Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wacha waje waanze kutukanaChawa sijui watajibu hoja gani? Zaidi ya matusi tu
Kwanini? Na wewe unaandika haya ukiwa nje ya JF au ndani?Dah! Ila JF ina wajinga aisee!!! Ptuuu
Hoja nzito hizi...Na Askofu Bagonza
1. Rushwa
Rushwa bandarini ndiyo imesababisha bandari ifanywe inachofanyiwa. Wakiishapeana rushwa, serikali inakosa mapato, mizigo inachelewa, inapotea, na bandari limekuwa pango la majizi.
Swali ni je, kila penye rushwa tuuze? Tubinafsishe? Tukabidhi sekta binafsi?
2 . Umoja na Utaifa
Mjadala umeonyesha, wanaodai wanaujenga/kuutetea umoja na utaifa, ndio wanaubomoa. Wanaoonekana kuubomoa, ndio wanaujenga. Bandari imeujeruhi umoja na utaifa wetu. Hii ina gharama mbeleni. Tumejuana, tuishi kwa tahadhari.
3 . Udini na Siasa Zetu
Viongozi wetu wana dini zao. Sitamani kuchagua kiongozi asiye na dini. Tatizo tunalo viongozi wa dini. Tunawakosoa viongozi wa dini ileee na kupongeza wa dini zetu. Au tunanyamaza mpaka tupigwe sindano ya kupongeza badala ya kushauri.
Inapendeza kumkosoa na kumshauri kiongozi wa dini yako japo haizuiwi kumkosoa wa dini isiyo yako.
4. Ujuzi wa Sheria na Uchumi.
Ajabu Wanasheria walioongea tukaelewa ni wachache sana. Walio wengi ujanja wao unaishia Kisutu.
Wanauchumi wetu ujanja wao unaishia Kariakoo.
Mkataba huu hawauelewi na wakiuelewa hawatuelezi tukaelewa. Huu ni ufa wa hatari.
5. Bunge
Hili lingebinafsishwa kabla ya bandari. Walichoongea bungeni sicho wanachoongea mitaani na kwenye baa. Wanamdanganya rais kuwa wanamuunga mkono wakati wamebeba mishale ya kumwangamiza.
6. Serikali
Mjadala na tabia za watu vimeonyesha serikali hii si ya rais Samia hata kama kaiteua yeye. Hii ni mchanganyiko wa serikali zilizopita. Ina utii uliogawanyika - kiapo kimoja Chamwino na vingine huko makaburini, Msufini, na Butiama.
Serikali bila “Uwajibikaji wa pamoja” ni sawa na genge la wasela. Ufa huu unadai tuanze upya.
7 . Rushwa part 2.
Katika Mjadala wa Bandari tumesikia malalamiko ya rushwa za aina tatu: Wanaonufaika na uzembe wa bandari wakikazana kukwamisha mkataba;

8. Rais Wetu
Rais SSH ni wetu sote. Ni muhimu kama taifa kumkinga na mipasuko inayotokana na mjadala huu. Kuna maisha baada ya mjadala wa bandari. Yeye analo jukumu la kutuongoza sote na makundi yote mpaka tuvuke. Subira itatufundisha kuliko haraka.
9 . Miafaka yetu
Mjadala huu umejeruhi miafaka yetu na kufukua baadhi ya makaburi. Baadhi ya makaburi tumekuta marehemu hawajaoza.
Katiba, maridhiano, Muungano, maelewano ya kidini, uhuru wa maoni na mamlaka ya wananchi bila bunge ni mambo muhimu sana katika kuziba nyufa.
10. Upinzani wetu
Mjadala unaonyesha aina mpya ya upinzani. Ndani ya chama tawala na serikali kuna upinzani mkali dhidi ya suala la bandari. Hii ni afya kwa nchi lakini hatari kwa utawala. Vyombo vyetu vijifunze kutotumia nguvu kupambana na maoni.
11. Bandari na Mipaka yetu
Bandari ya DSM ni mpaka kama ilivyo Tunduma, Namanga, Sirari, Mtukula na kwingineko. Kuharakisha mizigo bandarini wakati inaenda kukwama mipakani haisaidii. Kero za barabarani na rushwa zake haziwezi kumalizwa na DP World.
Mipaka yetu yote inanuka kwa uzembe, rushwa na ufisadi. Tusisafishe uso (bandari ya DsM) tukasahau makalio (mipaka mingine inayokwamisha mizigo ya nchi za jirani)
Nawashukuru wooote wanaochangia kwa hoja na kutuelimisha tulio wajinga wa sheria, uchumi na mikataba ya kimataifa
Chawa sijui watajibu hoja gani? Zaidi ya matusi tu
Kwakweli no 6🙌🤝Mimi namb 6
Ameeleza vizuri hajaegemea upande mmoja !! Amepiga pande zote !!Na Askofu Bagonza

💯Kimsingi maelezo yote kuanzia 1 hadi 11 yanajitosheleza.
Kila mmoja atimize wajibu wake kwa kujirekebisha pale palipoguswa kulingana na hoja za askofu.
Hatuna ukamilifu, kila siku tunajifunza na kujirekebisha.
ni PHd holder huyo, sio mpiga soga kama wale wa tv iman.Huyu baba ni Mwanafalsafa wa wakati huu. KITUO
Kagonga palepale kwenye donda 😂😂Kwakweli no 6🙌🤝
KKKT wakawa wajanja wakamkwepa kimtindo kuwa Kiongozi wao wa Kitaifa. Na yeye aliisoma ramani mapema, HAKUGOMBEA!Huyu baba ni Mwanafalsafa wa wakati huu. KITUO
Namba 12 ,kwa nini tusibinafsishe kwwanza ikulu kabla ya bandari kwa kuwa hata kujikuna tu ikulu inahitaji mwekezajiNimeielewa vizuri sana Namba 5
Taarifa zilizopo ni kwamba walimtimua kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya KKKT ambacho kinapiga kura na wajumbe wake wanakidhi vigezo vya kupigiwa kura. Lakini habari zilizopo ni kwamba pamoja na hilo alipata kura 15 ambazo zilihesabika kwamba zimeharibika soma hapa: Uchaguzi KKKT: Askofu Bagonza aibuka na mambo matatuKKKT wakawa wajanja wakamkwepa kimtindo kuwa Kiongozi wao wa Kitaifa. Na yeye aliisoma ramani mapema, HAKUGOMBEA!
Bandari ya DSM ,nimpaka kama ilivyo mipaka mingi kama tunduma ,siraliWanauchumi wetu ujanja wao unaishia Kariakoo.[emoji23]
Kumbe aligombea? Ahsante kwa masahihisho na nimeisoma hiyo habari. Ukweli ni kwamba Askofu Dk. Bagonza sio mtu mzuri wa kuongoza watu au taasisi. Kimsingi, mtu anayeamini yeye ni bora na mzuri kuliko wengine HASTAHILI hata kukaa na watu wengine. Askofu Dk. Shoo na Maaskofu na Wajumne wa Halmashauri Kuunya KKKT naamini wametumia busara kubwa kumuengua! Ni maoni yangu.Taarifa zilizopo ni kwamba walimtimua kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya KKKT ambacho kinapiga kura na wajumbe wake wanakidhi vigezo vya kupigiwa kura. Lakini habari zilizopo ni kwamba pamoja na hilo alipata kura 15 ambazo zilihesabika kwamba zimeharibika soma hapa: Uchaguzi KKKT: Askofu Bagonza aibuka na mambo matatu
Pole sana bagonza, tumeona huko kwako mambo yamekuwa si mambo, unaelezeaje kuhusu hilo?Na Askofu Bagonza
1. Rushwa
Rushwa bandarini ndiyo imesababisha bandari ifanywe inachofanyiwa. Wakiishapeana rushwa, serikali inakosa mapato, mizigo inachelewa, inapotea, na bandari limekuwa pango la majizi.
Swali ni je, kila penye rushwa tuuze? Tubinafsishe? Tukabidhi sekta binafsi?
2 . Umoja na Utaifa
Mjadala umeonyesha, wanaodai wanaujenga/kuutetea umoja na utaifa, ndio wanaubomoa. Wanaoonekana kuubomoa, ndio wanaujenga. Bandari imeujeruhi umoja na utaifa wetu. Hii ina gharama mbeleni. Tumejuana, tuishi kwa tahadhari.
3 . Udini na Siasa Zetu
Viongozi wetu wana dini zao. Sitamani kuchagua kiongozi asiye na dini. Tatizo tunalo viongozi wa dini. Tunawakosoa viongozi wa dini ileee na kupongeza wa dini zetu. Au tunanyamaza mpaka tupigwe sindano ya kupongeza badala ya kushauri.
Inapendeza kumkosoa na kumshauri kiongozi wa dini yako japo haizuiwi kumkosoa wa dini isiyo yako.
4. Ujuzi wa Sheria na Uchumi.
Ajabu Wanasheria walioongea tukaelewa ni wachache sana. Walio wengi ujanja wao unaishia Kisutu.
Wanauchumi wetu ujanja wao unaishia Kariakoo.
Mkataba huu hawauelewi na wakiuelewa hawatuelezi tukaelewa. Huu ni ufa wa hatari.
5. Bunge
Hili lingebinafsishwa kabla ya bandari. Walichoongea bungeni sicho wanachoongea mitaani na kwenye baa. Wanamdanganya rais kuwa wanamuunga mkono wakati wamebeba mishale ya kumwangamiza.
6. Serikali
Mjadala na tabia za watu vimeonyesha serikali hii si ya rais Samia hata kama kaiteua yeye. Hii ni mchanganyiko wa serikali zilizopita. Ina utii uliogawanyika - kiapo kimoja Chamwino na vingine huko makaburini, Msufini, na Butiama.
Serikali bila “Uwajibikaji wa pamoja” ni sawa na genge la wasela. Ufa huu unadai tuanze upya.
7 . Rushwa part 2.
Katika Mjadala wa Bandari tumesikia malalamiko ya rushwa za aina tatu: Wanaonufaika na uzembe wa bandari wakikazana kukwamisha mkataba;
Serikali bila “Uwajibikaji wa pamoja” ni sawa na genge la wasela. Ufa huu unadai tuanze upya.
8. Rais Wetu
Rais SSH ni wetu sote. Ni muhimu kama taifa kumkinga na mipasuko inayotokana na mjadala huu. Kuna maisha baada ya mjadala wa bandari. Yeye analo jukumu la kutuongoza sote na makundi yote mpaka tuvuke. Subira itatufundisha kuliko haraka.
9 . Miafaka yetu
Mjadala huu umejeruhi miafaka yetu na kufukua baadhi ya makaburi. Baadhi ya makaburi tumekuta marehemu hawajaoza.
Katiba, maridhiano, Muungano, maelewano ya kidini, uhuru wa maoni na mamlaka ya wananchi bila bunge ni mambo muhimu sana katika kuziba nyufa.
10. Upinzani wetu
Mjadala unaonyesha aina mpya ya upinzani. Ndani ya chama tawala na serikali kuna upinzani mkali dhidi ya suala la bandari. Hii ni afya kwa nchi lakini hatari kwa utawala. Vyombo vyetu vijifunze kutotumia nguvu kupambana na maoni.
11. Bandari na Mipaka yetu
Bandari ya DSM ni mpaka kama ilivyo Tunduma, Namanga, Sirari, Mtukula na kwingineko. Kuharakisha mizigo bandarini wakati inaenda kukwama mipakani haisaidii. Kero za barabarani na rushwa zake haziwezi kumalizwa na DP World.
Mipaka yetu yote inanuka kwa uzembe, rushwa na ufisadi. Tusisafishe uso (bandari ya DsM) tukasahau makalio (mipaka mingine inayokwamisha mizigo ya nchi za jirani)
Nawashukuru wooote wanaochangia kwa hoja na kutuelimisha tulio wajinga wa sheria, uchumi na mikataba ya kimataifa
Chawa sijui watajibu hoja gani? Zaidi ya matusi tu
Pole sana bagonza, tumeona huko kwako mambo yamekuwa si mambo, unaelezeaje kuhusu hilo?