea anapunguza hii nimeiona hata RC mission masista wanaita mazoezi ya kiroho, ulitegemea huyu mtumishi atoke kwake na mguu na aje gombania daladala, ndio Yesu hakumiliki lakini kila alipohitaji kitu aliagiza na kilipatikana mf hela ya kodi, chumba cha karamu ya mwisho, samaki na mikate ya kuwapa maskini. But in this era sio watu wote wapo saa zote kujitolea usafiri apande mtumishi ndio kanisa linapotoa au muumini mwenye uwezo anajitolea gari na kumpa, hawajaomba. Jamani na kama unamtumikia Mungu wa kweli, basi hatakupungukia.

Mama Joe, I think tatizo hapa ni aina na uthamani wa gari. punguza hasira
 
Hivi fungu la 10% na sadaka kanisani nani ane kula haswa? Zinaenda wapi kwa Mungu au wapi? Maana utasikia toa ndugu toa ulicho nacho ukikificha Mungu anaona wapi sasa zinako elekea nani anakula au kufaidi pesa za kanisa?

Fungu la Kumi ni kwa ajiri ya mchungaji au watu wanaohudumu madhabahuni (walawi) na si mchungaji peke yake, wajane, yatima na wageni
 
Naomba kuuliza hizi Hummer tanki lake la mafuta linachukua lita ngapi?
mafuta ya laki tatu?
 
Hivi fungu la 10% na sadaka kanisani nani ane kula haswa? Zinaenda wapi kwa Mungu au wapi? Maana utasikia toa ndugu toa ulicho nacho ukikificha Mungu anaona wapi sasa zinako elekea nani anakula au kufaidi pesa za kanisa?

Fungu la Kumi ni kwa ajili ya mchungaji au watu wanaohudumu madhabahuni (walawi) na si mchungaji peke yake, pia inaweza kutumika kwa ajili kuwasaidia wajane, yatima na wageni
Swali: "Biblia inasemaje juu ya kutoa fungu la kumi?"

Jibu: Kutoa fungu la kumi ni jambo ambalo wakristo wengi hung'ang'ana nalo. Katika makanisa mengine kutoa fungu la kumi imesisitizwa kupita kiasi. Wakristo wengi pia hukataa kutii agizo la kutoa sadaka kwa Bwana. Kutoa fungu la kumi au sadaka inahitajika kuwa ni kitendo cha furaha na baraka. Lakini sivyo katika makanisa ya sasa.

Kutoa fungu la kumi ni agizo la agano la kale. Hili lilikuwa sharti la kila mwenye kupata zao au mfugo alete sehemu ya kumi ya pato hekaluni (mambo ya walawi 27:30; hesabu 18:26; kumbukumbu la torati 14;24; mambo ya nyakati ya pili 31:5). Wengine huchukulia ya kuwa fungu la kumi, katika agano la kale ilikuwa kama sehemu ya ushuru uliokuwa ukitolewa kwa ajili ya makuhani na walawi. Agano jipya haiamrishi wala kupendekeza mfumo halali wa kutolea fungu la kumi. Paulo asisitiza kuwa waumini watenge sehemu ya mapato yao kwa ajili ya kusimamia kanisa (wakorintho wa kwanza 16:1-2).

Agano jipya halielezi kiasi cha pato ambacho kinachotakiwa kutengwa kwa ajili ya kusimamia kanisa. (wakorintho wa kwanza 16:2). Kanisa la kikristo leo limechukua kile kiwango cha fungu la kumi kutoka kwa agano la kale na kukisisitiza kuwa ndicho kiwango cha chini cha mkristo kutoa. ijapokuwa agano jipya haitoi kiwango cha kutoa, inaelezea umuhimu na manufaa ya kutoa. Ni watoe sawa na uwezo wao " kulingana na pato lake." Wakati mwingine ina maana ya kutoa zaidi ya fungu la kumi, na mara nyingine kichache kuliko fungu la kumi. Yote hutegemea uwezo wa mkristo mwenyewe na mahitaji ya kanisa. Kila mkristo sharti aombe na kutafuta hekima kutoka kwa Mungu juu ya swala hili (Yakobo 1:5). " kila mtu niatoe kile alicho azimia kutoa kutoka ndani ya moyo wake, si kwa manung'uniko wala kulazimishwa, kwa kuwa Mungu hupenda kwenye kutoa kwa moyo mkunjufu" (wakorintho wa pili 9:7).
 
Asante mtumishi wa Mungu. Hili ndilo tatizo kubwa la dini hizi za asili.
Nilizikimbia kwa sababu hizo hizo. Leo wanawasakama watumishi wa Mungu aliye hai wakisaidiwa na kondoo wao, wakati wachungaji wao hawawezi hata kupeleka wana wao shule na hawako tayari kuwasaidia chochote.

Ndo dini hizi hzi mfano katoliki wanaweka sheria watumishi wao wa mungu wa sio na wajitoe kwenye mambo ya dunia.. ili iwapunguzuie vishawishi.. hivi fikiri wale tenashara(wanafunzi w yesu ) wangekuwa wameoa au wakio oa tayari wangewarudia wake zao wangepata mda na yesu kweli.. wangeweza kuzunguka na yesu from place to place huku wakijua nyumbani wameacha mke na watoto amabo wanahitaji kwenda shule, wanahitaji huduma muhimu.. wamevaa nguo.. je wanaumwa.. nadhani yesu alionyesha wazi hw a preacher or Priest should be..
Luke 6:12-19.. when out of all his disciples he chooses 12 as his Apostles nowing that these should be examples of Preachers. sasa sisi wote ni disciples of Jesus and today's Preachers are the Apostles so do they look any similar to Jesus' apostles
 
Mama Joe, I think tatizo hapa ni aina na uthamani wa gari. punguza hasira
Oh so sorry, labda umenielewa vibaya hamna hasira kabisa kwangu, infact naona ni kichekesho ndo maana kuna symbol nyingi tu nimeweka hapo, this is not personal, kwa sababu mie na hawa watumishi tunakuwa wamoja kama wanasimama ktk Neno period, hivyo ninasema vile ninavyojua kuhusiana na Neno, mengine yote nimeomba mumfate mtumishi mumweleze kuwa this car is too expensive na inachafua mazingira ndo maana nimesema WAPO mission wako wazi kutoa ufafanuzi zaidi ya huu.
Kuiweka hii habari kwenye gazeti za udaku sio njia sahihi yta kupeleka habari kwa muhusika, ni majungu.
 
mama joe mimi pia ni muumini mzuri sana, yapo mengi yananitatiza sana na nimekutana na wachungaji wengi na hata mchungaji wangu, nimekuwa nikiwaauliza maswali mengi sana. tatizo lililopo makanisani kwa sasa ni mazingira ya kutaka utajiri kwa watumishi kwa haraka jambo ambalo linawashtua watu wengi. fikiria mchungaji ana gari la 250 ml na humo kanisani kuna yatima wanakosa chakula na ada za shule na kanisa haliwasaidii. Na mchungaji ananunua gari la 250ml bila kuwajali hao yatima na au wajane. Kweli hapo huoni kuna tatizo? na Huyo mwenye gari hilo anaweza kusema (kwa mfano akiulizwa) anaweza kusema anawasaidia wajane na yatima wangapi?

Ninamfahamu mchungaji mmoja ambaye ni marehemu sasa. amekuwa mchungaji pale temeke kwa zaidi ya miaka 40. amekufa akiwa mwenye amani na alikuwa akiwasomesha yatima zaidi ya mia mbili kuanzia shule za msingi mpaka vyuo.

hawa mnaowatetea mnaweza kutuambia wanasaidia au wamekwisha saidia yatima au wajane wangapi?
 
habari yako haijitoshelezi, weka wazi uyo mtumishi ni yupi, kuficha jina la uyo mtumishi wa mungu linatoa ladha nzima ya habari hii, na wengine wanaweza kukufikiria kua habari yako ni ya kutunga, epuka kuweka habari zenye hamasa bila link inayoeleweka hata picha ulizoweka ni za kutoka kwenye magazeti ya udaku, watafiti wanayaita hayo magazeti, uncredible newspapaer!
 
mama joe mimi pia ni muumini mzuri sana, yapo mengi yananitatiza sana na nimekutana na wachungaji wengi na hata mchungaji wangu, nimekuwa nikiwaauliza maswali mengi sana. tatizo lililopo makanisani kwa sasa ni mazingira ya kutaka utajiri kwa watumishi kwa haraka jambo ambalo linawashtua watu wengi.
Ni kweli hata mie nimekutana nao na bado ninakutana nao wengi tu, ila sio sababu ya kuwaita wooote wezi, pili kumbuka wao pia ni binadamu, wengi wao kama kina Petro hawana maarifa sana ya kidunia kwa hiyo usichoke kuwaambia kwa upole kama wao wanavyokuhubiria injili kuwa hapa kwa uelewa wako mtumishi unakosea. mie ni rafiki mzuri tu wa hawa watu, kwa kweli wala sio haambiliki kama wengi wanavyotaka kuwaonyesha isipokuwa ni kukosa exposure tu mara nyingine na wako tayari kujifunza,
 
mama Joe mtumishi wa Mungu na dini safi hupimwa kwa mstari huu. naomba uutafakari...
Yakobo 1:27 "Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao na kujilinda na dunia pasipo mawaa." Ubarikiwe!

Pia kumbuka kuwa wengi wameingia katika utumishi kama professionals, ndiyo maana tunaona vitu hivi. Swali mtu wa kawaida pengine hata Roho Mtakatifu angeweza kuuuliza, kama kweli wewe ni mtumishi, umeitwa kwa ajili ya kazi shambani nwa BWANA, shamba lina watu wenye mahitaji mengi, hasa wajane na yatima. Na hata kama ungekuwa wewe, usingeweza kununua hata gari ya thamani pungufu ya hizo au hata 50ml na kiasi kinachobaki ukawasaidia wenye shida na matatizo hata kama ni kuwakopesha waanzishe miradi kwa ajili ya kujikimu? kumbuka Yesu Kristo alisema "Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Mathayo 5.17-20..." Ikiwa wasio na Mungu wanawasaidia wajane na yatima, na wewe unayejiita mtumishi husaidii na pengine au badala yake unanunua gari la kifahari, hapo lazima kunakuwa tatizo si la kimwili tu bali pia hata la kiroho.
 
1263623961_humer.jpg

Awali Risasi Jumamosi lilipenyezewa ‘tipu’ juu ya kuwepo kwa Askofu mmoja (jina tunalo), anayemiliki gari aina ya ‘Hammer’ inayokadiriwa kuwa na thamani ya ‘ngawira’ za kitanzania Milioni 250 na ‘ushee’ ambapo uchunguzi ulianza mara moja na kutengeneza kichwa cha habari hii.

Katika ishu hiyo, baadhi ya waumini walilieleza gazeti hili kuwa, gari hilo analotumia Mtumishi huyo huku akivalia ‘krauni’ ya uaskofu, likitiwa mafuta ya shilingi elfu thelathini (30,000) haliwaki hivyo humlazimu kuweka ‘wese’ la shilingi laki tatu (300,000) ili kukamilisha mizunguko yake ya siku moja.

Katika nusanusa ya makachero wetu ilibainika kwamba, mbali na baadhi ya watumishi hao kumiliki magari, majumba na vitu vya kifahari, lakini pia mavazi na mfumo wao wa maisha unawashangaza baadhi ya ‘kondoo’ wanaowaongoza.

Ilisemekana pia kuwa, mmoja wa viongozi hao (naye jina tunalo), amekuwa akitinga madhabahuni na ‘pamba’ za mtoko mmoja zikiwa na thamani ya shilingi laki tano na nusu (550,000) huku akitoa ushuhuda kwa waumini wake kuwa, hayo ni matunda ya kumtumikia Mungu.

1263623961_sylvester_gamanywa.jpg

Katika chimbua chimbua ya hapa na pale, mapaparazi wetu walitonywa pia kuwa, mmoja wa viongozi hao ambaye yeye hujitambulisha kuwa ni Nabii, akiwa katika harakati zozote barabarani hupewa ‘eskoti’ ya msururu wa magari na ving’ora kama ule wa rais wa nchi.

Ernest Madewe, ambaye ni muumini wa moja ya makanisa ambayo kiongozi wake yuko kwenye listi hiyo, aliliambia Risasi Jumamosi kuwa, kondoo wa Mungu wamekuwa ‘wakikamuliwa’ fedha bila kujali umasikini unaowakabili.

Alisema: “Kuna wakati tunajaza fomu maalum za kueleza mali tulizonazo ili kuhakikisha tunatoa fungu la kumi linaloendana na kile tulichonacho bila kujali kuwa kuna baadhi yetu tuko hoi na hatuna kitu.

1263623961_rwakatarebc.jpg

“Suala la sadaka linapaswa kuwa siri ya mtu na Mungu wake, lakini kinachoshangaza, jamaa wanakaba kupita kiasi.”

Baadhi ya maaskofu, wachungaji, walimu na manabii wanaosifika kwa kutoa huduma ya kiroho vizuri ni pamoja na Onesmo Ndegi wa Kanisa la Living Water ‘kanisa la makuti’ lililopo Kawe na Mch. Getrude Lwakatare ‘Mama Lwakatare’ wa Kanisa la Assemblies of God la Mikocheni B, yote ya jijini Dar.

Wengine ni Askofu Zakaria Kakobe wa Kanisa la Full Gospel lenye makao yake makuu pembeni mwa Barabara ya Sam Nujoma, Josephat Mwingira wa Kanisa la Ephata Ministry na Askofu Silvester Gamanywa wa Huduma ya Hakuna Lisilowezekana, nayo ya jijini Dar.

Listi hiyo ndefu inaungwa na Mch. Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufalme na Ufufuo lililopo Ubungo, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ wa Ubungo Kibangu na Nabii GeorDavie wa Kanisa la Ngurumo ya Upako lenye makao yake makuu mkoani Arusha.

shigongo na magazeti yake ya udaku
mmhh! story not balanced how do they run their ministries correctly compare with others ? you should give us vivid example Mr. Editor!!
 
mama Joe mtumishi wa Mungu na dini safi hupimwa kwa mstari huu. naomba uutafakari...
Yakobo 1:27 "Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao na kujilinda dunia pasipo mawaa." Ubarikiwe!
Amen, ninaelewa, na je umeishajiuliza kuwa wanahudumia yatima, wagonjwa na wajane wangapi? all in all wachumi na wasomi mnahitajika kanisani ila kuwafundisha kuwa wauze hiyo gari wainvest ili wapate hela zaidi kusaidia yatima lakini wao kama wao wanaona sawa kwa kutokujua labda, lakini ole wao kama wanajua na wanfanya kusudi, nani mie wakuwahukumu bila kuwaambia hiyo ndo hoja yangu, Ubarikiwe
 
overtime ni zaidi ya mshahara wangu, na ukisema hadi umalize mahitaji yako yote, kweli kuna kitu utapeleka kwa mungu?
Mie kadri ninavyotoa ninapokea maradufu, na pia sina hofu kwani najua mbingu na nchi vyote ni mali ya bwana, na alisema hatanipungukia wala hataniacha, hata nikianguka nitasimama tena ivo sina hofu ya kumtolea mungu mradi nijue ni matumizi sahihi, lakini nikisikia tu watunza fedha au kanisa linalalamika mtumishi anatumia hela ya kanisa vibaya basi nitaacha. Pia tunaenda kiroho kwa hiyo utakuta unachotoa ni kwa kazi maalumu ya mungu sio unatoa tu kama njugu nakubaki unalalamika kama tunavyotozwa kodi serikalini. Tuna amani kabisa.

Nakubaliana na wewe mama joe ila kweli unataka kuniambia utakubali matumizi sahihi ya overtime yako yawe ni Hammer ya 250ml? Kweli? Does this make sense to you?

mama joe mimi pia ni muumini mzuri sana, yapo mengi yananitatiza sana na nimekutana na wachungaji wengi na hata mchungaji wangu, nimekuwa nikiwaauliza maswali mengi sana. tatizo lililopo makanisani kwa sasa ni mazingira ya kutaka utajiri kwa watumishi kwa haraka jambo ambalo linawashtua watu wengi. fikiria mchungaji ana gari la 250 ml na humo kanisani kuna yatima wanakosa chakula na ada za shule na kanisa haliwasaidii. Na mchungaji ananunua gari la 250ml bila kuwajali hao yatima na au wajane. Kweli hapo huoni kuna tatizo? na Huyo mwenye gari hilo anaweza kusema (kwa mfano akiulizwa) anaweza kusema anawasaidia wajane na yatima wangapi?

Ninamfahamu mchungaji mmoja ambaye ni marehemu sasa. amekuwa mchungaji pale temeke kwa zaidi ya miaka 40. amekufa akiwa mwenye amani na alikuwa akiwasomesha yatima zaidi ya mia mbili kuanzia shule za msingi mpaka vyuo.

hawa mnaowatetea mnaweza kutuambia wanasaidia au wamekwisha saidia yatima au wajane wangapi?

VERY GOOD! NO MORE EXPLANATIONS
 
ndo dini hizi hzi mfano katoliki wanaweka sheria watumishi wao wa mungu wa sio na wajitoe kwenye mambo ya dunia.. Ili iwapunguzuie vishawishi.. Hivi fikiri wale tenashara(wanafunzi w yesu ) wangekuwa wameoa au wakio oa tayari wangewarudia wake zao wangepata mda na yesu kweli.. Wangeweza kuzunguka na yesu from place to place huku wakijua nyumbani wameacha mke na watoto amabo wanahitaji kwenda shule, wanahitaji huduma muhimu.. Wamevaa nguo.. Je wanaumwa.. Nadhani yesu alionyesha wazi hw a preacher or priest should be..
Luke 6:12-19.. When out of all his disciples he chooses 12 as his apostles nowing that these should be examples of preachers. Sasa sisi wote ni disciples of jesus and today's preachers are the apostles so do they look any similar to jesus' apostles

kasome biblia vizuri utaone yesu alimponya mkwewe petro. Achana na falsafa za kikatoliki ambazo wala huzijui chimbuko lake
 
Amen, ninaelewa, na je umeishajiuliza kuwa wanahudumia yatima, wagonjwa na wajane wangapi? all in all wachumi na wasomi mnahitajika kanisani ila kuwafundisha kuwa wauze hiyo gari wainvest ili wapate hela zaidi kusaidia yatima lakini wao kama wao wanaona sawa kwa kutokujua labda, lakini ole wao kama wanajua na wanfanya kusudi, nani mie wakuwahukumu bila kuwaambia hiyo ndo hoja yangu, Ubarikiwe

Tatizo asilimia kubwa ya wachungaji wa leo hawashauriki na ukimshauri anaona unamkosoa au unamdharau. na anaweza kukuchafua kupitia madhabahu yake mpaka ukaamua kuwa mlevi. I am a victim of this, trust me!!
 
I hear you PK...and nothing personal....
1.The bottomline is, no one has been robbed of his/her money at gun point!If I am a follower ( meaning i went there of my own free-will) and I contributed in facilitating Kakobe to ride expensive wheels while im treading on my two feet, then the likes of Kakobe should be left alone to face judgement at the end of time.

2.Lets not engage in trivialities - a hummer, ferrari,bentley - it doesnt matter.If it is a status car - its us who gives that interpretation maana mimi binafsi I dont give a hoot kama mtu anaendesha gari gani, anavaa nini au anaishi kwenye nyumba gani.Attention seeker... let him get the attention- so what i would say.

3.Before reading this thread and your post, i never even knew that Kakobe ana baiskeli let alone a Hummer maana kwangu he is just Kakobe doing his business ( yes running a church is a business dont raise eye-brows hahah) kama ambavyo mimi ni Wos naendesha my own business!

its true haja mrob mtu, umeota kwa moyo wako mwenyewe.. but he had an influence on you mpka ukatoa sadaka ryt.. ??? huyu ni mchungaji wa mungu should be kioo kwa congregation yake.. hivi angenunua Rav4 au normal gari kama ya watu wakawaida alaf hiyo rest of the money ingetumika kwenye mambo mengine kwani ujumbe usingefika vile vile...
 
mama Joe mtumishi wa Mungu na dini safi hupimwa kwa mstari huu. naomba uutafakari...
Yakobo 1:27 "Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao na kujilinda na dunia pasipo mawaa." Ubarikiwe!

Pia kumbuka kuwa wengi wameingia katika utumishi kama professionals, ndiyo maana tunaona vitu hivi. Swali mtu wa kawaida pengine hata Roho Mtakatifu angeweza kuuuliza, kama kweli wewe ni mtumishi, umeitwa kwa ajili ya kazi shambani nwa BWANA, shamba lina watu wenye mahitaji mengi, hasa wajane na yatima. Na hata kama ungekuwa wewe, usingeweza kununua hata gari ya thamani pungufu ya hizo au hata 50ml na kiasi kinachobaki ukawasaidia wenye shida na matatizo hata kama ni kuwakopesha waanzishe miradi kwa ajili ya kujikimu? kumbuka Yesu Kristo alisema "Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Mathayo 5.17-20..." Ikiwa wasio na Mungu wanawasaidia wajane na yatima, na wewe unayejiita mtumishi husaidii na pengine au badala yake unanunua gari la kifahari, hapo lazima kunakuwa tatizo si la kimwili tu bali pia hata la kiroho.

ndugu yangu hapa ndipo wanaojiita watumishi w Bwana wanapoingia chaka(wanapotea njia) kwa kuzingatia ulafi na ubinafsi kwa kulitajia jina la bwana eti njoo kwa bwana uwe tajiri. yes hatukatai je yeye huo utajiri anaupata kwa njia gani? only one SADAKA za watu yeye badala ya kuzitumia hata kwa kusaidia maskini na yatima,anatia puani tena kwa kujilimbikizia,hatukatai mtu kuwa na gari,but gari ya aina gani je utukufu wa Mungu wewe kutembelea250m wakati kuna waumini wanakuja church bila hata ya kitafunwa?
 
But jambo la msingi ni nini kazi ya kueneza injili?ni kuhubiri dar es salaam na kujenga hapo majumba ya kifahari ya Ibada? tena sababu dar kunalipa kuna hela?kuna tofauti gani na anaehama toka Iringa kuja kufanya biashara Dar ili kufuata soko? so first thought ya wahubiri wetu wa siku hizi sio penye kiu ya neno la Mungu bali ni penye watu wenye hela,very good Marketing research!!
 
kasome biblia vizuri utaone yesu alimponya mkwewe petro. Achana na falsafa za kikatoliki ambazo wala huzijui chimbuko lake
kuoi hapo nimekwambia kwa wale walio oa.. hawakuwarudia wake zao.. kuna sehemu bibblia inaonesha petro alimrudia mke wake... wewe kanisa lako chimbuko lake ni wapi???
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom