Askofu Bagonza ajiepushe na upindifu wa kimantiki unaoweza kuzaa taharuki ya kijamii bila uhalali

Askofu Bagonza ajiepushe na upindifu wa kimantiki unaoweza kuzaa taharuki ya kijamii bila uhalali

Mfano, kwenye Safina ya Nuhu tunaambiwa kuwa Nuhu aliagizwa kuweka kila kiumbe kwa kuzingatia kanuni ya ME na KE.

Lakini, leo hii sayansi inatwambia kuwa kuna viumbe havina mgawanyo huo wa ME na KE. Mfano ni minyoo. Kwa hiyo, mwandishi wa Agano la Kale hakuwa na habari ya ukweli huu wa viumbe wasio na mgawanyo wa jinsia ya ME na KE.

Na hii maana yeke ni kwamba, wanateolojia wanaofanya udadavuzi kwa kuanzia kwenye Biblia wanahitaji kuelimishwa na wanabayolojia katika suala ya asexual reporoduction. Biblia haina mamlaka katika jambo hili.

Sote tunakamilishana kimaarifa, na hivyo kuna haja ya kuunganisha nguvu katika kufanikisha mradi wa kujenga imani ya jamii yenye utulivu, haki na amani.

Tujenge hoja bila mihemuko wala taharuki.
Asante Mama Amon , kwenye Safina ya Nuhu, aliweka binadamu, wanyama, ndege na viumbe hai wa juu ya uso wa dunia ambao watakuwa destroyed by water, lakini hakuweka organisms kama minyoo, unicelular, protozoa, flagelata na kina paramecium kina bacteria kwasababu hawawi destroyed by water.

Kwenye hili la ushoga na ulawiti, linahitaji uelimishaji umma mkubwa kuwa kuna watu wanazaliwa na hormonal disorder kwa mwanaume kuzaliwa na homoni za like na mwanamke kuzaliwa na homoni za kiume, ni ulemavu kama ulemavu mwingine wowote, tujifunze kuikubali hii hali na kuishi nao positively.

Ulawiti na usagaji ni tabia chafu tuu katika jamii yetu kwa kufanya sexual perversion, kuna wanaume wengi tuu sio mashoga lakini wanafanya mapenzi kinyume cha maumbile na kuna wanawake wengi tuu wanalawitiwa!. Tena kundi jipya la wadada wanajiita wanaondanga wakipata danga nene, wanatoa offer ya vitu adimu kwa dhana hilo ndilo hitaji la wanaume wengi ambalo hawalipati kwenye ndoa zoo au kwa wapenzi wao, hivyo wao kujiover ili wawakamate.

P
 
Sawa...

Japo sijui alikuwa anaongea akiwa wapi, lakini kama alichokiongea kililenga umma wote kwa ujumla wake, bado nasema hakuna kosa kwa sababu ujumbe wa kuwa "ushoga ni kosa la kimaadili" katika jamii yetu umefika na kueleweka vyema...

Hilo la kutafuta "makosa ya kimantiki" ni la kwenu wana taaluma mnapotaka kupeleka paper mbele ya jopo la wana - taaluma ili kufanyiwa assessment ya PhD yako...

Jamii inahitaji ujumbe ulio straight forward ktk lugha rahisi na ya kueleweka..

Mfano;

✓ Iambie jamii kuwa wizi ni mbaya na hatari ili mtu aepuke hata kufikiri tu kuchukua kitu kisicho chake...

AU

✓ Au, waambie straight forward kumuua (kumwaga) damu ya mwenzako ni dhambi mbele ya Mungu na ni kosa la kimaadili pia. Usiingize mambo ya sijui kuna kuua bila kukusudia ama kukusudia..

Hayo ni ya baadae huko mbeleni kama ikilazimu kuchunguza tukio fulani la mauaji. Lakini all in all, uuaji kwa ujumla wake ni kosa...!!

Sioni kosa la ujumbe wa Askofu Bagonza. Sisi wengine tumemwelewa...
Umeongea Vyema,mleta mada katumia lugha za darasani Sana badala aongee uhalisia wa hoja,akiulizwa swali anaanza kuchomekea vi terminologies vigumuvigumu ili tu kumchanganya muuliza swali na Lengo kuu likiwa ni kuutetea ushoga.Tukubaliane tu ushoga Ni kinyume na maadili yetu haya mambo ya kuanza kuhalalisha kwamba kazaliwa na hormones Basi mabazazi wote watasema wamezaliwa na hormones husika na ushoga utakuwa halali kwenye jamii...
 
HUwezi kuwatofautisha.
Hapo ndipo upiga ramli wa kuwavisha joho ya ushoga watu unapokosa nguvu.
KUna vipimo vya kisayansi vtumike.
Nukta
Kama huwezi kuwatofautisha naona huu mjadala huishie hapa, kwasababu huwezi kujua yupi ni muharibifu na yupi sio, vyema wote watazamwe kwa jicho la ziada.

Askofu Bagonza yupo sahihi.
 
Kumjadili mleta hoja badala ya kujadili hoja ni dalili za kufilisika kimawazo
Daaah wewe dada/MAMA huwa unanivutia SANA yaani kuna muda unajihisi duniani hukusoma kabisa kiukweli navituwa sana na maandiko YAKO yanafanya ubongo ufikirie SANA. Naomba uwe unaendelea kutuletea mada kama hizi binafsi huwa narudia mara tatu mpaka tano ILI nikuelewe MUNGU hakika wazazi wako hawakupoteza pesa😂🙏🙏
 
ushoga Ni kinyume na maadili yetu
Hivi maneno kama vile "ushoga, usagaji, uchicha, ubasha, ulawiti, wizi, ubakaji" nk ni maneno yaliyoletwa na wageni ili kuongelea tabia zilizoletwa na wageni hapa nchini kwetu?

Let us own our problems and solve them by ourselves without blaming a strawman!

Can't we think loundly?

Nionavyo mimi, hoja hii ina matatizo:

1. Imani na tabia zote zilizoletwa Afrika na wageni katika Afrika ni haramu kimaadili.
2. Imani na tabia hii inayoitwa "X" imeletwa na wageni katika Afrika.
3. Kwa hiyo, imani na tabia "X" ni haramu kimaadili.

Hoja hii sio sahihi kwa sababu mbili.

Kwanza, kuna dini za Kikristo na Uislamu zipo Afrika na hazijakataliwa kwa sababu ya madai kwamba zililetwa na wageni.

Na pili, misamiati asilia ya lugha za Afrika kabla ya wageni kufika inataja tabia kama vile wizi, uwongo, ulawiti, usagaji, na kadhalika, kama tabia zilizokuwepo Afrika kabla ya wageni hao.

Kwa hiyo, sio sahihi kuwabebesha lawama wageni kwa mabaya yetu.

Hebu tujenge hoja badala ya kupayuka.
 
kuna wanaume wengi tuu sio mashoga lakini wanafanya mapenzi kinyume cha maumbile na kuna wanawake wengi tuu wanalawitiwa!.
Mkuu Pashal, the seasoned journalist, my simple question to you: How do you know this, where is your incontrovertible evidence, what is the magnitude of the problem, and does that magnitude bestow to this matter the status of a "social problem" that deserves public attention? Remember: verification is the midwife of journalism.....
 
ccm mna mambo ya hovyo kabisa!
Wamefanya nini? Napendekeza tujielekeze kwenye mada badala ya kujielekeza katika hoja za ama-uccm-au-uchadema, zisizo na mantiki.

Kwa mujibu wa maudhui ya social media ya mwaka 2020, maswali yanayopaswa kupatiwa majibu kutoka kwa Lissu na wafuai wake ni mawili hasa:

(1) Je, 2D:4D ratio ya vidole vya Lissu ni kubwa kuliko moja? (Yaani kidole cha pili ni kirefu kuliko kidole cha nne?)

(2) Kama jawabu ni ndiyo, 2D:4D ratio iliyo kubwa kuliko moja inamaanisha kwamba mhusika ni shoga? (Yaani, kidole cha pili kikiwa ni kirefu kuliko kidole cha nne, ukweli huo unamaanisha kwamba mhusika ni shoga?

Sasa tujielekeze kwenye mada.

1676277025221.png
 
Hebu niambie;

- Lini na wapi, Lissu aliwahi kuteuliwa kuwa mwakilishi wa mashoga Afrika? hapa napenda nione na hiyo picha nyingine ya Lissu unayodai unayo.
Sijaongelea jambo hili. Usipotoshe.

Hoja hapa sio mashoga wako upande wa CCM wala upande wa CHADEMA.

Bali hoja ilianzia kwenye vidole vya Lisu siku ile akiwa Kayanga, Karagwe Kagera.

Wafitini wa mambo wakasema kidole cha pili cha Lissu ni kirefu kuliko kidole cha nne cha Lissu. Yaani ukitafuta 2D:4D ratio ya vidole vyake unapata namba kubwa kuliko moja.

Kwa maoni yao, watu wente 2D:4D ratio iliyo kubwa kuliko moja ni mashoga.

Hivyo, wakabeba hoja hiyo mitandaoni. Kwa hiyo maswali yanayohitaji majibu ni mawili:

(1) Je, ni kweli kwamba 2D:4D ratio ta vidole vya Lissu ni kubwa kuliko moja?

(Yaani, ni kweli kwamba kidole cha pili cha Lissu ni kirefu kuliko kidole chake cha nne?)

(2) Na kama 2D:4D ratio ya Lissu ni kubwa kuliko moja, takwimu hiyo inamaanisha kuwa Lissu ni shoga?

(Yaani, ni kweli kwamba kama kidole cha pili cha Lissu ni kirefu kuliko kidole chake cha nne, hiyo maana yake ni kwamba Lissu ni shoga?)

1676276853025.png
 
Hii misingi si imewekwa na mwanadamu, unaweza kunihakikishia uborawa misingi hiyo mpaka ukaifanya kuwa marejeo yako ? Jibu huwezi Sasa kwanini uturejeshe katika dhaifu ya kimantiki ?
Nyongeza: kanuni za kimantiki ni kielelezo cha kanuni za maumbile. Sio zao la akili ya mtu.

Mfano, law of excluded muddle kimantiki inasomeka hivi:

A statement what is the case can not be true and false at the same time and in the same respect.

Yaani:

An entity can not possess and fail to possess a given attribute at the same time and in the same sense
 
Nyongeza: kanuni za kimantiki ni kielelezo cha kanuni za maumbile. Sio zao la akili ya mtu.

Mfano, law of excluded muddle kimantiki inasomeka hivi:

A statement what is the case can not be true and false at the same time and in the same respect.

Yaani:

An entity can not possess and fail to possess a given attribute at the same time and in the same sense
Safi kabisa. Tamko Mantiki kwa kiasili ni chenye kitamkwa,lakini kiistilahi ni chenye kuleta maana. Mantiki imekuwa fani pweke yaani taaluma Fulani ambayo Ina misingi yake na wapo watu waliasisi fani hiyo.

Unaposema ni kielelezo Cha kanuni za kimaumbile, lazima mantiki iepukane na makosa, kitu ambacho mantiki haina Ina makosa mengi kutokana na misingi kwayo imemili taaluma hiyo.

Huwa nawauliza kati ya maneno na mantiki kama fani kipi kilianza ?

Hii kanuni nani aliiweka ? Usahihi wake uko wapi ? Unaweza kunionyesha ?
 
Kwani hizo kanuni zimebumiwa au zimegunduliwa??
Hizo kanuni zimebuniwa ndiyo maana ukifatilia, utaona definitions nyingi katika Falsafa, Fizikia na taaluma nyingine nyingi Zina makosa sana Bali Zina uongo mwingi. Sababu watu walikuwa wanahoji tangu zamani na kupatia vile vile.
 
Hizo kanuni zimebuniwa ndiyo maana ukifatilia, utaona definitions nyingi katika Falsafa, Fizikia na taaluma nyingine nyingi Zina makosa sana Bali Zina uongo mwingi. Sababu watu walikuwa wanahoji tangu zamani na kupatia vile vile.
Duh! Unataka kusema kuwa, mfano, THE LAW OF NON-CONTRADICTION imebuniwa na watu?

Hapana!


It says: a thing can not be and fail to be at the same time.

Hii ni kanuni ya maumbile ndugu!


Jielimishe!
 
Safi kabisa. Tamko Mantiki kwa kiasili ni chenye kitamkwa,lakini kiistilahi ni chenye kuleta maana. Mantiki imekuwa fani pweke yaani taaluma Fulani ambayo Ina misingi yake na wapo watu waliasisi fani hiyo.

Unaposema ni kielelezo Cha kanuni za kimaumbile, lazima mantiki iepukane na makosa, kitu ambacho mantiki haina Ina makosa mengi kutokana na misingi kwayo imemili taaluma hiyo.

Huwa nawauliza kati ya maneno na mantiki kama fani kipi kilianza ?

Hii kanuni nani aliiweka ? Usahihi wake uko wapi ? Unaweza kunionyesha ?
Nitaendelea kutumia mfano wa THE LAW OF NON-CONTRADICTION

Kimantiki iko hivi:

A claim P can not be true and false simultaneously and in the same sense.

Kiontolojia inasomeka hivi:

An entity cannot have attribute X and fail to have attribute X at the same time.


Umeona tunavyotoka ktk ngazi ya mantiki hadi ngazi ya metafizikia?

Kanuni za metafizikia hazijabuniwa na mtu. Zinagunduliwa.

Hope this helps
 
Swali kwa mama amoni ; Katika kueleza na bainisha Hoja ya msingi katika andiko lako hili , unatumia methodolojia gani ambayo ,kwanza inakubalika katika muktadha wa kifalsafa na hata dhana za kitaaluma ili kufikia hitimisho uliloweka ?!
 
Back
Top Bottom