Askofu Bagonza ajiepushe na upindifu wa kimantiki unaoweza kuzaa taharuki ya kijamii bila uhalali

Kaweke kambi bagamoyo wiki mbili tu uone wanavyomiminika kwenye semina zinazofadhiliwa na NGOs baada ya mama kufungua nchi.
 
Ngumu sana kuutetea uovu, jambo dogo sana umetumia muda mwingi na maneno mengi kulielezea na ndani yake ukaandika ujinga , uongo na uzandiki.

Kaida za kiusuli za jambo ovu huwa lina chain, yaani mlolongo. Mfano kwetu sisi Waislamu, Leo hii, ukimuelekeza mtu sehemu mbaya, mfano umekutana na mtu akakuomba umeulekeze kijiwe Cha pombe kipo wapi, na unajua kabisa huyu ataenda kunywa hiyo pombe. Aisee yule akifanya uovu na wewe unasehemu yako ya uovu,sababu wewe unakuwa umeshiriki katika kumuelekeza hata kama wewe hujafika wala hujanywa hicho kilevi.

Hali ilivyo mpaka hao wote ulio jinasibu kuwababadua wote wanahukumiwa ushoga,ndiyo maana hukumu ya mashoga inamkumba mfanyaji na mfanywaji. Wote adhabu yao ni kifo.

Sasa acheni ujuaji katika mambo yasiyo hitaji ujuanj bali akili na kutafakari na kuchukua hatua.
 
Yaani kuna mlawiti homofiliki, mlawiti asiye homofiliki, homofiliki mlawiti, na homofiliki asiye mlawiti. Hizi ni kada nne za watu, lakini Bagonza haonekani kuzitofautisha.
Naomba utuwekee ushahidi wa mtu mwenye kuwatamani watu wa jinsia yake na hafanyi hivyo vitu.
 
Lakini, leo hii sayansi inatwambia kuwa kuna viumbe havina mgawanyo huo wa ME na KE. Mfano ni minyoo. Kwa hiyo, mwandishi wa Agano la Kale hakuwa na habari ya ukweli huu wa viumbe wasio na mgawanyo wa jinsia ya ME na KE.
Muandishi una upeo mdogo sana katika kung'amua mambo, suala la kimaadili linawahusu viumbe wenye akili na siyo hayawani. Kwahiyo hapakuwa na haja ya maandiko hayo kumuanisha mnyoo, sababu ni katika hayawani.

Jikote katika kumuelezea kiumbe mwenye utashi na akili, kumjadili mnyoo katika suala hili ni kuonyesha uchachefu wako wa maarifa na kupotosha Ile kweli. Jifunze kuweka kila kitu mahala pake.
 
Upindifu wa kimantiki, yaani logical fallacy, ni kosa la kimantiki ambapo mwongeaji hutunga hoja inayokiuka misingi bora ya usanifu wa hoja na uendeshaji wa mijadala.
Hii misingi si imewekwa na mwanadamu, unaweza kunihakikishia uborawa misingi hiyo mpaka ukaifanya kuwa marejeo yako ? Jibu huwezi Sasa kwanini uturejeshe katika dhaifu ya kimantiki ?
 
I miss you mama Amon


USSR
 
Mfano, sauti iko katika tabaka la vitu vinavyosikika, wakati harufu iko katika tabaka la vitu vinavyonuka. Lakini, mara nyingi utasikia watu wanasema, "nasikia harufu ya chakula."
Hiki ulichokiandika kinaonyesha ni kwa namna gani mtoa mada huna Elimu na haya mambo. Lugha au usahihi wa lugha haupimwi kimantiki kama unavyofanya wewe au kwa mtindo wa falsafa unataka kuuleta wewe, ndiyo maana hapa umekosea, lugha usahihi wake ni kwa vile ilivyo sikiwa na wale wazungumzaji wa asili wa lugha husika.

Sisi Waswahili tumesikika tukisema ya kuwa "Nasikia harufu ya kitu Fulani" Kiswahili hivi tuko sahihi sababu ndiyo imepokelewa hivi na imesikika hivi kwa Waswahili na tunaelewana.

Kingine unaposema harufu ipo katika tabaka la vitu vinavyo Nuka, hapa umepindisha maana aidha kwa ujinga au kwa makusudi siyo kila harufu inanuka, inayo Nuka ni Ile harufu mbaya na inayonukia ni Ile harufu nzuri hivi ndivyo sisi Waswahili muweko wetu wa lugha na maana uko hivi. Huwezi kumkuta mswahili akisema "Kitu Fulani kina nuka" akamaanisha harufu nzuri bali ni harufu mbaya.
 
Hujasoma hoja yangu.
NImeunga mkono wazo la kubana haki za mahomofiliki walawiti.
NIkatetea haki za mahomofilia wasio walawiti.
Bagonza hatofautishi haya mawili.
Ndio ugomvi wangu na hoja yake
 
Sisi Waswahili tumesikika tukisema ya kuwa "Nasikia harufu ya kitu Fulani" Kiswahili hivi tuko sahihi sababu ndiyo imepokelewa hivi na imesikika hivi kwa Waswahili na tunaelewana.
Ndugu yangu, category mistake ni kosa linalokusaidia kuelewa kiwango duni cha maarifa cha mzungumzaji.
Usilipigie upate. Tusaidiane kusahihisha.
 
upinde unatumia nguvu kubwa sana kutetea upinde wenzako.bladfaken
 
Kifupi pamoja na porojo za andiko na nukuu za hao walionukuliwa. Neno moja ni hakika Ushoga ni dhambi, laana na HAIKUBALIKI.
Kama mtu anatumika ili kujenga hoja za mashoga wakubalike ni Big No
 
Kifupi pamoja na porojo za andiko na nukuu za hao walionukuliwa. Neno moja ni hakika Ushoga ni dhambi, laana na HAIKUBALIKI.
Kama mtu anatumika ili kujenga hoja za mashoga wakubalike ni Big No
Kuna mambo ya msingi nataka uyaelewe. Moja huwezi kumtambua shoga mpaka akwambie au ajitangaze. Kwa hiyo, tunajadili mashoga wapi? Tunaogopa mashiga wapi? Hebu tufikiri kama watu wenye ubongo aisee...
 
Hii misingi si imewekwa na mwanadamu, unaweza kunihakikishia uborawa misingi hiyo mpaka ukaifanya kuwa marejeo yako ? Jibu huwezi Sasa kwanini uturejeshe katika dhaifu ya kimantiki ?
Kwa ufupi kuna kanuni nne zinazoongoza fikra sahihi za kibindamau:
1. Law of identity
2. Law of excluded middle
3. Law of non-contradiction
4. Law of sufficient reason.

Mengine yote yanaanzia hapo.
Jielimishe
 
Kama kila mtanzania atalazimika kufuata mlolongo wote huo kulaumu au kusifia kitu basi tutakumbwa na tatizo la vichaa wenye elimu
 
Mama Amon, naomba umu acknowledge mtunzi wa hii makala tafadhali.
 
Sikubaliani na ushoga ila itoshe kusema ww Mama Amon ni gifted sana..
Hapa labda Kiranga na barafu ndio mnaweza bishana
Inside10 kuna pointi umeongea, hoja zilizopo kwenye hii mada ni za upeo wa juu mno wa uelewa, wanaJF wenye uwezo wa kuelewa na kujadili vitu kama hivi walishaacha kushiriki mijadala JamiiForums, amebaki Kiranga peke yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…