Askofu Bagonza ajiepushe na upindifu wa kimantiki unaoweza kuzaa taharuki ya kijamii bila uhalali

Ndugu yangu, category mistake ni kosa linalokusaidia kuelewa kiwango duni cha maarifa cha mzungumzaji.
Usilipigie upate. Tusaidiane kusahihisha.
Hapa tunajadili Elimu bibie siyo maoni yetu binafsi, unajua kama lugha inahukumu ? Labda kama hujihusishi na na mambo ya lugha. Shida bandiko lako umeliandika kihisia na falsafa na si uhalisia.

Hapo hakuna kosa ndiyo maana hutakuta andiko hata Moja la lugha linatia dosari kauli hiyo.

Sasa unapigia upatu wewe ambae umeamua kupindisha ukweli kwa makusudi.
 
Kwa ufupi kuna kanuni nne zinazoongoza fikra sahihi za kibindamau:
1. Law of identity
2. Law of excluded middle
3. Law of non-contradiction
4. Law of sufficient reason.

Mengine yote yanaanzia hapo.
Jielimishe
Hujajibu swali nililo kuuliza.
 
Hujasoma hoja yangu.
NImeunga mkono wazo la kubana haki za mahomofiliki walawiti.
NIkatetea haki za mahomofilia wasio walawiti.
Bagonza hatofautishi haya mawili.
Ndio ugomvi wangu na hoja yake
Nimekusoma vizuri nikakuelewa.

Sasa utawatofautisha vipi hao mahofolia wasio walawiti, na wale mahofolia ambao ni walawiti, hasa wanapokuwa kwenye public?

Hawa wote watakuwa na muonekano wa aina moja, kwasababu huo ulawiti hufanywa sirini, mlawiti hana alama usoni.

Hivyo, kitendo chochote cha kuwaacha hao mahofolia [ bila kujali kama ni walawiti au wasio walawiti] wazidi kuenea kwenye jamii, ndio utakuwa mwanzo wa kuiharibu jamii yetu, binafsi nataka makundi yote ya mahofolia yasiachwe, yabanwe.

Bado niko upande wa Askofu Bagonza.

NOTE.

Matumizi yako ya picha ya Bagonza na Lissu ndio unazidi kuiharibu mada yako, unaitoa kwenye usomi na kuipeleka kwenye siasa.

Matokeo yake wachangiaji watakuja na muelekeo wa kisiasa na kupoteza mantiki ya hoja yako ya awali, unapoleta mada kama hizi jitahidi uwe impartial, kwasababu kama ni ushoga, hata CCM upo, na picha zao zipo nyingi mitandaoni.
 
Nimesoma yote. Ila kwa nini utumie ubongo wako kuona negative tu? Kukumbatiana inaweza kuwa ishara ya upendo. PSYCH-K
 
Sasa utawatofautisha vipi hao mahofolia wasio walawiti, na wale mahofolia ambao ni walawiti, hasa wanapokuwa kwenye public?
HUwezi kuwatofautisha.
Hapo ndipo upiga ramli wa kuwavisha joho ya ushoga watu unapokosa nguvu.
KUna vipimo vya kisayansi vtumike.
Nukta
 
Nimesoma yote. Ila kwa nini utumie ubongo wako kuona negative tu? Kukumbatiana inaweza kuwa ishara ya upendo.
Nakubaliana nawe.
Nami hoja yangu ni kwamba Watanzania wengi wana wepesi wa kutumia fallacy of association kutengeneza sleepery slop argumentszinazojadili ushoga, wakati hilo sio tatizo la kijamii kwetu hapa Tanzania.
 
Sorry, hujaona ninachotaka ukione kwenye picha hiyo. For sure, picha hii ni mwafaka.
Natumia picha halisi kunyesha uzoba wa kifikra tulio nao Watanzania.
Bahati mbaya hata mwanazuoni kama Bagonza ametumbukia kwenye mtaro huo.
 
ila nawe umetumia neno la kidikiteta la kuwafunga watu midomo "taharuki".
Neno "taharuki sio neno la kidikteta.
NImetafsiri "moral panic" ambayo ni maneno rasmi katikamijadala kama hii.
Bagonza anaelewa vema sana.
 
Huyu Askofu, tangu alipounganan na yule Askofu wa Konde ambaye ni mwizi na kuwa na matatizo mengi, simuweki maanani sana.
Ni mchumia tumbo kama wengine.
 
Upindifu wa kimantiki kwenye public discourse ni kosa kubwa.
Kauli mfagio (unsupportee claims) kwenye midahalo ni kosa kubwa.
Sawa...

Japo sijui alikuwa anaongea akiwa wapi, lakini kama alichokiongea kililenga umma wote kwa ujumla wake, bado nasema hakuna kosa kwa sababu ujumbe wa kuwa "ushoga ni kosa la kimaadili" katika jamii yetu umefika na kueleweka vyema...

Hilo la kutafuta "makosa ya kimantiki" ni la kwenu wana taaluma mnapotaka kupeleka paper mbele ya jopo la wana - taaluma ili kufanyiwa assessment ya PhD yako...

Jamii inahitaji ujumbe ulio straight forward ktk lugha rahisi na ya kueleweka..

Mfano;

✓ Iambie jamii kuwa wizi ni mbaya na hatari ili mtu aepuke hata kufikiri tu kuchukua kitu kisicho chake...

AU

✓ Au, waambie straight forward kumuua (kumwaga) damu ya mwenzako ni dhambi mbele ya Mungu na ni kosa la kimaadili pia. Usiingize mambo ya sijui kuna kuua bila kukusudia ama kukusudia..

Hayo ni ya baadae huko mbeleni kama ikilazimu kuchunguza tukio fulani la mauaji. Lakini all in all, uuaji kwa ujumla wake ni kosa...!!

Sioni kosa la ujumbe wa Askofu Bagonza. Sisi wengine tumemwelewa...
 
Neno "taharuki sio neno la kidikteta.
NImetafsiri "moral panic" ambayo ni maneno rasmi katikamijadala kama hii.
Bagonza anaelewa vema sana.
Taharuki kwa tafsiri ya kimtaani mi keosi, si neno la mjadala ni neno la kumshutumu mtu kwa kutaka watu wachanganyikiwe na kusababisha vurugu, neno hili lilikuwa maarufu wakati wa mwendazake dhidi ya wabaya wao na nchi za kidikiteta dhidi ya wapinga udikiteta.
 
Ndio maana nilipata mashaka na sababu hasa ya kuanzisha hili bandiko lako, mwanzo uliliegemeza kielimu, lakini sasa naanza kuona unapoteza muelekeo na kwenda kwenye siasa, jambo ambalo bado nakusisitiza UNAKOSEA.

Na, unaposema unatumia picha halisi kuonesha uzoba wa waAfrica, sijui kwanini hasa utumie picha ya aina/mtu mmoja kuonesha huo uzoba, napata mashaka na nia yako, hasa nikizingatia wapo wengine, toka vyama vingine, wanaostahili kutolewa mfano kama huo wa uzoba tena waliojipambanua kwa uwazi zaidi, lakini unawaficha.

Hebu niambie;

- Lini na wapi, Lissu aliwahi kuteuliwa kuwa mwakilishi wa mashoga Afrika? hapa napenda nione na hiyo picha nyingine ya Lissu unayodai unayo.

- Inawezekana vipi mtu unayemwita mwakilishi wa mashoga Afrika akawa na familia?
 
Sorry, picha hii ni mwafaka.
Tena kuna picha nyingine inamwinyesha Lissue akiwa anaonekana kuteuliwa kuwa mwakilishi wa Mashoga Afrika.
Natumia picha halisi kunyesha uzoba wa kifikra tulio nao Watanzania.
Mmh! Kumbe ndiye mwakilishi wao?🤔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…